Unnao: Mwanamke wa India achomwa moto akielekea mahakamani kusikiliza kesi ya ubakaji

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamke wa miaka 23-anayedaiwa kuwa muathiriwa wa ubakaji anapigania maisha yake baada ya kuchomwa moto akiwa njiani kuelekea mahakamani kaskazini mwa India.
Mwanamke huyo alikua akienda kusikiliza kesi aliyowasilisha mahakamani dhidi ya wanaume wawili mwezi Machi, katika eneo la Uttar Pradesh.
Anasemekana kuwa katika hali mahututi na anapokea matibabu baada ya kupata majeraha mabaya ya moto.
Wanaume watano wakiwemo wawili wanaotuhumiwa kumbaka wamekamatwa kwa kushukiwa kumchoma moto, polisi inasema.
Mwanamke huyo alikuwa akielekea katika kituo cha treni, aliposhambuliwa na kundi la wanaume ambao walimburuza katika uwanja uliokuwa karibu na kumchoma moto, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini India.
Madktari wanaomtibu katika hospitali ya mji wa Lucknow, wanasema alipata majeraha ya moto kwa 90% na kwamba atalazimika kusafirishwa kwa ndege haraka iwezekanavyo hadi hospitali ya mji mkuu wa Delhi, kwa matibabu zaidi.
Kisa hicho kilitokea katika Wilaya ya Unnao, ambao hivi karibuni uliangaziwa katika vyombo vya habari kuhusiana na kisa kingine cha ubakaji.
Polisi walianzisha uchunguzi dhidi ya mbunge wa chama tawala mwezi Julai baada ya mwanamke aliyemtuhumu kwa ubakaji kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari.
Wawili kati ya mashangazi zake waliuawa na wakili wake kujeruhiwa.
Tukio hili la hivi punde limezua ghadhabu katika miji tofauti nchini India, ambako kesi ya kushangaza ya mauaji na ubakaji iliangaziwa pakubwa na vyombo vya habari dunia chini ya wiki moja iliyopita.

Unyanyapaa mkubwa
Mamia ya ya visa vya ubakaji huripotiwa nchini India kila siku kwa mujibu wa takwimu za uhalifu. Katika maeneo ya mijini na vijijini, watoto na hata wanaume wanashambuliwa. Visa vingi haviripotiwa wala kuangaziwa katika vyombo vya habari.
Katika siku za hivi karibunika kumeshuhudiwa ongezeko la ghasia hasa baada ya kisa cha kubakwa na kuuawa kwa daktari wa mifugo mjini Hyderabad. Kisa cha hivi punde katika wilaya ya Unnao imezidisha hasira miongoni mwa watu.
Katika nchi ambayo kuripoti visa vya ubakaji hukabiliwa na unyanyapaa, je wale wanaoripoti visa hivyo wanapewa usalama? Je mamlaka inafanya lipi kuhakikisha wanaofanya uhalifu huo wanadhibiwa?
Mwezi Decemba mwaka 2012 niliangazia genge la wabakaji mjini Delhi ambalo liliamua kuanzisha gumzo kuhusu unyanyasaji wa kingono nchini India. Lakini ni mambo machache yaliobadilika.
Katika siku za hivi karibuni baadhi ya maafisa walitoa wito kwa wanawake kuenda nyumbani mapema au kutotumia usafiri wa umma nyakati fulani za usiku.
Lakini wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanashinikiza umuhimu wa kubadili mtazamo wa jamii dhidi ya wanawake badala yakuwashauri jinsi ya kujikinga na wabakaji.

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwisho wa X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ubakaji dhidi ya wanawake umekuwa ukiangaziwa India tangu mwaka 2012 baada ya genge la wanaume kumbaka na kumuua mwanamke ndani ya basi katika mji mkuu wa Delhi.
Kwa mujibu wa takwimu za serikali kuhusu uhalifu, polisi wali visa 33,658 vya ubakaji viliripotiwa nchini India mwaka 2017 - kuashiria kuwa karibu watu 92 hubakwa kila siku.