Dawa ya sumu za kikohozi ilitumwa vipi nchini Gambia?

Chanzo cha picha, WHO
Vifo vya karibu watoto 70 nchini gambia, vilivyohusishwa na dawa za vikohozi nchini India, vinachunguzwa huku kukiwa na hofu kuhusu ufanisi wa wadhibiti wa viwango wa watengenezaji na katika biashara za madawa.
Ni kosa gani lililofanyika nchini Gambia?
Wiki iliyopita, Shirika la afya duniani (WHO) lilitoa tahadhari kwa dunia kuhusu nembo nne za dawa nne za kikohozi za maji maji, ikisema zinaweza kuhusishwa na uharibifu mbaya wa figo, kufuatia ripoti kutoka Gambia za watoto waliopatikana na matatizo makubwa ya figo.
Tathmini ya maabara kuhusu dawa za maabara ya dawa za maji maji "ilithibitisha kwamba zilikuwa na kiwango kisichokubalika cha diethylene glycol na ethylene glycol kama sumu", kulingana na WHO.
Maafisa wa India na watengenezaji wa dawa za kikohozi za maji maji, Maiden Pharmaceuticals, wanasema dawa hizoziliuzwa kwa Gambia pekee.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nini kinachofahamika kuhusu watengenezaji ? Maiden Pharmaceuticals inasema ilitimiza viwango vya udhibiti vya kimataifa. Lakini baadhi ya bidhaa zake zilishindwa kutimiza viwango vya taifa vya udhibiti wa viwango nchini India.
Rekodi rasmi nchini India zinaonyesha kuwa kampuni:
- Iliwekwa kwenye orodha ya makampuni ambayo hayatakikani katika jimbo la Bihar , katika mwaka 2011, kwa kuuza dawa za maji ambazo zilishindwa
- Ilipitia mchakato wa kisheria wa wadhibiti wa viwango vya dawa nchini India mwaka 2018, kwa kukiuka udhibiti wa ubora mwaka 2018
- Ilishindwa katika jaribio la udhibiti wa ubora katika majimbo ya Jammu na kashmir, katika mwaka 2020
- Ilishindwa kudhibiti ubora katika jimbo la Kerala mara nne katika mwaka 2022
- Iko miongoni mwa makampuni karibu 40 ya kutengeneza dawa yaliyoorodheshwa na Vietnam kwa kuuza bidhaa ambazo za chini ya viwango vinavyostahili.
Kampuni hiyo yenye makao yake katika jimbo la Haryana, imesema ime "shitushwa" na vifo katika gambia, na ''imekuwaikifuata kikamilifu itifaki za maafisa wa afya, ikiwa ni pamoja na mdhibiti mkuu [ wa India] na wadhibiti wa jimbo wa madawa, Haryana".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Haiwezi kutoa kauli zaidi wakati wadhibiti wa dawa wakiendelea bado kuzipima, iliongeza.
Waziri wa afya wa Haryana Anil Vij aliiambia BBC News kuwa sampuli zilitumwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kama kuna kitu ambacho hakiko sawa kitabainika, hatua itachukuliwa.
Je udhibiti wa ubora ni wa ufanisi wa kiasi gani?
India huzalisha theluthi ya madawa yanayotumiwa duniani, mengi yakiwa ni madawa ya muundo wa nakili (generic drugs).
Ni msambazaji mkuu wa dawa kwa nchi za Afrika, Amerika Kusini na sehemu nyingine za Asia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Viwanda vyake vya kutengeneza madawa vinawajibika kuheshimu na kuzingatia viwango vya udhibiti wa ubora na tendaji wa uzalishaji kwa ujumla.
Lakini makampuni ya india yamekabiliwa na ukosoaji na hata kupigwa marufuku na wadhibiti wa kigeni kama vile Taasisi ya Marekani ya utawala wa chakula na madawa (FDA) kwa matatizo ya udhibiti wa bora katika baadhi ya viwanda vyake.
Uchambuzi mmoja kuhusu sekta ya madawa nchini India ulielezea juu ya ukosefu wa fedha za kutosha za ufadhili wa taasisi na ukosefu wa ufafanuzi wa kutosha wa sheria kama tatizo kuu, pamoja na ukosefu wa haja ya kuhakikisha viwango vinafuatwa.
Mwanaharakati wa afya ya umma Dinesh Thakur pia alielezea kutolewa kwa adhabu rahisi nchini India kwa kuepuka viwango vya ubora - faini ya $242 (£220) na uwezekano wa hukumu ya kifungo cha gerezani cha hadi miaka miwili.
Na pia India haijajumuishwa viwango vya WHO kwa mashirika ya taifa ambayo yanadhibiti madawa, ingawa imejumuishwa kwa chanjo.
"Hii inaweza kusababissha kutokuwepo kwa udhibiti unaoendelea kuhusu shughuli za utengenezaji wa madawa ," Leena Menghaney, Mkuu wa mpango wa utoaji wa dawa Kusini mwa Asia katika Médecins Sans Frontières (MSF), anasema.
Je Gambia ingepaswa kupima dawa?
Wizara ya afya mjini Delhi imeanzisha uchunguzi lakini inasema "ni jambo la kawaida kwamba nchi inayoagiza inapima bidhaa hizi zilizoagizwa... na kujiridhisha yenyewe na ubora".
Lakini Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Gambia la udhibiti wa madawa Markieu Janneh Kaira anasema kipaumbele chake ni kuchunguza dawa za kutibu malaria, dawa za magonjwa ya maambukizi- antibiotics na dawa za kuzuia maumivu, kuliki dawa za kikohozi.
BBC News iliwasialiana na shirika kwa ajili ya kupata ufafanuzi lakini haikupata jibu.
Rais wa gambia , Adama Barrow, amesema "atafuatilia kwa kina " sababu ya mkasa na kutangaza kuundwa upya kwa "maabara ya taifa ya udhibiti wa ubora kwa ajili ya usalama wa dawa na chakula".
Gambia "itaanzisha mpango wa kumaliza uagizaji wa dawa zilizo chini ya viwango", aliongeza.
MSF inataka nchi yenye ufanisi wa kupima kuzisaidia nchi zenye kipato cha chini kama vile Gambia.
"Hii sio kuhusu wajibu tu wa nchi zinazoagiza," Bi Menghaney anasema. nchini Nigeria, Shirika la taifa la Udhibiti wa viwango vya dawa na chakula kwa sasa linataka bidhaa zote zilizoagizwa kuidhinishwa na shirika hilo kabla ya kuondoka India.
