Mabadiliko ya tabia nchi: Kijiji cha India ambacho kipo hatarini kutoweka chini ya maji

Maelezo ya video, Mabadiliko ya tabia nchi: Kijiji cha India ambacho kipo hatarini kutoweka chini ya maji

Uppada, kijiji cha pwani katika jimbo la kusini mwa India la Andhra Pradesh, kinajulikana kwa utamaduni wake wa kipekee wa kusuka.

Lakini uwepo wake uko chini ya tishio kwa sababu ya kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari. Tayari watu wamelazimika kusogea ndani zaidi kwani mmomonyoko mkubwa wa pwani umeharibu nyumba zao.

Watafiti wa hali ya hewa wanasema mji jirani wa Kakinada unaweza kuwa unaofuata kuathiriwa.