Kwanini kumekuwa na ununuzi mkubwa wa wachezaji katika ligi ya Pro league Saudia?

Cristiano Ronaldo alijiunga na Al-Nassr mnamo Desemba 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Msimu wa 2024-25 wa ligi ya Saudi Pro League unaanza leo 22 Agosti. Mwaka mmoja uliopita, ilionekana kuna mchezaji nyota aliyewasili Riyadh, Jeddah na kwingineko kila siku.

Kwa jumla, zaidi ya pauni milioni 700 zilitumika kuwanunua wachezaji kama Neymar, Karim Benzema na Riyad Mahrez miongoni mwa wengine waliojiunga na Cristiano Ronaldo Mashariki ya Kati.

"Yamekuwa majira tulivu katika soka la kimataifa," Simon Chadwick, profesa wa michezo na uchumi wa kijiografia katika Shule ya Biashara ya Skema mjini Paris, aliiambia BBC Sport.

Chadwick anajihusisha na "mchanganyiko wa hali mbaya ya kiuchumi, kuchelewa kukamilika kwa mashindano ya timu ya taifa ya bara, na vilabu katika maeneo mbalimbali kujaribu kutumia kanuni za fedha za ndani".

Pia unaweza kusoma

Ingawa kumekuwa na mawasiliano na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr, bado hakuna dili la uhamisho wa kuhama Saudi Arabia msimu huu.

Mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney ndilo jina la hivi punde linalomvutia, huku The Bees wakikataa dau la pauni milioni 35 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Al-Ahli wiki iliyopita.

"Tatizo la kutumia pesa nyingi kwenye vipaji ghali kutoka nje ni kwamba kuviendeleza kunamaanisha kuendelea kufanya hivyo daima," aliongeza Chadwick.

"Hii ni ghali, haitoi hakikisho la mafanikio, inaweza kusababisha kukosekana kwa utulivu, na kudhoofisha utendaji wa timu ya kitaifa.

"Ndani ya soka ya Saudi Arabia kuna uwezekano wa kuwa na fikra za kimkakati zaidi sasa hivi, ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita."

Kuna nguvu nyingi za nyota zilizopo nchini hata hivyo, na majina mengi makubwa bado yapo. Ligi hiyo ilipeleka wachezaji 14 kwenye Ubingwa wa Uropa msimu huu wa joto, akiwemo Merih Demiral, beki wa kati wa Al-Ahli wa Uturuki.

"Tulidhihirisha kwa kila mtu kwamba Saudi Pro League sio ligi rahisi," Demiral aliiambia BBC Sport.

"Tunafanya kazi kwa bidii sana hapa, mazoezi yetu na michezo yetu sio rahisi kama watu wengi wanavyofikiria."

'Timu nne kubwa'

Al-Ahli ni mojawapo ya 'klabu nne kubwa', zinazomilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa nchi hiyo (PIF) ambao unaunga mkono Newcastle United na walimaliza wa tatu kwenye Ligi ya Saudia msimu uliopita.

Al Hilal walitawala mchezo na kufanikiwa kushinda taji la 19 la ligi , ikimaliza alama 14 mbele ya al -Nasser hatua iliovunja rekodi yao ya mechi 34 bila kushindwa

Aleksandar Mitrovic na Ruben Neves waliwasili kutoka Fulham na Wolverhampton Wanderers. Mshambuliaji huyo wa Serbia alizidiwa tu na Ronaldo, na Neves alisaidiwa tu na Mahrez, huku safu ya ulinzi iliyojumuisha Kalidou Koulibaly ikiwa mbaya.

Swali kubwa ni lini Neymar, ambaye alicheza mechi tano pekee kabla ya kuumiza kifundo cha mguu mwezi Oktoba, atarejea.

Wapinzani wa Riyadh Al-Nassr walimaliza msimu wakiwa mikono mitupu licha ya kufunga mabao 100 na kumaliza na alama 17 juu ya Al-Ahli katika nafasi ya tatu.

Ronaldo kwa mara nyiengine tena atagonga vichwa vya habari , ijapokuwa inasalia kuonekana iwapo ataweza kupitisha au kusawazisha idadi ya magoli 35 aliyofunga msimu uliopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 anashirikiana na wachezaji kama vile Sadio Mane, Aymeric Laporte na Marcelo Brozovic.

Al-Ittihad ya Jeddah walistahili kuwa mabingwa msimu wa 2022-23, lakini walimaliza wa tano mwaka jana licha ya kuwasajili N’Golo Kante, Benzema na Fabinho. Meneja Nuno Espirito Santo hakudumu kwa muda mrefu, na pia mrithi wake Marcelo Gallardo.

Nafasi yake imechukuliwa na Laurent Blanc. Huku kukiwa hakuna ahadi ya kushiriki katika Ligi ya mabingwa barani Asia, kusainiwa kwa Moussa Diaby kutoka Aston Villa kwa takribani pauni milioni 50 katika mkataba mkubwa zaidi wa msimu huu wa kiangazi hadi sasa, mashabiki wana matumaini.

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Paris St-Germain Neymar alijiunga na klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal Agosti mwaka jana kwa mkataba wa thamani ya £77.5m pamoja na nyongeza

Chanzo cha picha, Getty Images

Majirani wa Al-Ahli pia wana utajiri wa kushambulia kupitia Mahrez, Roberto Firmino na Firas Al-Buraikan, mfungaji bora wa ligi ya Saudi.

Allan Saint-Maximin ameondoka kuelekea Fenerbahce nchini Uturuki, lakini kuna dalili katika mechi za kabla ya msimu mpya kwamba mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Firmino, ambaye hakuwa katika ubora wake msimu uliopita, anaonekana mkali.

Jeshi maarufu la klabu hiyo la mashabiki waliovalia mavazi ya kijani litataka kumaliza katika nafasi ya tatu chini ya kocha Mjerumani Matthias Jaissle mwenye umri wa miaka 36 kuwa jukwaa la kupigania ubingwa wakati huu.

"Mashabiki wetu wanashangaza sana kwa sababu, tunapokwenda kwenye mechi za ugenini, wanajitokeza kwa wingi, kama watu 20,000 kila mchezo," alisema Demiral.

"Hii ni hatua nzuri sana kwetu, haswa kama wachezaji, kwa sababu tunahisi ushabiki wao wakati wote. Katika Saudi Pro League hakuna mashabiki kama wetu, ndiyo maana tuna bahati."

Kwa jumla hata hivyo, ligi itakuwa na matumaini ya kuimarika katika wastani wa mahudhurio ya msimu uliopita ya zaidi ya 8,000. Timu nne kubwa Wanne wakubwa ndizo zinazoungwa mkono zaidi, na kuboresha idadi katika ligi iliyosalia ni jambo la kupewa kipaumbele.

pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Abdalla