Ufanye nini kuzuia kuongezeka kwa uzito wako msimu wa sikukuu?

.
Maelezo ya picha, Donasi

Kuongezeka uzito wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka ni jambo la kawaida kwa watu wazima wengi.

Likizo mbalimbali za msimu zinaweza kushawishi ulaji kupita kiasi, tabia ya kukaa tu, na ulaji wa vyakula vyenye kalori nyingi.

Hapa kuna vidokezo kadhaa vya kukusaidia kuepuka kuongezeka kwa uzito wakati wa msimu wa likizo.

Unaweza kusoma

Uchunguzi unaonesha kwamba wale wanaokula bila kuzingatia wana uwezekano mkubwa wa kula kupita kiasi. Hii ni kwa sababu hawawezi kuzingatia afya za miili yao.

Ili kuzuia hili, kula kwa uangalifu na kupunguza vikwazo, ikiwa ni pamoja na kazi na vifaa vya elektroniki.

Jaribu kutafuna polepole na vizuri, hali ambayo itawawezesha kutumia kalori chache .

Inaweza pia kusaidia kuvuta pumzi chache za kina kabla ya kuanza kula. Hii inaweza kuleta utulivu na kukusaidia kuweka mawazo yako kamili kwenye sahani yako, badala ya orodha yako ya mambo mengi ya kufanya.

Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa wale wanaojihusisha na mazoea ya kula kwa uangalifu wana uwezekano mdogo wa kupata uzito mkubwa.

Mlo wako uwe na vyakula vyenye protini

Vyakula vyenye protini

Chanzo cha picha, Getty Images

Milo ya likizo kwa kawaida huwa na wanga nyingi lakini ina protini kidogo.

Hata hivyo, ni muhimu kujumuisha protini kwa kila mlo, kwa kuwa inakuza utimilifu na inaweza kuwa muhimu kwa kudumisha uzito

Kwa kweli, kula protini pamoja na milo kunaweza kupunguza ulaji wa kalori kwa kupunguza njaa na hamu ya kula.

Protini pia ni ya manufaa kwa udhibiti wa uzito kwa sababu huongeza metaboliki yako na viwango vya homoni za kupunguza hamu ya kula.

Vyanzo vya protini ni pamoja na nyama, kuku, samaki, na baadhi ya vyakula vya mimea kama maharage.

Vyakula vya nyuzinyuzi

Nyuzinyuzi ni kirutubisho kingine muhimu ambacho huchochea shibe.

Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa nyuzi lishe ulioongezeka unaweza kupunguza ulaji wa kalori kwa ujumla, ambayo inaweza kusaidia kuzuia kuongezeka kwa uzito wakati wa likizo.

Kwa bahati mbaya, vyakula vingi vya kawaida nyakati za likizo havina kiasi cha kutosha cha nyuzinyuzi.

Jitahidi uwezavyo kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi, kama vile mboga, matunda, kunde, nafaka zisizokobolewa, karanga na mbegu.

Watu wengi hutumia wakati mwingi kupika na kuoka wakati wa likizo.

Haishangazi, hii inaweza kusababisha kupata ongezeko la uzito kwa sababu ni rahisi kuonja au kujaribu.

Hata kuumwa kidogo kwa sahani za likizo kunaweza kuongeza kalori.

Kuonja chakula chako kunaweza kuwa muhimu, haswa ikiwa unawapikia wengine, lakini kumega kidogo kidogo kunaweza kuwa zaidi ya kiasi.

Unapaswa pia kuhakikisha kuwa huna njaa wakati wa kupika, kwani ni rahisi zaidi kuonja ladha kupitiliza wakati tumbo lako linanguruma.

Dhibiti ulaji wa kitindamlo (Dessert)

Kitindamlo

Chanzo cha picha, Getty Images

Dessert ziko katika kila mlo wakati wa likizo. Hii mara nyingi husababisha matumizi ya sukari kupita kiasi na ongezeko la uzito.

Badala ya kula ya kila ladha inayoonekana, zingatia tu unayopendelea na uachane na nyingine.

Njia nyingine mwingine ni kufurahia kitindamlo kwa kula polepole, njia ambayo inaweza kukufanya uhisi kuridhika zaidi na uwezekano mdogo wa kuzidisha ulaji wake.

Tumia sahani ndogo wakati wa kula

Karamu zenye chakula cha jioni ni kawaida wakati wa likizo kwani huwaleta pamoja wapendwa, ndugu, jamaa, marafiki.

Lakini sherehe hizi hazipaswi kuharibu mlo wako ikiwa unakula kwa sahani ndogo.

Watu huwa na tabia ya kula sehemu kubwa kutoka kwenye sahani kubwa, ambayo inaweza kusababisha kula kupita kiasi.

Kwa hivyo, sahani ndogo ni njia rahisi ya kudhibiti kiasi cha chakula au mlo wako.

Epuka vyakula vilivyosindikwa

Vyakula vilivyochakatwa wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka, kama vile viazi vilivyopakiwa vyema kwenye mikebe vinapatikana zaidi kuliko hapo awali.

Ingawa ni vyakula vya haraka na rahisi, vyakula hivi mara nyingi huwa na sukari nyingi na mafuta yasiyofaa ambayo huathiri uzito wako.

Ili kuzuia kuongezeka kwa uzito, chagua vyakula na upike milo yako kutoka mwanzo.

Kwa njia hiyo, unaweza kufuatilia mlo wako na kudhibiti uzito wako.

Chakula kilichosindikwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa likizo, watu wengi wana mawazo ya "nitaanza kesho", kuzingatia kula kwa afya, mawazoambayo yanaweza kuendeleza tabia zisizofaa.

Ikiwa una nia ya dhati ya kudhibiti uzito wako, inaweza kusaidia kuchora mstari, kujiwekea mipaka, na kushikamana na malengo yako kuhusu ulaji wa chakula.

Ni sawa kusema hapana kwa vyakula na tabia fulani ambazo haziendani na malengo yako.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa unaweza kuteleza mara moja au mbili.

Mara nyingi watu huacha malengo yao baada ya hali hii kutokea. Hata hivyo, ni bora kuendelea na kufanya chaguo bora zaidi wakati ujao unapokula.

Kipima uzito

Chanzo cha picha, Getty Images

Ingawa kuyasimamia malengo yako ya uzani kunaweza kuchosha wakati wa msimu wa likizo, vidokezo na njia nyingi zinaweza kukusaidia kuwa na afya njema, furaha, na kuzingatia uzito wakati huu wa mwisho wa mwaka.

Zaidi ya vidokezo vya jumla vya lishe, ni bora kuhakikisha kuwa unafanya mazoezi mengi na kupunguza ulaji wako wa vyakula visivyofaa.

Ikiwa una bidii, unaweza kubaini kwamba haujazuia tu kuongeza uzito lakini hata kupunguza uzito wakati wa msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Unaweza kusoma

Imeandikwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Abdalla