Kwanini mtoto huyu wa Gaza aliyefanyiwa upasuaji wa moyo anarejeshwa katika eneo la vita?

- Author, Adnan El-Bursh
- Nafasi, BBC News Arabic
- Akiripoti kutoka Doha
Katika hema ambayo ni makaazi ya muda ya watu katika kambi ya wakimbizi wa Al-Shati, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Enas Abu Daqqa,33, anaonekana akiwa amempakata mtoto wake mchanga. Kuna mtu anasikika akiimba mara kwa mara nyuma yake angalau kuto kiburudisho licha ya joto kali la asubuhi.
Enas anahofia afya ya Niveen huenda ikazorota wakati wowote. Ana umri wa miezi saba tu, na alizaliwa wakati wa vita aikiwa na tundu kwenye moyo wake.
Mtoti Niveen analiakwa maumivu mama yake anapoelezea hali ngumu anayopitia kujaribu kuokoa maisha yake baada ya miundo mbinu ya afya ya Gaza kusambaratika
"Vita imemuathiri san," Enas aliiambia BBC. "Uzani wake hauongezeki nahofia anaweza kuwa mgonjwa."
Niveen anaweza kupata nafuu akipokea huduma ya dharura ya afya nje ya Gaza. Mnamo mwezi Machi, Jordan ilifanikisha hilo.
Wakati mapigano yalipositishwa kati ya Hamas na Israel, watoto 29 wa Gaza, akiwemo Niveen, walipelekwa Jordan kupokea matibabu katika hospitali za nchi hiyo. Mama yake na dada zake walisafiri pamoja nao.
Walikuwa watoto wa kwanza kupelekwa Jordan baada ya Mfalme Abdullah kutangaza mpango wa kutoa huduma za matibabu kwa watoto 2000 wa Gaza wakati wa ziara yake nchini Marekani mwezi ullioyotangulia. Mpango huo uliratibiwa na mamlaka ya Israel ambao ilikagua wazazi wanaosafiri na watoto wao.
Madaktari wa Jordan walimfanyia Niveen upasuaji wa moyo, na alikuwa ameanza kupata nafuu.
Lakini takribani wiki mbili baada ya watoto hao kupokea matibabu Jordan, makubaliano ya kusitishaji mapigano huko Gaza yaliporomoka wakati Israel ilipoanza tena mashambulizi yake dhidi ya Hamas.
Kwa wiki kadhaa, Enas alifuatilia habari kutoka katika chumba cha hospitali cha bintiye huko Jordan, akiwa na wasiwasi juu ya usalama wa mume wake na watoto wengine ambao walisalia Gaza.
Akiwa bado anahofia usalama wa familia yake Gaza tarehe 12 Mei, mamlaka ya Jordan ilimwambia Enas ajiandaye kurejea nyumbani siku iliyofuata, kwani walisema Niveen alikuwa amemaliza matibabu yake.
Enas alishtuka.
"Tuliondoka huku wakati mapigano yalikuwa yamesitishwa. Wanawezaje kuturudisha baada ya vita kuanza upya");