Jinsi kucha inavyoelezea hali ya afya yako

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutunza kucha zako ni zaidi ya kwenda kwenye saluni za urembo wa kucha. Sehemu hii ya mwili, inaweza kuonyesha matatizo mbalimbali ya afya.
Ni muhimu kuzingatia mabadiliko ya rangi, kwenye kucha zako na vipengele vingine vinavyotumika kama tahadhari kwa magonjwa mengi. Hii inapotokea, inashauriwa kutafuta daktari wa ngozi ili kutathmini kwa kina na kufanya vipimo kama vile vya damu na zinginezo ambazo daktari anaweza kuamua.
Wakati kitu kikubwa kikishukiwa, mtaalamu anaweza kuagiza seli au tishu kuondolewa kwa uchunguzi.
Kuna magonjwa ambayo ni yanachukua muda kujulikana, yanayoathiri sehemu moja au zaidi za mwili, ambayo hutokea kwa miguu na kwa mikono.
Matatizo ya kawaida husababishwa na figo, ngozi, ini, lishe, na hali ambayo mfumo wa kinga ya mwili hushambulia seli zenye afya.
Habari njema ni kwamba tofauti fulani za kucha hazimaanishi shida kubwa kila wakati, mara nyingi husababishwa na utaratibu wa urembo.
"Kucha za miguuni wakati mwingine zinakabiliwa na matatizo zaidi. Ukucha, kwa mfano, unaweza kuwa njano na mzito," anasema Valéria Zanela Franzon, daktari wa ngozi na profesa wa Tiba katika Chuo Kikuu cha Katoliki huko Paraná (Pur).
Zifuatazo ni ishara kadhaa ambazo zinaweza kuonyesha matatizo ya kiafya na zinastahili kuzingatiwa:
Kucha nyeupe
Rangi ya kucha lazima izingatiwe wakati mtu anapoona mabadiliko yasiyo ya kawaida.
Kwa mfano rangi nyeupe, kivuli nyepesi kinaweza kuashiria mtu ana ugonjwa wa mycosis unaosababishwa na kuambukizwa na vimelea, kama vile upele. Psoriasis, ugonjwa wa ngozi unaosababisha vipele kwa kuwashwa, mabaka magamba, mara nyingi kwenye magoti, viwiko, shina na ngozi ya kichwa, na pneumonia au homa ya mapafu na hata moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Ukosefu wa baadhi ya virutubisho, utapiamlo na chakula cha chini katika vyakula vya protini pia husababisha picha.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kuwa na kucha nyeupe kunaweza pia kuonyesha upungufu wa damu. Husababishwa na ukosefu wa madini ya chuma na kunaweza kufanya ukucha uwe na umbo la kijiko na kukunjamana," asema Juliana Piquet, daktari wa ngozi na mshiriki wa Jumuiya ya Madaktari ya Ngozi ya Brazil na Jumuiya ya Amerika kwa Tiba ya Laser na Upasuaji.
Pia kuna kinachojulikana leukonychia, ni madoa meupe kwenye kucha kwa kawaida si ishara ya kutisha, lakini wakati mwingine inaweza kufichua matatizo makubwa ya utaratibu au hali ya kuzaliwa.
Ili kutibu hali hizi, madaktari huwaomba mgonjwa kuchunguza sababu ya tatizo. Kwa hiyo, unashauriwa kufanya vipimo mbalimbali na ufuatiliaji na mataalamu wa ngozi na wataalamu wengine wa masuala ya moyo na lishe.
Kucha ya njano
Rangi inaweza kuwa na sifa ya urithi wa maumbile au kwa kuzeeka kwa msumari, na kuacha kuwa mzito na kwa sauti ya njano.
Inaweza pia kutokana na rangi inayosababishwa na mycoses maalum na fungasi.
Katika hali mbaya zaidi, pia inaonyesha hali kama vile psoriasis, Virusi Vya Ukimwa, na ugonjwa wa figo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wavutaji sigara wanaweza pia kubadilisha rangi ya kucha zao, kutokana na kushika sigara moja kwa moja. Rangii hii kawaida huonekana kwenye kucha ya kidole.
Kucha zenye mabaka meupe
Mabaka haya yanajulikana kama "pitting" dots na zinaweza kuonekana kwenye kucha.
Yanahusishwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama atopic dermatitis -hali ambayo husababisha ngozi kuwa kavu, kuwasha na kuvimba na hali nyingine za ngozi na nywele.
Ni kawaida kwa watoto wadogo, lakini inaweza kutokea katika umri wowote.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kucha ya bluu
Ingawa ni nadra, rangi hii inaweza kutokana na matumizi ya dawa maalum. Mojawapo ya kawaida ni zile zinazotibu chunusi na dawa za malaria ambazo hutumiwa kutibu malaria.
Wakati hali hii inapojitokeza, daktari lazima atathmini ikiwa kuna haja ya kusimamisha dawa fulani na kuendelea na aina mpya ya matibabu.
"Inazingatiwa ikiwa kucha ndio udhihirisho pekee na athari ya pili inayokubalika", anaongeza Valéria Zanela Franzon, kutoka P ur.
Kucha yenye maambukizi ya mara kwa mara ya vimelea
Ugonjwa wa mycosis unasababishwa na maambukizi ya vimelea na unaweza kutokea tena wakati matibabu yanapositishwa.
Wakati ufuatiliaji haufanyiki vizuri, vimelea vinaweza kutokea na kushambulia kucha mara kwa mara.
Tatizo linaathiri zaidi kucha miguuni na linapaswa kutibiwa hadi miezi sita.
Katika mikono inashauriwa kutibu kwa muda wa miezi mitatu hadi minne.
Muathiriwa anapaswa kuzingatia wakati unaofaa wa kila dawa na kufuata kwa makini ushauri wa daktari hadi matibabu yatakapokamiliaka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kucha yenye mistari
Mistari hii inajulikana kama mistari ya Beau, inafanana na mistari ya horizotal na inaweza kuonekana baada ya homa kali au matibabu maalum.
Wakati kiwewe kinatokea katika eneo hilo, ni kawaida kwa mistari kuunda mahali hapo, na kuacha ukucha ukiwa na makunyanzi zaidi.
Wakati mistari unapokuwa giza na kuonekana kwenye kidole kimoja tu, inaashiria hali inayofahamika kama melanoma, ambayo ni saratani ya ngozi.
Maudhui yote ya afya kwenye BBC yametolewa kwa maelezo ya jumla pekee, na hayapaswi kuchukuliwa kama mbadala wa ushauri wa matibabu wa daktari wako au mtaalamu mwingine yeyote wa afya. Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu afya yako kwa ujumla, unapaswa kuwasiliana na mtoa huduma wa afya wa eneo lako.