Lulu Hunt Peters, mtaalam wa lishe bora aliyevumbua kuhesabu kalori zaidi ya karne moja iliyopita

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Laura Plitt
- Nafasi, BBC World
Idadi ya kalori huonekana kwenye lebo nyingi za vyakula na vinywaji vilivyopakuliwa, na hata kwenye menyu za baadhi ya mikahawa na baa:taarifa za kalori zipo kila mahali.
Unaweza kujua ni hatua ngapi unatembea na kuchoma kalori kila siku kwa kutazama kipimo kilichoko kwenye simu yako, na kama unakwenda ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo, utaona idadi ya kalori zikionekana kwenye kielezo cha baiskeli au kinu cha kuendesha kwa miguu (treill) za mazoezi.
Lakini hata bila msaada huu, pengine unajua kwamba saladi ya lettuce na nyanya ina kalori kuliko mkate wa nyama na kwamba kukimbia kutachoma kalori zaidi kuliko kutembea.
Hata hivyo, kuhesabu kalori ilikuwa ni jambo geni katika karne moja iliyopita.
Kalori kama kipimo cha lishe kilianza kutumika mwishoni mwa karne ya 19.
Lakini ni mwishoni mwa miaka ya 1920 ndipo ilipovuka kutoka uwanja wa sayansi hadi kwenye jamii kwa msaada wa Lulu Hunt Peters, daktari kutoka Marekani ambaye alihitimu kutoka chuo kikuu cha California wakati wanawake walikuwa chini ya asilimia 5 ya wanafunzi wa udaktari nchini Marekani.
Makala yake yaliyochapishwa kwenye vyombo vikubwa vya habari nchini Marekani,b ambayo ilielezea uzoefu wake wa kupunguza uzito, zilisomwa na maelfu ya wasomaji na kitabu chake cha "Diet and Health:With the key to Calories"(1918) kilikuwa kitabu cha kwanza cha lishe kilichouzwa kwa wingi katika historia.
Na ingawa sasa tunajua kuwa kuhesabu kalori sio mkakati bora wa kudumisha lishe bora au kupunguza uzito, tafiti zinaonyesha kwamba karibu asilimia 80 ya watu wanaopunguza uzito mkubwa kwa kupunguza ulaji wa kalori wanarudi tena kwenye uzito wao wa awali.
Kabla ya kueleza kwa undani ni kwa nini mfano wa Peters ulivuma namna hiyo na kwa nini watu wengi bado wanahesabu kalori, hebu tuelewe jinsi wazo hili lilivyotokea.
Kalori, kitengo cha kupima nguvu ya chakula
Kalori – neno lililotokana na neno la Kilatini “calor” linalomaanisha “joto” – iligunduliwa kwa mara ya kwanza na mtaalamu wa kemia na fizikia wa Kifaransa, Nicolas Clément, katika miaka ya 1820.
Kalori ilikuwa kipimo cha joto ambacho kinaweza kubadilishwa kuwa nishati, na kilitumika kupima kiasi cha mvuke kinachohitajika kuendesha injini za mitambo.
Hata hivyo, maana ya kalori kama tunavyoijua leo (joto linalohitajika kuinua joto la kilo 1 za maji kutoka 0 hadi 1° Celsius) iliingia kwenye uwanja wa lishe ya binadamu kutokana na kazi ya mtaalamu wa kemia wa Marekani, Wilbur O. Atwater.
Atwater alichukua likizo ya mwaka mmoja na kwenda Ujerumani, ambapo alijifunza kutumia kipima joto kinachoitwa kalorimeter, kifaa kinachotumika kupima kiasi cha joto kinachotolewa au kupokewa na miili, ambacho wakulima wa Kijerumani walikitumia ili kutoa chakula bora kwa mifugo yao.
“Aliporejea kwenye maabara yake huko Connecticut, Atwater alijaribu kurudia mchakato huu, si kwa ajili ya lishe ya mifugo, bali kwa ajili ya chakula cha binadamu,” anasema Giles Yeo, profesa wa neuroendocrinology katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza, na mwandishi wa kitabu “Why Calories Don’t Matter”.
“Hivyo akaanza kuchapisha majarida yenye maelezo ya kina kuhusu kalori zilizomo katika vyakula, kiasi gani kinatoka kwa protini, mafuta na kabohaidreti,” anaendelea.

Chanzo cha picha, getty
Kanuni maarufu tunayojifunza shuleni (kalori 4 kwa gram 1 ya protini, kalori 4 kwa gram 1 ya kabohaidreti, na kalori 9 kwa gram 1 ya mafuta), anasema Yeo, ndiyo ile ile tunayotumia leo kutathmini kalori kwenye kila kilicho kwenye vyakula na vinywaji tunavyokula.
Wakati ambapo utapia mlo ulikuwa tatizo, kuwa na taarifa hizi ilikuwa muhimu kusaidia jamii maskini kula vizuri kwa rasilimali chache.
“Awali, watu walijali zaidi ni kalori ngapi wataweza kupata kwa bei rahisi,” anasema Helen Zoe Veit, mtaalamu wa historia ya chakula katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan, Marekani.
“Hata waajiri wengine walitumia kalori kuthibitisha malipo ya chini, wakisema, ‘kulingana na hesabu ya kalori, unapaswa kuwa na uwezo wa kununua chakula cha kutosha kwa kile tunachokulipa,’” anasema pia mtaalamu huyu wa historia ya chakula.
Kutoka kwa uhaba hadi kwa utoshelezaji
Hata hivyo, mabadiliko ya kijamii yalikuwa yakijitokeza.
Mwanzoni mwa karne ya 20, wakati ambapo upatikanaji wa chakula uliongezeka—na maendeleo ya teknolojia mpya za kuhifadhi na kusafirisha chakula, idadi ya watu, hasa nchini Marekani ilianza kuongezeka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanablogu wa wakati huo
Akiwa ameelewa kazi za Atwater kupitia taaluma yake, daktari huyu alikuja na wazo la kutumia zana zilezile, lakini kwa lengo kinyume: badala ya kuzitumia kuongeza uzito mzuri, aliona kuwa angeweza kuanza kuhesabu kalori ili kupunguza kilo alizoziona kama tatizo.
Kwa kutumia mantiki ya kimaandishi (kula kidogo kuliko unavyotumia), Peters, ambaye wakati huo alikuwa na uzito wa karibu kilo 90, alifanikiwa kupunguza karibu kilo 30.
Akifurahishwa na matokeo yake, alianza kuandika mara kwa mara matokeo yake kwenye safu ya makala katika magazeti mbalimbali ya wakati huo, na kuelezea kwa kina mbinu yake katika kupunguza uzito na kupelekea kitabu chake kupata umaarufu na kuuzwa sana.
Mitindo pia ilibadilika kulingana na dhana mpya ya uzuri iliyohimiza mwili wenye umbo lililochongeka.
Mtindo mwingine ambao ulipata umaarufu wakati huo kama vile mkanda wa kiunoni ulianza kupitwa na wakati.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mafanikio ya Peters katika kubadilisha mwili wake yalikuwa na hamasa, na kitabu chake kilikuwa cha kuvutia hasa kwa wanawake (weupe na wa tabaka la kati).
“Ni kitabu kilichoandikwa vizuri,” anasema Yeo. Na ingawa leo maoni yake yangetafsiriwa kama ubaguzi dhidi ya watu wanene, maandiko yake “ni ya kufurahisha na ya kuvutia,” anasema.
Kwa vile yeye mwenyewe alikuwa na uzito wa ziada, maoni yake—yaliyokuwa na chuki na ubaguzi kwa mtazamo wa kisasa—yalionekana wakati huo kama kujikosoa badala ya kumshtumu mtu “mnene kupita kiasi”.
Uzito na Afya
Lakini kitabu hicho kilikuwa na athari kubwa kwa sababu, wakati mmoja, maono mapya ya mwili yalikuwa yakijitokeza, na pia kwa sababu uhusiano kati ya mafuta ya ziada ya mwili na afya ulianza kugunduliwa.
“Katika miaka ya 1910, ushahidi mpya ulionyesha kuwa uzito kupita kiasi unaweza kuwa na madhara,” anasema Veit.
“Tafiti zilizofanywa na makampuni ya bima, kwa mfano, zilionyesha kuwa kadri watu wanavyokuwa na uzito mkubwa baada ya umri wa miaka 35, ndivyo walivyokuwa na uwezekano mkubwa wa kufariki.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa mapendekezo ya Peter yaliangazia kalori, 22alielewa kuwa unapaswa kula kwa kiwango hitajika na ule lishe bora lakini hakukataza kabohaidreti, nyama, na maziwa. Lakini hakukataza watu kula gluteni, Yeo aelezea.
Ukilinganisha miko ya kupunguza unene kupita kiasia kama vile utumizi wa aina ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumizi wa mipira- Mkakati wa Peter haukuwa na ishara kuwa haufuati maagizo ya kiafya.
Kupendelea matumizi ya kalori
Kwa kuzingatia habari mpya kuhusu lishe, muundo wa chakula, jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi, na zaidi, tunajua kuwa njia ya kuhesabu kalori ni bora kwa kudumisha lishe bora au hata kupoteza uzito kwa njia endelevu.
Bado, hamu ya kuhesabu haijaisha kabisa katika mtindo, na wengi wanaamini kuwa mawazo haya yanachangia shida ya sasa ya unene kupita kiasi.
Kwanini tunaendelea kuhesabu?
Ingawa kalori hazina maana katika suala la afya kwa sababu hazituelezi chochote kuhusu thamani ya lishe ya chakula, Yeo anaamini kwamba watu wengi bado wanazitumia kwa sababu, kwa njia fulani, ni njia rahisi ya kuhesabu kiasi tunachokula.
"Ni njia rahisi ya kufanya maamuzi, lakini inamaanisha kuzingatia jambo lisilofaa," mtaalamu huyo anasema.
Kulingana na mtafiti, nambari "huwapa watu udanganyifu kwamba ni kitu ambacho wanaweza kudhibiti, kwamba unaweza kupanga kisayansi na kupoteza uzito, ikiwa unashikamana na chakula."
Mwishowe, kuhesabu kalori "ni pendekezo rahisi sana, la mantiki: unapaswa kutumia kidogo kuliko unavyotumia. Na hiyo imechangia kuendelea kwake kwa ushupavu."
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Asha Juma