Fahamu meli ya uchunguzi yenye nguvu zaidi kati ya Yuan Wang-5 ya China na Dhruv ya India

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuwasili kwa meli ya uchunguzi ya satelaiti ya China Yuan Wang-5 katika Bahari ya Hindi kumekuwa kukifuatiliwa kwa karibu na nchi jirani ya India.
Wizara ya mambo ya nje ya India ilikataa kutoa maoni moja kwa moja ikiwa meli hiyo ilikuwa tishio kwa India. Wakati huo huo, kwa kuzingatia aina ya meli hiyo ya China, mashirika ya kijasusi ya India yanaiangalia kwa mashaka fulani.
Vyombo vya habari vya kimataifa, vyombo vya habari vya India na Sri Lanka vimechapisha habari na taarifa nyingi kuhusu meli hii ya China katika wiki za hivi karibuni. Ukweli wa kwamba meli hiyo ina vifaa gani na uwezo wake wa kisayansi na kiufundi haujulikani kikamilifu.
Watu wengi wameanza kutafuta kwenye mitandao ya kijamii ikiwa kuna meli nchini India yenye vifaa sawa na meli hiyo ya China. Jibu ni 'ndiyo' kwa baadhi ya sehemu. Walakini, hakuna habari nyingi juu ya meli hiyo.
Meli ya ``Yuanwang-5'', inayotambuliwa kama `` Chombo cha utafiti na Kufuatilia Satelaiti'' nchini China, kina uwezo wa kufuatilia satelaiti na kurusha makombora.
Hali kadhalika meli kama hiyo, iliyotolewa kwa huduma ya majini nchini India mwaka jana inaitwa Dhruv. Ina uwezo wa kutambua mapema na kutoa tahadhari dhidi ya meli za kivita za makombora zinazoingia baharini.
Pia, Dhruv imeundwa kugundua ufuatiliaji wa anga na satelaiti katika anga ya India na kuarifu Shirika la Utafiti wa Anga na Ulinzi la India.
Yuanwang meli katika aina nyingi
Neno Yuanwang linamaanisha "muonekano wa mbali" au "kuona mbali" kwa Kichina.
Serikali ya China imezitaja meli zinazofuatilia anga ya bahari kuwa ni Yuan Wang.
China ina meli nne za daraja la Yuan Wang. Kila meli ina antena za kufuatilia setilaiti, rada na vifaa vya skana vilivyounganishwa kwenye vyombo tofauti. Meli hizo zimetambuliwa kuwa ni Yuanwang 3, Yuanwang 5, Yuanwang 6 na Yuanwang 7. Duniani, ni nchi pekee zikiwemo China, Marekani, Urusi na Ufaransa ndizo zilizo na uchunguzi wa satelaiti na uchunguzi wa angani. Marekani ina meli 23 kama hizo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya China inasema imeunda chombo cha anga za juu cha Yuanwang ili kuwasaidia wanaanga wake sehemu mbalimbali duniani ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa anga za juu wa Shenzhou.
Kwa hivyo, ingawa meli hizi zilijengwa mapema mwaka 1977, zilitumika baada ya mwaka 1986 kufuatilia Mpango wa Uzinduzi wa Satellite wa Kimataifa kutoka mikoa mingine ya bahari nje ya eneo lao la maji. Wakati huo meli za Yuanwang 1 na 2 zilitumika.
Mwaka 1995 meli mbili za aina ya Yuanwang 3 zilitaifishwa. Baada ya hayo, mwaka 1999, chombo cha anga za juu cha Yuanwang 4 kilijengwa ili kufuatilia programu ya kurusha satelaiti ya China. Meli mbili zaidi za aina ya Yuan Wang zilijengwa baadaye mwaka wa 2007. Katika mfululizo huu, meli za Yuanwang 5 na 6 ziliundwa mahususi kwa ajili ya mradi wa Shenzhou na kupelekwa sehemu mbalimbali za bahari.
Katika suala hilo, meli za uchunguzi za Yuan Wang zinatumwa kwenye "Bahari Tatu" ili kusaidia katika ukaguzi wa satelaiti kabla ya kuzinduliwa.
Meli za Yuanwang zinavyovuka mipaka ya bahari

Chanzo cha picha, PMD SRI LANKA
Hasa, vyombo hivi hutumwa katika Bahari ya Pasifiki ya Magharibi, Bahari ya Pasifiki ya Kusini, Bahari ya Hindi ya Magharibi ya Australia, na Bahari ya Atlantiki ya Kusini.
Aina hii ya meli ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye bahari mwaka 1999. Kisha ilitumwa kwa Bahari ya Pasifiki. Yuanwang 4 ilitumwa kwenye Bahari ya Hindi na bandari ya Fremont, Australia. Yuanwang 3 ilitumwa Durban na kisha Bahari ya Atlantiki.
Yuanwang 4 ilitia nanga mwaka 2007 wakati meli ya mizigo iliyokuwa imebeba makaa ilipogongana nayo. Baada ya moto katika bodi libadilishwa kuwa ya mafunzo ya kulenga meli. Wakati wa majaribio mwaka 2010, meli iliyolengwa iliharibiwa na kombora lililorushwa kutoka katika meli ya kivita ya DF21 iliyotia nanga katika bandari ya Jiangyin.
Hapo awali, mwaka 2007, Shirika la Viwanda la Kujenga Meli la China lilijenga meli za kizazi cha tatu za Yuanwang 5 na Yuanwang 6.
Yuanwang 5 imebuniwa kufuatilia setilaiti.
Meli ya ya Yuanwang 6 imeundwa kusimamia uwekaji wa nyaya za chini ya bahari zinazotumika katika huduma ya mtandao. Meli hii inaweza kuzalisha umeme kwa jiji lenye wakazi wapatao laki tatu.
Njia za meli za Yuanwang 7, Yuanwang 21 na 22 zinasimamiwa na Waangalizi wa Satellite za majini wa China. Ingawa meli kama vile Yuanwang 21 na 22 hutumika kubeba makombora ya Long March ya China, mienendo na huduma zake huwekwa kwa siri sana.
Lengo ni nini?
Miongoni mwao, meli ya uchunguzi na utafiti ya setilaiti ya Yuan Wang-5 ya China kwa sasa imetia nanga kwenye bandari ya Hambantota inayosimamiwa na kampuni ya Kichina nchini Sri Lanka. Huko, meli imepewa ruhusa ya kujaza mafuta na kufanya shughuli za matengenezo kwa muda wa wiki moja.
Urefu wake ni mita 220, upana ni mita 25.2. Meli hiyo ina uwezo wa kubeba tani elfu 25 za bidhaa na inaweza kusafiri kwa kasi ya juu ya 37 km / h.
Meli hii ina mchanganyiko wa maumbo yanayopatikana katika meli nyingine nyingi. Ingawa China haijarusha roketi za aina ya Shenzhou angani katika miezi au wiki za hivi karibuni, China haijaeleza madhumuni ya safari ya Yuanwang 5. Kimsingi sio meli ya kivita. Lakini ni ubongo wa meli za kivita na zinaweza kutoa nguvu za kiteknolojia.
Kwa kadiri nchi inavyohusika, inasemekana tangu awali kwamba hii ni safari ya baharini ya majaribio ya kawaida
Dhruva ya India - Ni yapi yaliyoangaziwa?

Chanzo cha picha, INDIAN NAVY
Ingawa China ina aina kadhaa za meli katika safu ya Yuanwang, INS Dhruv ndio meli pekee nchini India iliyo na mifumo ya tahadhari ya satelaiti na makombora kwa mahitaji yake ya ulinzi.
Meli hiyo ilitaifishwa mnamo Septemba 2021. Ilijengwa yote na Shirika la Kujenga Meli la Hindustan kwa ushirikiano na Shirika la Utafiti wa Ulinzi wa India (DRDO) na Shirika la Utafiti wa Kiufundi la India (NTRO).
Meli hiyo imewekwa Visakhapatnam na inaendeshwa kwa Jeshi la Wanamaji la India. Hapo ndipo jukwaa lake na kituo cha udhibiti kinapatikana. Meli hiyo inaendeshwa na timu ya pamoja ya Jeshi la Wanamaji la India, NTRO na DRDO.
Meli hiyo ina vifaa vya kisasa vya rada (AESA) vilivyotengenezwa na DRDO. Inaiwezesha kuchanganua masafa mbalimbali, kufuatilia satelaiti za kijasusi zinazofuatilia India na kufuatilia majaribio ya makombora yaliyofanywa katika eneo la bahari la India.

Chanzo cha picha, Getty Images
Meli hiyo inayoitwa INS Dhruv, ina uwezo wa kufuatilia kwa masafa marefu makombora yenye silaha za nyuklia. Imeundwa kukabiliana na ongezeko la tishio la kombora la balestiki la nyuklia katika eneo la Indo-Pasifiki. Dhruv pia ina uwezo wa kufuatilia manowari za adui na kutahadharisha jeshi la wanamaji.
Chombo hicho kina uzito wa tani 5,000 na kina mfumo maalum wa ufuatiliaji unaojumuisha antena tatu zenye umbo la duara zilizojaa vifaa vya utambuzi. Kwa mara ya kwanza uwezo wa meli hiyo ulijaribiwa mnamo 2018.
14 MW za umeme zinaweza kuzalishwa katika meli hii. Husaidia katika kufuatilia makombora ya adui na hutoa data sahihi kutoka kwa majaribio ya kawaida ya makombora yaliyofanywa.
Jeshi la Wanamaji la India linasema kuwa meli hiyo imejengwa chini ya mpango wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi's Make in India. Ingawa inasemekana kuwa kiasi cha hadi milioni 725 zimetumika katika mradi huu, serikali ya India bado haijatoa taarifa rasmi kuuhusu.
Meli zilizo na vifaa kama hivyo zinapatikana tu USA, Ufaransa, China na Urusi.
Ingawa hailinganishwi na meli za Yuanwang za China, Dhruv ina vifaa vya kisasa vya kufuatilia setilaiti na makombora kama meli za Yuanwang 5 ambazo zimewasili Sri Lanka. Dhruv sio meli ya kivita. Inatoa msaada wa kiufundi kwa meli za kivita na Vikosi vya Ulinzi vya India pekee.