Lishe: Hizi ndizo faida za kiafya za kula mayai    

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtaalamu wa lishe Jo Lewin  anaelezea faida za mayai.

Mayai hayauzwi tu kwa bei nafuu , bali pia yana kiwango kikubwa cha protini. 

Je yai ni nini hasa?

Kadri watu wengi wanavyofuga kuku nyumbani, ndivyo idadi kubwa ya mayai inavyoliwa.

  Sehemu nyeupe yay ai pamoja na kiini cha rangi ya manjano vimejaa virutubisho. Vina protini, vitamini na madini. Kiini cha manjano kina aina za vitamini zenye uwezo wa kuyeyuka   (kama vile vitamini D na E) na asidi muhimu za mafuta. Sehemu nyeupe yai ina kiwangi kikubwa cha protini.  

 Mayai ni chakula cha afya. Unaweza kutengeneza aina nyingi za mapishi ya mayai.  Mayai yanayofahamika zaidi ni ya kuku.  Lakini pia kuna mayai ya bata, bata bukini na  mayai ya kware.   

G
Maelezo ya picha, Sehemu nyeupe na ya manjano ya yai zimesheheni virutubisho

Faida za lishe za mayai 

Yai moja la kuku lina:

Kalori 84 kcal / 351 KJ

Gramu 8.3 za protini

Gramu 5.7 za mafuta

Gramu 1.6 za mafuta   

Miligramu 18 za follicic acid

Miligramu 1.89 za vitamini D

G
Maelezo ya picha,  Mayai yana aina zote za madini ya  amino acids yanayohitajikwa kwa afya

Faida za mayai

1. Umuhimu wa ulaji wa kirutubisho cha mayai

Mayai yamejaa virutubisho. Huwa na takriban karibu virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili. Huwa na virutubisho vya nadra kama vile   vitamini  D, B12 na madini ya  iodine.

 Zina chanzo muhimu cha protini kwasababu yana amino acids  muhimu kwa chakula bora.

 Mayai yana kiwango cha juu cha mafuta ya  omega-3 fatty pamoja na vitamini A na E.

2. Huboresha afya ya mishipa ya moyo

Mayai yana kiwango kikubwa cha  betaine na  choline, virutubisho vya moyo vinavyozuia magonjwa ya moyo. Utafiti uliofanywa na Uchina na kuwashirikisha karibu watu nusu milioni, unapendekeza kuwa watu wanapaswa kula yai moja kwa siku. 

Hii inaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Wataalamu wamesisitiza kwamba ulaji wa kiwango cha juu cha mayai kunafaa kuendana na mtindo wa maisha wa afya.   

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni chanzo cha  Cholini

Mayai ni mojawapo ya vyanzo bora vya lishe ya  cholini

Choline ni kirutubisho muhimu ambacho  kwa kawaida hupatikana katika kundi la Vitamini B. 

Kirutubisho hiki ni muhimu katika uundwaji wa utando wa seli na kwa utendaji wa ubongo, ikiwemo kumbukumbu. 

Mayai ni bora kwa afya ya macho 

Kadri tunavyozeeka, ni jambo la kawaida kupungua kwa uwezo wetu wa kuona.  Kwa bahati mbaya, kuna virutubisho vinavyopatikana katika lishe bora ambayo inaweza kusaidia kuboresha afya  nzuri ya macho.

 Watu wanashauriwa kula mayai kwa ajili ya afya ya macho. Kiini cha yao kina kiwango kikubwa cha  carotenes, hususan lutein na zeaxanthin, ambazo ni bora zaidi katika kuzuia magonjwa mbali mbali  ya macho. 

 Mayai pia ni chanzo cha Vitamini A, ambayo ni muhimu kwa uwezo mzuri wa kuona.   

5. Mayai husaidia kudhibiti uzito wako wa mwili 

Mayai yana kiwango cha juu cha protini. Protini ya mayai hushibisha haraka kuliko mafuta na wanga.

Tafiti zimeonyesha kuwa kifungua kinywa cha mayai humfanya mtu ahisi shibe zaidi  na huwa na kiwango kikubwa cha wanga.

Mayai yanaweza kukusaidia kupunguza kiwango cha karoli unachokula kwa siku.   

G
Maelezo ya picha, Mayai yana kiwango kikubwa cha protini

Je mayai ni salama kwa kila mtu?

Sumu ya chakula ya  Salmonella  inaweza kusababishwa na ulaji wa mayai mabichi au ambayo hayakupikwa  kwa kiwango kinachohitajika. Hatahivyo, kutokana mabadiliko ya uzalishaji wa mayai, Shirika la viwango vya vyakula nchini uingereza  (FSA) limetoa mapendekezo mapya. 

Ushauri wa hivi sasa unathibitisha kuwa watoto wachanga, watoto, wanawake wajawazito na wazee wanaweza kula mayai mabichi au yaliyopikwa kiasi ili mradi mayai hayo yawe yametengenezwa kwa viwango bora. 

Mayai pia yapo katika aina za vyakula vinavyoweza kusababisha mzio. Watoto wanaweza kuwa miongoni mwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata mzio kutokana na mayai.

Ingawa watoto wengi wanaweza kuuepuka mzio way ai wakati wanapoanza shule, baadhi yao huendelea kuathirika nao mpaka baadaye utotoni mwao na wakati mwingine hadi wanapokuwa watu wazima.