Raybird: Ifahamu Droni ya siri ya Ukraine inayolenga vituo vya mafuta vya Urusi

Raybird inaweza kuruka bila kusimama kwa zaidi ya kilomita 1,000 ili kupeleleza na kupiga shabaha ndani ya Urusi.
Maelezo ya picha, Raybird inaweza kuruka bila kusimama kwa zaidi ya kilomita 1,000 ili kupeleleza na kupiga shabaha ndani ya Urusi.
  • Author, Abdujalil Abdurasulov
  • Nafasi, BBC News

Katika eneo la siri, mbali na watu, wahandisi wa Ukraine wanafanya majaribio ya ndege isiyo na rubani inayolenga masafa marefi inayofahamika kama Raybird.

Mashine hii inafana na ndege ndogo na hurushwa angani kupitia chombo maalumu

Ndege isiyo na rubani hii (Droni) ya Raybird ina uwezo wa kuruka bila kupumzika saa 20 na kufika zaidi ya kilomita 1000.

Inatumika kufanya misheni ya kipekee na pia kushambulia Urusi pamoja na askari walio vitani.

Maeneo lengwa ni vituo vya kusafishia mafuta na bohari ya mafuta.

Lakini baada ya Urusi na Ukraine kuingia kwa mkataba wa makubaliano wa kusitisha mapigano kwa siku 30 misheni za droni hiyo zimekwisha.

Vile vile, kukomesha vita ndani ya meli katika bahari nyeusi wiki hii nchini Saudi Arabia, mataifa haya mawili yaliafikiana kuacha vita hivyo ambavyo wamejadiliana kwa muda mrefu.

Rais wa Ukraine Zelensky amesema nchi yake tayari imetekeleza usitishaji wa vita .

Wakati huo, wamelaumu Urusi kwa kukiuka baadhi ya vipengee vya mkataba wa makubaliano.

Kwa upande wa Urusi wanadai Ukraine haifanyi kama inavyohitajika katika maridhiano ya amani.

Pia unaweza kusoma:
Urusi inaendelea na mashambulizi dhidi ya Ukraine, lakini inasema si kwa ajili ya nishati

Chanzo cha picha, State Emergency Service

Maelezo ya picha, Urusi inaendelea na mashambulizi dhidi ya Ukraine, lakini inasema si kwa ajili ya nishati

Hata hivyo, Alexey kutoka Skyeton, kampuni inayounda Raybird, ana wasiwasi kuhusu uwezo wa Moscow kuendelea kushikilia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Oleksiy anasema: "[Warusi] wanakupiga usoni, kisha siku inayofuata wanafanya makubaliano lakini wanakuomba ufunge mikono yako. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wataendelea kupigana."

Makubaliano haya yanaweza pia kuleta nafuu kwa Urusi.

Inakadiriwa kuwa Ukraine imefanya mashambulizi zaidi ya 30 dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Urusi kwa kutumia droni na silaha nyingine mwaka huu pekee.

Vile vile, wamevamia baadhi ya vituo vikubwa vya mafuta nchini Urusi, kama vile kiwanda cha kusafisha mafuta cha Ufa kilichozunguka kilomita 1,500 kutoka eneo linalopiganiwa, na kiwanda cha Tuapse kilichopo Krasnodar Krai.

Kwa mujibu wa ripoti za Reuters, uwezo wa usafishaji mafuta wa Urusi umepungua kwa takriban asilimia 10% kutokana na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Aidha, uamuzi wa Moscow wa kupanua marufuku ya usafirishaji wa mafuta unaonyesha kwamba wanahisi madhara ya mashambulizi haya.

Silaha za Ukraine za kushambulia kwa kina zinaendelea kuongezeka.

Rais Zelensky alitangaza hivi karibuni kuwa wahandisi wa Ukraine wameunda droni yenye uwezo wa kufika umbali wa kilomita 3,000, ambayo inamaanisha inaweza kufika si tu Moscow, bali hata maeneo ya Siberia.

Kyiv pia inadai kuwa imeunda "makombora ya droni" yenye injini ya mvuke, ambayo huruka kwa kasi kubwa na hivyo kuwa vigumu kuzuiwa.

Rais Zelensky anasema Ukraine sasa imetengeneza ndege zisizo na rubani kufikia shabaha hata huko Siberia
Maelezo ya picha, Rais Zelensky anasema Ukraine sasa imetengeneza ndege zisizo na rubani kufikia shabaha hata huko Siberia

Zelensky alieleza kuwa Ukraine imefanikiwa kupima silaha yake ya kwanza ya balistiki inayozalishwa nchini na pia imeboresha kombora lake la Neptune kwa ajili ya mashambulizi ya angani ili kushambulia malengo ya ardhini na baharini.

Inaripotiwa kuwa kombora hilo lilitumika kushambulia kituo cha anga cha Urusi cha Engels wiki iliyopita, ingawa maafisa wa Ukraine hawajathibitisha wala kukanusha ripoti hizo.

Afisa mkuu wa serikali ya Ukraine ameripoti kuwa shambulio hilo liliharibu makombora karibu mia moja ya majini ambayo yangeweza kusababisha hatari kubwa juu ya Ukraine.

Makubaliano ya kusitisha mapigano ya nishati ni habari njema kwa Ukraine.

Urusi imekuwa ikishambulia kwa ukali mitambo ya umeme ya Ukraine, na wakati mmoja mwaka jana, uwezo wa nishati wa Ukraine uliporomoka hadi theluthi moja ya kiwango chake cha kabla ya vita.

Mwezi uliopita, wakati halijoto iliposhuka chini, droni za Urusi zilishambulia mtambo wa kuzalisha umeme wa joto huko Mykolaiv, kusini mwa Ukraine.

Siku chache baadaye, shambulio jingine kubwa la angani liliacha zaidi ya wakazi 250,000 wa Odessa bila umeme na joto.

Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya gesi ya Ukraine pia yamekuwa yakiendelea kwa wingi.

Maeneo yanayo shambuliwa mara kwa mara ni pamoja na vituo vya kuhifadhi gesi vilivyopo chini ya ardhi katika magharibi mwa Ukraine na vituo vya uzalishaji katika sehemu za kati na mashariki za nchi.

Urusi imeshambulia mara kwa mara miundombinu ya nishati ya Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wake kamili mnamo Februari 2022.

Chanzo cha picha, IGOR TKACHENKO/EPA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Urusi imeshambulia mara kwa mara miundombinu ya nishati ya Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wake kamili mnamo Februari 2022.

Lengo la Moscow ni kupunguza uzalishaji wa gesi nchini Ukraine, jambo muhimu kwa usalama wake wa nishati, anasema Artem Petrenko, mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Wazalishaji wa Gesi wa Ukraine.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa kundi moja la ufuatiliaji, mwishoni mwa Machi, vituo vya kuhifadhi gesi nchini Ukraine vilikuwa vimejaa asilimia 4 pekee.

Kama Urusi itaendelea na mashambulizi yake, kujaza vituo hivi kutakuwa vigumu sana, hali ambayo inaweza kusababisha matatizo makubwa katika msimu ujao wa baridi.

Kurudi kwa uwanja wa majaribio, baada ya mizunguko michache, Raybird inafungua parachuti zake na kutua kwa mafanikio uwanjani.

Oleksiy anafurahi na matokeo hayo.

Anasema kuwa ingawa makubaliano ya kusitisha mapigano ni hatua nzuri, bado hawawezi kusimamisha kazi zao na maendeleo ya silaha mpya.

"Adui yetu anataka tu kupumzika, kujiandaa upya na kushambulia tena," anasema. "Lazima tuwe tayari kwa hilo."

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid