Unajua mara ngapi unapaswa kuosha miguu yako yenye mamilioni ya bakteria?

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Author, Jasmin Fox-Skelly
  • Nafasi,

Baadhi ya watu husugua miguu yao kila siku, huku wengine wanapendelea kumwagia maji miguu inatosha.

Lakini, je, unatunza miguu yako vya kutosha?

Unapoingia bafuni kuoga, ni kawaida kuna sehemu ambazo huziangazia zaidi na hata kuna baadhi ya viungo havipati maji ya kutosha au hupendelei kuosha.

Hata hivyo, wataalamu wanasisitiza kuwa miguu inahitaji umakini wa kutosha.

Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza (NHS) na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) wanashauri kuosha miguu kila siku kwa sabuni na maji.

Sababu moja ya kufanya hivyo ni kuzuia harufu mbaya.

Nyayo za miguu zina tezi nyingi za jasho, zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya mwili.

Ingawa jasho lenyewe halina harufu, lina mchanganyiko wa virutubishi vinavyoweza kuleta bakteria kwenye ngozi yako.

"Mguu, hasa kati ya vidole, ni mazingira ya unyevu, joto na giza, ambayo hufanya kuwa sehemu bora kwa vijidudu kuishi," anasema Holly Wilkinson, mhadhiri wa uponyaji wa majeraha katika Chuo Kikuu cha Hull. Zaidi ya hayo, wengi wetu huvaa viatu na soksi, hivyo hufungia unyevu ndani.

Hii ikiwa mojawapo ya sababu kwanini unapaswa kuosha miguu yako.

Kwa mujibu wa wataalamu, miguu yetu inajumuisha aina nyingi za bakteria na fangasi.

Walakini kwa sababu nyayo za miguu yako zimejaa vijidudu, hiyo haimaanishi kwamba lazima iwe na harufu au kwamba kuna chochote cha kuwa na wasiwasi.

Kama kawaida, sio idadi tu, lakini aina ya bakteria ambayo ni muhimu.

Wakati mwingine, bakteria aina ya Staphylococcus ndiyo husababisha harufu ya miguu kwa kutengeneza kemikali zinazozalisha harufu mbaya.

Katika utafiti mmoja, watafiti waligundua kuwa kuosha miguu mara mbili kwa siku hupunguza sana idadi ya bakteria, wakati wale wanaoosha mara moja kwa siku au baada ya siku mbili, wanakutana na bakteria wengi zaidi.

Pia unaweza kusoma:

Katika utafiti mmoja wa 2014, watafiti walichunguza miguu ya watu 16 na kugundua kuwa asilimia 98.6% ya bakteria waliopo kwenye nyayo walikuwa Staphylococci.

Hata hivyo, si kila bakteria kwenye miguu husababisha matatizo.

Baadhi yao ni muhimu kwa afya ya ngozi yetu.

Bakteria kama Staphylococcus huunda asidi zinazohusika na harufu ya miguu.

Hata hivyo, kusafisha miguu mara kwa mara husaidia kuzuia magonjwa ya ngozi kama vile maambukizo ya fangasi, hasa mguu wa mchezaji, ambao husababishwa na fangasi zinazokua kwenye mazingira ya unyevu.

Kulingana na Zeichner, shida ya kawaida ni ukuaji wa fangasi, ambayo ni maambukizo ya kuvu ya juu ya ngozi kwenye miguu.

Kuvu wanaosababisha fangasi hustawi katika mazingira ya joto, giza na unyevunyevu - ndiyo sababu hali hii huathiri zaidi nafasi zilizo katikati ya vidole vya miguu.

Weka eneo hili safi na kavu na utaepukana na fangasi ambazo zinapendelea mazingira hayo.

Dalili kubwa ya fangasi ni muwasho unaokulazimisha kujikuna, harufu mbaya ya muozo katika miguu, na kumomonyoka ama kulika kwa ngozi yenye fangasi.

Pia kuvuja kwa majimaji yenye kuteleza na harufu nzito, maumivu au kuhisi kuchomachoma baada ya kuchubuka na pia mara nyingine kuhisi joto kwenye eneo lililovamiwa na fangasi.

Fangasi husambaa na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kugusana na vitu vilivyotumiwa na mwenye vimelea aina ya fangasi.

Chanzo cha picha, Gorka Olmo/BBC

Maelezo ya picha, Fangasi husambaa na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kugusana na vitu vilivyotumiwa na mwenye vimelea aina ya fangasi.

"Miguu ina uwezekano mkubwa wa kuambukizwa kwa sababu kuna bakteria nyingi sana huko, na pia ikiwa una nyufa au majeraha kwenye miguu yako, inachukua muda kupona kuliko maeneo mengine ya mwili," anasema Wilkinson. "Katika hali kama hiyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba ikiwa una jeraha, vimelea vinaweza kuingia kwenye jeraha hilo, kujaa na kukua."

Pia, miguu isiyosafishwa inaweza kuwa na bakteria hatarishi kama Staphylococcus au Pseudomonas, ambayo inaweza kuingia mwilini kupitia majeraha, na kusababisha maambukizo makubwa.

Hii ni hatari zaidi kwa watu wenye kisukari, ambao wanakutana na majeraha yasiyopona haraka.

Wataalamu wanashauri kwamba watu wenye kisukari wanapaswa kuosha miguu yao kila siku ili kuepuka maambukizo.

Kwa hivyo, ni muhimu sana kwamba watu walio na ugonjwa wa kisukari kuzingatia usafi wa miguu yao, kwa sababu wako katika hatari zaidi ya kupata maambukizi kwa sababu hiyo, "anasema Wilkinson.

"Ikiwa una ugonjwa wa kisukari, unaweza kuwa na uharibifu wa mishipa kwenye miguu yako, hivyo huwezi kuhisi miguu yako vizuri," anasema Wilkinson. "Kitendo cha kuosha tu hukuruhusu kuangalia vizuri miguu yako ikiwa kuna michubuko midogo au ukavu ambao unaweza kuchangia kuwa na maambukizi."

Kwa sababu hiyo, Wilkinson - na mashirika ya misaada kama vile Diabetes UK - inapendekeza kwamba wagonjwa wa kisukari kuosha miguu yao kila siku.

Njia za kukabiliana na fangasi

Hata hivyo, kwa watu wasiokuwa na matatizo ya kiafya, kuosha miguu kila baada ya siku mbili ni ya kutosha.

Lakini ni muhimu kuhakikisha miguu inakauka vizuri baada ya kuosha ili kuepuka fangasi na maambukizo mengine.

"Pia ni muhimu kutosugua sana au kuchubua ngozi kwenye miguu," anasema Zeichner. "ngozi sugu hutokea kwasababu ya kusuguliwa kupitiliza kila siku. Lakini kwa hakika hulinda miguu kutokana na mazingira. Kuondoa gamba la nyayo huondoa ulinzi huo."

Pia kuna wasiwasi kwamba sabuni zina kuwa na kinga ya bakteria zinaweza kuvuruga usawa dhaifu wa vijidudu kwenye ngozi, na kuua spishi zenye faida na kuruhusu kuibuka kwa aina ngumu zaidi, za vidudu ambazo ni sugu dhidi y adawa za kupambana na bakteria.

Hatimaye, mfumo wetu wa kinga unahitaji kupewa changamoto kwa kadiri fulani na vijidudu ili kufanya kazi yake.

Ikiwa hatuwezi kuwasiliana na mkondo wa kutosha wa bakteria na virusi utotoni, basi miili yetu haijifunzi jinsi ya kujibu vizuri mashambulizi ya bakteria.

Wataalamu wengine wanaamini kuwa kuoga au kuoga mara kwa mara kunaweza kuwa na madhara kwako kwa sababu hii.

ff

Chanzo cha picha, Gorka Olmo/BBC

Kwa hivyo hiyo inatuacha na swali la kudumu, ni mara ngapi tunapaswa kuosha miguu yetu? Jibu linategemea kwa kadiri fulani juu ya mtu binafsi.

"Kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, wanashauriwa asilimia 100% kuosha miguu yako kila siku," anasema Wilkinson.

"Lakini ikiwa huna hali yoyote ya kiafya, basi mtaalamu wa ngozi anashauri kwamba kila siku kadhaa ni zaidi ya kutosha ili kudumisha usafi, bila kuondoa mafuta mengi ya asili kwenye ngozi yako."

Hata hivyo, Wilkinson anadokeza kwamba ikiwa wewe ni mtu anayependa kukimbia au kufanya mazoezi, basi ni wazi utahitaji kuosha miguu yako mara kwa mara kuliko mtu ambaye hana shughuli nyingi.

Pia sio tu mzunguko wa kuosha ambao ni muhimu pia.

Jinsi ya kuosha na kukausha miguu yako pia ina athari za kiafya.

"Watu wengi wanafikiri kwamba ikiwa unaoga na kuacha tu maji yatiririke, kwamba hiyo ni kuosha miguu, lakini sivyo - unahitaji kuosha miguu yako kwa maji ya sabuni," anasema Wilkinson.

Hata hivyo, kulingana na Dan Baumgardt, GP na mhadhiri wa sayansi ya neva na fiziolojia katika Chuo Kikuu cha Bristol nchini Uingereza, jambo muhimu zaidi analosisitiza kwa wagonjwa ni kuhakikisha unakausha miguu yako vizuri.

"Unapokuwa na unyevu au unyevu katikati ya vidole vinavyoruhusiwa kubaki tu katika mazingira ya joto, hapo ndipo unakuwa na uwezekano wa kuendeleza mambo kama vile maambukizi mengine ya fangasi," anasema Baumgardt.

Matibabu ya dawa za fangasi za kupaka zilizo katika mtindo wa poda pia ni muhimu.

Hakikisha pia ukiwa una tatizo hili kiasi cha kufikia kupata vidonda miguuni, unapata chanjo ya tetenasi.

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid