Kilauea: Volkano yarusha mawe makubwa angani Hawaii, Marekani

The ash plume erupting from Hawaii's Mount Kilauea, and some "ballistic blocks" it has spewed

Chanzo cha picha, Reuters/Getty Images

Maelezo ya picha, Volkano hiyo ilirusha mawe makubwa mamia ya mita juu angani, mawe ambaye yanaweza kufikia uzani wa tani kadha

Mlipuko mkubwa ulitokea katika volkano ya Kilauea katika jimbo la Hawaii nchini Marekani na kuzua wasiwasi zaidi eneo hilo.

Mlipuko huo ulirusha majivu futi 30,000 (9,100m) juu angani. Aidha, ulirusha juu mawe makubwa wa kilo kadha, na baadhi inakadiriwa kuwa yanaweza kuwa na uzani wa tani kadha.

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa kumi na robo alfajiri saa za huko.

Wanasayansi wanasema bado kuna uwezekano mlipuko mwingine unaweza kutokea.

Watu waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha kufuatilia volkano hiyo waliokuwa kwenye mbuga ya taifa ambapo kunapatikana volkano hiyo wamehamishwa.

Shirika la Jiolojia la Marekani linasema mawe ya ukubwa wa hadi 60cm (2ft) yalionekana hatua kadha kutoka kwenye shimo la mlipuko wa volkano hiyo.

Lakini walitahadharisha kwamba huenda mambo yakawa mabaya zaidi.

Fissure on Kilauea volcano, 13 May

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Matope moto kutoka kwa volkano hiyo yamekuwa yakimwagika kisiwani

"Wakati wa milipuko ambayo imesababishwa na mvuke, mawe ya ukubwa wa hadi 2m yanaweza kurushwa pande zote umbali wa 1km au zaidi," shirika hilo lilisema.

"Mawe hayo yanaweza kuwa na uzito wa kilo kadha hadi tani kadha. mawe madogo yanaweza kurushwa mbali, kilomita kadha."

Tangu milipuko ya volkano ilipoanza kutokea eneoi jipya Kilauea, matope yenye moto yamekuwa yakimwagika na kuharibu mamia ya nyumba eneo hilo na kulazimu maelfu ya watu kuhamishwa.

Hawaii National Guard soldiers wear masks to protect themselves from volcanic gases in Pahoa during ongoing eruptions of the Kilauea Volcano in Hawaii, U.S., May 17, 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi walitumia mavazi maalum kujikinga dhidi ya majivu na gesi za volkano

Tahadhari ya kiwango cha juu zaidi imetolewa, na marubani wa ndege wameonywa kuhusu hatari inayoweza kutokana na 'wingu' la majivu ya volkano hiyo.

Shirika la Jiolojia la Marekani lilikuwa limeonyesha kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko mkubwa eneo hilo.

Hii ni baada ya kina cha 'ziwa la matope moto' kwenye vilkano hiyo kuonekana kupungua na kuongeza uwezekano wa maji yanayopatiukana chini ya ardhi kukutana na matope hayo moto chini ya ardhi, maji yakijaribu kujaza mianya inaoachwa wazi na kupungua kwa matope hayo.

Shirika la huduma za dharura Hawaii liliwatahadharisha watu walio maeneo yaliyoathiriwa na majivu hayo kusalia ndani ya nyumba zao.

Kina cha ziwa la matope moto kwenye volkano hiyo kimeshuka kwa zaidi ya 200m

Chanzo cha picha, US Geological Survey

Maelezo ya picha, Kina cha ziwa la matope moto kwenye volkano hiyo kimeshuka kwa zaidi ya 200m
Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kilauea ni moja ya volkano tano ambazo bado hulipuka katika kisiwa cha Hawaii.

Ni moja ya milima inayolipuka sana duniani na imekuwa ikilipuka mara kwa mara ingawa hakujakuwa na mlipuko mkubwa kwa miaka zaidi ya 30.

Mlipuko wa mwisho mkubwa eneo hilo ulitokea 1924.

Hata kabla ya mlipuko huo wa Alhamisi, majivu kutoka kwa volkano hiyo yalikuwa yanaweza kuonekana kutoka kituo cha kimataifa cha anga za juu (ISS).

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Hawaii volcano eruption map