'Mtu anapodhibiti pesa katika uhusiano, inamaanisha anauthibiti kwa kila njia'

Chanzo cha picha, TABITHA LASLEY
Na Norberto Paredes
BBC World News
Tabitha Lasley alitaka kujua jinsi tabia wanaume inavyokuwa wakati hakuna wanawake karibu nao, lakini licha ya kuwa na fursa na wakati mzuri, hakuwahi kufanikiwa kuwaelewa. "Mimi ni mwanamke," anacheka.
Jambo zuri ni kwamba aliweza kuja na wazo na la kuvutia sana.
Baada ya kugundua kuwa alihitaji kumuacha mpenzi wake aliyemnyanyasa na kwamba kazi yake kama mwandishi wa habari katika jarida la makazi la London haikumfurahisha, Tabitha aliamua kuachana na hayo yote.
Alipakia mifuko yake na kufuata msukumo wake na ndoto yake kubwa: kuandika kitabu kuhusu majukwaa ya mafuta ya Bahari ya Kaskazini na wafanyakazi wao, wengi wao walikuwa wanaume waliotoka ya viwandani kaskazini mwa Uingereza, ambapo yeye binafsi alikulia.
Aliwasili katika mji mkuu wa mafuta wa Ulaya, Aberdeen, Uskochi, ambapo alitumia sehemu kubwa ya akiba yake kwa kukodisha nyumba ndogo kwa miezi mitano, wakati ambako aliishi kwa kuzungukwa na wanaume ambao waligeuza maisha yake juu chini.
Mwishowe, alipata alichokuwa akikitarajia.
Kubwa zaidi ilikuwa uchapishaji wa kitabu chake Sea State, ambapo aliandika kuhusu kumbukumbu zake huko Aberdeen.
Katika mji huo alimpenda mfanyakazi wa kwanza ambaye alimhoji , akajitambua tena, alilia na, zaidi ya yote, alijaribu kukabiliana na chuki dhidi ya wanawake katika sekta ambayo inatawaliwa na wanaume.
Kazi waliyoifanya inashughulikia masuala ya kijamii na Tabitha alipata kuvutiwa nayo zaidi kuliko uchimbaji wa mafuta yenyewe, kama vile pesa na jinsi inavyounda matabaka ya kijamii, na maisha ya familia ya wanaume hawa ambao hutumia nusu ya muda wao mbali na familia zao.
BBC News Mundo, idhaa ya BBC ya Kihispania, ilizungumza naye wakati wa tamasha la Hay Festival Cartagena de Indias, ambalo lilifanyika kuanzia tarehe 25 hadi 28 Januari, huko Cartagena, Colombia.

Chanzo cha picha, Getty Images
BBC - Maisha ya familia yanaathiriwaje wakati mwanafamilia yuko mbali na kazi?
Tabitha Lasley - Wakati unapokwenda mbali na familia yako nusu ya muda wako wa siku , huwezi kujenga uhusiano wa karibu sawa wale wanaoishi pamoja nao kwa muda mrefu kama vile saa tisa kwa siku.
Mwanaume anayefika nyumbani , anakula na familia yake, na kuwaaga watoto wake watoto wake wanapoenda kitandani atakuwa na hisia thabiti zaidi za maono ya jinsi anavyotaka familia yake iwe.
Wafanyakazi karibu na meli ya usambazaji mizigo katika bandari ya mji wa Aberdeen, unaojulikana kama mji mkuu wa mafuta wa Ulaya.
BBC- Wafanyakazi katika sekta ya mafuta hupata pesa nyingi, lakini mazingira ya kazi ni duni na hawaoni familia zao mara nyingi. Je, fedha wanazopata zinatokana na haya yote?
Lasley - Kwa kweli, moja ya mada kuu ya kitabu ni pesa.
Wakati mtu anadhibiti pesa zote katika uhusiano, pia hudhibiti uhusiano, na kwa kiasi kikubwa sana.
96% ya wahusika wa unyanyasaji ni wana uhusiano na unyanyasaji wa kifedha pamoja na aina nyingine za unyanyasaji.
Ni wazi si watu wote ambao hutengeneza pesa nyingi zaidi kuliko wengine katika uhusiano ni matusi kufafanua hili.
Lakini zaidi ya yote, karibu kila mnyanyasaji ni mnyanyasaji wa kifedha kwa sababu ukiwa na pesa ni njia bora sana ya kupata udhibiti.
Unapodhibiti pesa, kwa ujumla unadhibiti kila kitu kingine chochote kile.
Kwa bahati mbaya, ni kawaida kwa mtu ambaye anapata zaidi kuliko mwenzi wake kumchukulia mwenzi wake kwa usawa.
BBC – Katika kitabu chako pia ulizungumzia kuhusu pesa, ni nani anazo n ani nani hana. Unaweza kusema ni nini tofauti kubwa kati ya makundi haya mawili?
Lasley – Hapana. Kwa sababu kwa kweli hawapati pesa nyingi kama walivyozoea. Katika miaka ya 70 na 80 walipata pesa nyingi, lakini tangu wakati huo mishahara imeshuka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nilipowahoji wafanyakazi, nilikutana na wanandoa ambao waliniambia walikuwa na furaha. Lakini hii inaweza kuwa kutokana na tabia: kuna watu ambao wana furaha katika karibu hali zote.
Wengi wa wafanyakazi walikuwa na huzuni na daima katika hali mbaya.
Ni sekta ambayo idadi kubwa ya wafanyakazi huwa wanaume, na ulianza kuandika kitabu ukitaka kujua wanaume ni nini wakati hakuna wanawake wanaowazunguka. Wanafanyaje na wanafanya nini? Wanazungumzia nini?
Lasley – Kamwe sikujua wanaume wanakuwaje wakati hakuna wanawake karibu nao, kwa sababu mimi ni mwanamke.
Hii iliathiri mawasiliano kati yao na hii ndio sababu sehemu ya msingi wa malengo ya kitabu changu haikufanikiwa
Lakini ingawaje sikuwahi kugundua kwanza ukweli kuhusu mienedo na tabia zao, niliweza kupata wazo.
Mazingira ya kazi ya kiume yana athari mbaya sana kwa wanaume.
Wengu huwa na chuki dhidi ya wanawake, kwa sababu wengi wa wanaume ambao wanafanya kazi huko wametalikiana na wanawake mara moja au mbili na kubeba aina ya chuki kwa wanawake ambayo huwa wanairithidha kwa vijana.
Tabia hiyo hiyo mbaya inaendelezwa katika maeneo mengine ambapo kuna umati mkubwa wa watu, kama vile mashabiki wa mpira wa miguu au magereza. Wanawake wana athari za kistaarabu kwa wanaume.
Je, unadhani athari hii ya kistaarabu inatokana na tabaka la kijamii na kwamba kuna usawa zaidi kati ya wanawake na wanaume wakati wana kipato sawa?
Lasley - Kwa ujumla nadhani kwamba, angalau leo nchini Uingereza, miongoni mwa watu wenye pato la kati ni muhimu chini haijalishi ni nani mwenye kipato cha chini au cha juu. Jinsia zote mbili zina mapato zaidi au ya chini.
Katika mji wa London, kwa mfano, mpenzi wangu wa zamani alikuwa na udhibiti sana kwangu , lakini hakuwa na shida na kwangu mimi kuwa na marafiki wa kiume.
Ilikuwa tofauti sana huko Aberdeen, ambapo wafanyakazi w aliniambia kuwa hawawezi kuwa na marafiki wa kiume. Walidhani ilikuwa ajabu kuwa na marafiki wa kiume
Na hii hutokea kwa sababu majukumu ya kijinsia yanafafanuliwa zaidi. Wanawake nyumbani na wanaume ni kutafuta fedha zaidi.
BBC - Mmoja wa wafanyakazi hawa alikuita kahaba na kusema ulionekana rahisi. Mtu alikuambia umpuuze kwa sababu hivyo ndivyo jinsi watu husungumza huko. Umejifunza kupuuza aina hii ya chuki dhidi ya wanawake?
Lasley - Yeye hakuwa mtu pekee aliyeniita kahaba.
Sikuwahi kujifunza kupuuza aina hii ya tabia, lakini nilikua na nguvu zaidi hadi mwisho wa wakati wangu huko.
Nakumbuka machozi yakijaza macho yangu mara ya kwanza mtu aliniita kahaba. Nilihisi kama nilikuwa naenda kulia, lakini nikajiambia, "Usilie."
Sikuwa nasikia matusi kama hayo.
BBC - Ulimpenda mtu wa kwanza uliyemhoji kwa ajili ya kitabu hicho. Unakumbuka nini kuhusu hadithi hii ya mapenzi? Je, unajua kwamba hii itaishia kuwa janga?
Lasley – Ndio ni haibu ! Nadhani kila mtu karibu nami alijua hadithi hiyo itaisha vibaya, isipokuwa mimi.
Tulikuwa pamoja kwa miezi mitano, lakini kila kitu kilikuwa cha kushangaza sana.
Nakumbuka nikifikiria, "Wow, maisha yangu yanahisi kama tamthiria."
Kila siku kulikuwa na mkwaruzano. Kila siku kitu kilikuwa kinatokea. Mtu huyo alikuwa janga, aligeuza maisha yangu juu chini kama kimbunga.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi