Kenya yazindua oparesheni dhidi ya wezi wa mifugo

Kenya imeanzisha operesheni ya kuwakamata wezi wa mifugo walioua watu 11 katika shambulizi la kuvizia siku ya Jumamosi katika eneo la Turkana kaskazini mw nchi hiyo.
Maafisa wanane, raia wawili na chifu wa eneo hilo wanasemekana kuwa miongoni mwa waathiriwa wa ghasia katika kaunti ya Turkana.
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa operesheni hiyo inalenga kuwakamata wahalifu, kuwapata wanyama walioibiwa na kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo.
Iliwataka watu kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa genge hilo na kupatikana kwa wanyama walioibiwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Eneo hilo limekuwa mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame mbaya zaidi ambao mewahi kushuhudiwa Afrika Mashariki katika miongo minne.
Ukosefu wa mvua kwa misimu minne umesababisha idadi kubwa ya mifugo kufa na mazao kukauka.
Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limesema hadi watu milioni 20 katika eneo la Afrika Mashariki wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa.
Polisi wa Kenya wamelaani shambulio hilo na kulitaja kuwa "uvamizi wa uhalifu na woga" dhidi ya "wananchi na polisi wasio na hatia".
Maafisa wa ziada wametumwa katika kijiji cha Turkana Mashariki ili kuimarisha usalama na kuendeleza msako wa wale waliohusika, ambao walisema ni watu wa jamii ya Pokot.
Uvamizi wa sasa unafuatia kisa cha mwezi uliopita ambapo watu saba waliteketezwa hadi kufa katika kaunti hiyo wakati wa uvamizi wa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Pokot.
Jeremiah Lomorukai, Gavana wa Turkana, alisema wenyeji "wamechoshwa na maombolezo ya vifo vya wanafamilia wao".