Fahamu sababu zinazochangia baadhi ya watu kukosa furaha

Mujer pensativa

Chanzo cha picha, Getty Images

Sekta za kujitegemea zinazidi kushamiri. Imekuwa ikishika kasi kwa miaka mingi mingi kupitia saikolojia chanya, utafiti wa kisayansi wa kile kinachofanya watu kufanikiwa. Hata hivyo, viwango vya wasiwasi, huzuni na kujiumiza vinaongezeka duniani. Je, tunaweza kukosa furaha, licha ya hatua zilizopigwa kataikolojia?

Tunapozungumza kuhusu saikolojia chanya, tukumbuke makala yaliyochapishwa kwenye jarida la Saikolojia ya mwaka 2005, iliyobadilish mtazamo wetu kuhusu furaha.

Utafiti huo ulifichua kuwa asilliamia 50 ya furaha ya watu hutokana na jeni zao, asilimia 10 hutegemea hali zao na asilimia 40 hutegemea shughuli wanazofanya.

Kwa miongo kadhaa watafiti walifanya tafiti wakitumia pacha na kubaini jinsi jeni zinavyoashiria kutofautiana kwa furaha yao kwa asilimia 40 hadi 50.

Hii ndio sababu watu wawili waliolelewa katika mazingira sawa wanaweza kujibu tofauti kwa kichocheo kimoja. Hii inaondoa dhana ya kitabia inayochangiwa na mazingira ya usawa na kusababisha majibu sawa.

Kutokana na mbinu hii ya kimaumbile na mazingira ya watu katika misingi ya mahusiano ya kifamilia ndio sababu pacha wanatumiwa hapa.

Ili kujibu ukosoaji wa makala hiyo ya mwaka 2005, waandishi wale wale waliandika makala nyingine mwaka 2019 iliyoeleza kwa njia tofauti athari za kimaumbile kwa furaha, ikitambua mwingiliano kati ya jeni zetu na mazingira tuliyo ndani.

Asili na elimu

Asili na malezi hazilingani.

Jeni hushawishi tabia inayosaidia watu kuchagua mazingira yao. Kwa mfano jeni zilizorithiwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto husaidia watoto kujenga vikundi vya marafiki.

Mujeres leyendo

Chanzo cha picha, Getty Images

Vile vile mazingira hubadilisha tabia za jeni.

Kwa mfano, akina mama wanaokuwa hasira wakati wakiwa wajawazito, jeni za watoto wao hubadilishwa na kutokana na mabadiliko ya kemikali inayoathiri ukuaji wa mtoto. Kutokana na hilo watoto huzaliwa wakiwa wadogo wakikiwa na matatizo kama vile ugonjwa wa moyo.

Hii ndio sababu ya watu wawili wanaolelewa mazingira sawa wanaweza kujibu kichocheo sawa kwa njia tofauti.

Wengine huchangia mazingira yao kwa hivyo wanaweza kubadilisha sana mawazo yao, hisia na tabia kuambatana na hali mbaya au nzuri.

Kwa hivyo wakati wanahudhuria semina za ustawi au wanaposoma kitabu kinachohusu saikolojia nzuri, wanaweza kuchochewa na kubadilika wakilinganishwa na wengine. Pia mabadiliko hayo yanaweza kudumu kwa muda mrefu.

Lakini hakuna saikolojia nzuri inayofanya kazi kwa kila mtu kwa sababu ya tofauti ya chembe chembe ya vinasaba (DNA). Hii inaashiria kuwa tuna viwango tofauti vya ustawi na mabadiliko yake katika maisha.

Mujer triste.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tunaelekea mkondo wa kukosa furaha

Baadhi ya watu lazima wapambane zaidi kuboresha ustawi wao kuliko wengine, hali ambayo inaweza kuwafanya wakakosa furaha kwa kipindi kirefu.

Tofauti ni kwamba wale walio na uwezo wa kubadilika kuambatana na mazingira yao wanaweza kuboresha ustawi wao na hata kupiga hatua zaidi ikiwa watachagua mtindo wa maisha wa kuzingatia afya bora na kuishi katika mazingira yanayochochea furaha.

Kilicho muhimu pia ni maamuzi tunayofanya kuhusu maeneo tunayoishi, wale tunaoishi nao na vile tunavyoamua kuishi maisha yetu katika hali ambayo huathiri furaha yetu na furaha ya vizazi vijavyo.

Makala ya BBC Mundo.