Je, Unafahamu faida za kiafya za kuvua viatu nje unapoingia ndani ya nyumba?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Manal Mohammed
- Nafasi, My Conversation
Mama yangu alikuwa alikutalazimisha tufuate sheria hii: kutovaa viatu ukiingia nyumbani. Hakujali ni nani aliyekuwa anatutembelea iwe ni mgeni au jirani ilikuwa ni lazima uvue viatu kabla ya kuingia nyumbani.
Nilipokuwa mdogo nilidhani mama yangu alikuwa mkali . Lakini nilipoanza kujifahamu niligundua sio tu kwa ajili ya kuzingatia usafi. Lengo la mama lilikuwa ni kudumisha afya na usafi.
Usafi huonekana wazi wazi. Lakini linapokuja suala ya viatu kinachokuwa hatari ni uchafu usioonekana unaoganda chini ya viatu.
Viatu vinavyovaliwa katika mazingira ya nje ya nyumba huwa vinabeba vijidudu na bakteria ambao husababisha changamoto za kiafya.
Hebu tafakari viatu unavyovaa hukanyaga sehemu ngapi? si msalani barabarani, hospitali na pia kwa bustani ambazo zimenyunyiziwa dawa za wadudu wa kukabiliana na magugu.
Kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Arizona kilichoko Marekani, 96 % ya viatu vinabeba baktria inayojulikana kama coliform ambayo hupatikana kwa kinyesi.
Na cha kustaajabisha zaidi, ni kwamba asilimia 27% ina bakteria ya E coli ambayo husababisha magonjwa hatari zaidi kwa binadamu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati baadhi ya aina za bakteria ya E. coli si hatari kwa binadamu, aina nyingine ya bakteria ni ya Shiga, ambayo husababisha kuhara damu na inaweza kupelekea hali hatarishi ijulikanayo kama hemolytic uremic syndrome—maradhi yanayoweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi na hatimaye kusababisha kifo.
Watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wako katika hatari zaidi kutokana na mfumo wao wa kinga kutokomaa kikamilifu, na pia kwa tabia ya mara kwa mara ya kuweka mikono midomoni.
Hata hivyo, E. coli siyo kirusi pekee kinachoweza kuwepo katika mazingira ya nyumbani, hasa sebuleni.
Viatu navyo huweza kubeba bakteria wa Clostridium, wanaosababisha kuhara na wakati mwingine madhara makubwa, pamoja na Staphylococcus aureus, wakiwemo wale wa aina sugu kama MRSA—bakteria wanaostahimili dawa ambao wanaweza kusababisha maambukizi ya ndani ya ngozi, homa ya mapafu, au hata maambukizi hatari ya damu.
Sio vijidudu pekee
Hatari za kiafya haziishii kwa bakteria peke yake.
Viatu pia hubeba kemikali hatarishi na vichochezi vya mzio.
Utafiti umebaini kuwa viatu vinavyovaliwa nje ya nyumba huweza kubeba mabaki ya dawa za kuua wadudu, dawa za kuua magugu, na metali nzito kama chuma , vitu ambavyo ni hatari kwa afya, hasa kwa watoto wadogo na wanyama wa kufugwa nyumbani.
Risasi, ambayo hupatikana kwa kiasi kikubwa katika vumbi au udongo wa maeneo ya mijini, ni sumu hatari inayoweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto na kusababisha matatizo ya kiakili ya kudumu.
Zaidi ya hayo, viambato kama chavua vinaweza kushikamana kwenye nyayo za viatu, na hivyo kuchochea mzio na matatizo ya mfumo wa upumuaji hata ndani ya nyumba, mahali panapopaswa kuwa salama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata zaidi ya kutia wasiwasi, lami za kuzibia barabara huwa na kemikali hatarishi zinazoweza kusababisha saratani.
Utafiti uliofanyika Marekani ulibaini kuwa kemikali hizi huweza kuingia ndani ya nyumba na kujikusanya kwenye vumbi la nyumbani, mara nyingine kwa viwango vinavyofikia mara 37 ya vile vinavyopatikana nje.
Na nani huathirika zaidi?
Watoto na wanyama wa kufugwa.
Watoto hutambaa, hucheza sakafuni, na mara nyingi huweka mikono yao mdomoni.
Wanyama nao hulamba nyayo zao baada ya kutembea kwenye sehemu zilizochafuliwa.
Kuvaa viatu vya nje ndani ya nyumba kunaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya kueneza kemikali hizi hatarishi.
Sakafu safi, nyumba salama
Kwa kuzingatia ushahidi huu, kanuni ya mama yangu ya kuondoa viatu unapoingia nyumbani haionekani kuwa ya ajabu tena.
Kwa hakika, ni mojawapo ya hatua rahisi na zenye ufanisi mkubwa katika kulinda afya ya familia.
Kwa kuvua viatu mlangoni, hauzuii tu uchafu na madoa kwenye sakafu, bali pia unapunguza sana uwezekano wa kuingiza vijidudu na kemikali hatari ndani ya nyumba.
Hatua hii si ngumu kutekeleza.
Tengeneza eneo mahsusi la kuwekea viatu karibu na mlango.
Unaweza pia kuweka rafu, kikapu, au hata kuandaa viatu vya ndani kwa ajili ya wageni.
Ingawa huenda kuomba watu wavue viatu kikawa kigeni mwanzoni, ni muhimu kutambua kuwa hata jambo dogo kama kuingia nyumbani linaweza kuwa chanzo cha hatari zisizoonekana kwa urahisi.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid