Maharashtra: Kwa nini familia za jamii hii ya Kihindi zinaishi kwenye barabara kuu na wanyama

ggg
Maelezo ya picha, Mwezi mmoja baada ya mafuriko makubwa kukumba wilaya ya Gadchiroli, wakaazi wake bado hawajarejea makwao

"Imekuwa zaidi ya mwezi mmoja wa kuishi bila chochote," Neelakka Modem, mwanamke wa kabila kutoka jimbo la magharibi mwa India la Maharashtra, anasema kwa huzuni huku mvua ikinyesha kwenye hema lake la plastiki lililochakaa.

Yeye na familia yake, pamoja na wengine 700, walilazimika kuacha nyumba zao katika kijiji cha Somanpalli wilayani Gadchiroli baada ya mvua kubwa kunyesha Julai kusababisha mafuriko makubwa. Wamekuwa wakipiga kambi kando ya barabara kuu tangu wakati huo.

"Mamlaka walikuja katikati ya usiku na kututaka tuhamie mahali salama. Hatukuondoka na chochote zaidi ya nguo tuliyokuwa tumevaa," Bi Modem, 70, alikumbuka.

Serikali ya jimbo imetoa chakula na maji, lakini kuishi kando ya barabara kuu kuna hatari - magari yaendayo kasi, wanyama pori, wakiwemo nyoka wauaji, ni kawaida katika eneo hili ambalo ni makazi ya misitu minene ya kitropiki.

Huko kijijini, mtoto wa Bi Modem Madhukar, mfanyakazi wa shambani, anajaribu kuokoa chochote awezacho kutoka kwa nyumba yao iliyoharibiwa. Lakini Bi Modem anajiuliza kama watawweza kurudi.

"Hatuwezi kuishi huko tena - mahali hapo hapakaliki tena. Serikali inapaswa kuturekebisha mahali pengine," alisema.

ggg
Maelezo ya picha, Wakaazi wa kijiji cha Somanpalli huko Gadchiroli wamekuwa wakiishi katika kambi kando ya barabara kuu

Mvua kubwa ni kawaida wakati wa masika katika wilaya ya Gadchiroli, ambayo imezungukwa na misitu.

Mto wa Godavari, wa pili kwa urefu zaidi nchini India, pamoja na vijito vyake, hutengeneza eneo linalokabiliwa na mafuriko kati ya Juni na Septemba. Wakati wa miezi hiyo, mara nyingi hufurika na maji kuingia katika vijiji.

Lakini wakaazi wanasema mafuriko yamekuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Mvua kubwa mwaka huu kati ya Julai 11 na 19 iliacha uharibifu, angalau miji na vijiji 34 kati ya 52 kando ya mto wa Gadchiroli vilizama kwa siku, wakati vitatu kati yao, ikiwa ni pamoja na Somanpalli, vilikaribia kusombwa wakati kina cha maji kilipopanda hadi kiwango chao cha juu zaidi katika kipidni cha miaka 35.

Mvua zimekoma sasa, lakini watu bado hawajarejea majumbani au kuanza kujenga upya maisha yao.

"Sijawahi kuona mafuriko kama haya. Safari hii, imechukua kila kitu," Bi Modem alisema.

ggg

Chanzo cha picha, ANI

Maelezo ya picha, Mkoa wa Gadchiroli hupata mvua kubwa kila mwaka

Wanakijiji na wataalam wa mazingira wanasema mafuriko makubwa yanasababishwa na kumwagika kwa maji kutoka kwa bwawa la karibu huko Medigadda - kijiji katika jimbo jirani la Telangana. Lakini mamlaka imekanusha madai hayo.

"Bwawa halina athari kwa hali ya mafuriko huko Gadchiroli na maeneo ya jirani. Kwa kweli, kwa sababu ya ujenzi wa kingo za mito unaweza kuzuia uharibifu mkubwa wa mafuriko ya hivi karibuni," alisema Dk Rajat Kumar, afisa mkuu wa idara ya umwagiliaji wa Telangana.

Bwana Kumar aliongeza kuwa maafisa wa umwagiliaji katika jimbo lake walikuwa "wakiendelea kuratibu" na wenzao huko Maharashtra juu ya hali hiyo.

Bwawa hilo, linalojulikana kama Lakshmi Barrage, liko kwenye mpaka kati ya Maharashtra na Telangana. Iilijengwa 2016 baada ya majimbo hayo mawili kutia saini makubaliano ya kugawana maji.

Tangu kuanzishwa kwake, mradi huo umekumbwa na utata kuhusu madai ya ukiukaji wa sheria za mazingira madai ambayo yamekanushwa na serikali zote mbili za majimbo.

"Watu walipinga ujenzi wa bwawa hili na kulikuwa na maandamano, lakini serikali ya Maharashtra na Telangana haikujali, sasa, tunateseka kwa sababu hiyo," Ranjit Gagapurwar, mwanaharakati wa kijamii wa eneo hilo.

Aliongeza kuwa wanakijiji wanaoishi kwenye kingo za mto Godavari wanahitajika kuhamishwa kabisa kwa sababu "itafurika kila msimu wa mvua".

Jitendra Shiktode, afisa wa serikali huko Maharashtra ambaye anasimamia Gadchiroli, alisema: "Tunajaribu sana kuwasaidia wanakijiji. Lakini haiwezekani kuwahamisha haraka hivyo."

ggg
Maelezo ya picha, Wataalamu wa mazingira wanasema kwamba kiwango cha mafuriko katika eneo hilo kinaongezeka kwa miaka sasa

Wataalamu, hata hivyo, wanasema kuwa suala si tu kuhusu ukarabati, lakini kuhusu usimamizi wa miradi ya maji.

"Kila bwawa ni chanzo kinachowezekana cha maafa. Huo ndio ukweli na mtu anatakiwa kuufahamu," anasema Himanshu Thakkar, mwanaharakati na mratibu wa Mtandao wa Mabwawa wa Asia Kusini kuhusu Mabwawa, Mito na Watu. SANDRP),

"Sio tu bwawa linaweza kupasuka lakini pia kama halitaendeshwa ipasavyo, linaweza kusababisha mafuriko."

Tarehe 8 Agosti, wizara ya rasilimali za maji ya India ilikubali kwamba "operesheni mbovu za hifadhi wakati mwingine zinaweza kusababisha mafuriko katika maeneo ya chini ya mto."

Bw Thakkar alielezea jinsi hii inaweza kutokea: "India imeongeza mvua katika miezi mitatu hadi minne ya masika. Kwa hivyo ikiwa bwawa litajazwa mwanzoni mwa msimu na mvua ikanyesha zaidi, mamlaka huishia kutoa maji kutoka kwenye bwawa na eneo hilo. Mto wa chini tayari umejaa mafuriko, hali inazidi kuwa mbaya."

Mojawapo ya mambo ya kuhakikisha uendeshaji mzuri wa mabwawa ni "kanuni ya mzunguko" au mchoro wa grafu inayoonyesha wakati na jinsi bwawa linapaswa kujazwa hatua kwa hatua msimu wote.

Grafu hii, Bw Thakkar alieleza, lazima iundwe kwa kuzingatia kujaa kwa udongo na uwezo wa kubeba mto wa chini au muda wa mawimbi, ikiwa bwawa liko karibu na pwani.

ggg
Maelezo ya picha, Wakazi wanasema kuwa bwawa lililoko katika jimbo jirani la Telangana ndilo lililosababisha mafuriko hayo

Kando na hilo, mamlaka pia zinahitaji kuboresha mkondo mara kwa mara ili kushughulikia mabadiliko ya mifumo ya mvua. "Tunazidi kushuhudia mvua za masika zinazochelewa. Hivyo tunatakiwa kubadili kanuni ipasavyo," alisema.

Hili ni muhimu sana kwa maeneo kama vile Asia Kusini, ambapo hali mbaya ya hewa kama vile mafuriko yanatarajiwa kuwa ya mara kwa mara huku kukiwa na ongezeko la joto, kulingana na ripoti ya 2022 ya Mabadiliko ya Tabianchi the Intergovernmental on Climate Change (IPCC).

Huko Somanpalli, viwango vya maji vimepungua. Lakini wanakijiji bado wanaishi kando ya barabara kuu.

Wanaogopa mafuriko mengine kwa kuwa msimu wa masika bado haujaisha.

"Kuna faida gani kurudi? Tumepoteza kila kitu," Bi Modem alisema.