Jinsi bakteria na fangasi katika utumbo wako wanavyokufanya ufikirie vizuri

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Utunzaji wa bakteria kwa wingi pamoja na vijidudu vingine vinavyoishi tumboni kunaweza kutusaidia kufikiria vyema na hata kutoa njia mpya za kutibu hali ya afya ya akili.

Kuna matrilioni na maelfu ya aina tofauti ya viumbe hivi. Viumbe hawa wengi, ikiwa ni pamoja na bakteria, archaea na eukarya, wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu kabla ya wanadamu, na wamekuwa kwa wingi na sasa wanazidi seli zetu mara nyingi zaidi.

Hakika, kama John Cryan, profesa wa anatomy na neuroscience kutoka University College Cork, anasema: "Unapoenda chooni kujisaidia unavitoa baadhi ya vijidudu hivi: na unakuwa kama binadam mpya zaidi."

Kwa ujumla, vijidudu hivi vinajulikana kama "microbiota" - na vina jukumu lililowekwa vyema katika kudumisha afya yetu ya mwili, kuanzia usagaji chakula hadi kinga.

Pia huzalisha vitu muhimu ambavyo mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza peke yake. Lakini vipi ikiwa pia vijidudu hivi vina mchango katika akili zetu? Katika kitabu kipya kinachoitwa Are You Thinking Clearly? tunachunguza sababu nyingi za ndani na nje ambazo huathiri jinsi tunavyofikiri, kuanzia jeni, utu, upendeleo, teknolojia, tangazaji na lugha.

Na kwa upande mwingine vijidudu hivi hufanya miili yetu kuwa nyumba yao na vinaweza kuwa na udhibiti wa kushangaza juu ya akili zetu.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika miongo michache iliyopita, watafiti wameanza kufichua udadisi, wakati mwingine wenye utata - na kukusanya ushahidi unaoeleza kwamba 'microbiota' kwenye utumbo haisaidii tu kuweka akili zetu katika mpangilio bora wa kufanya kazi kwa kusaidia kunyonya virutubishi kutoka kwwenye vyakula tunavyokula, lakini pia inaweza kusaidia kutengeneza mawazo na tabia zetu.

Matokeo yao yanaweza hata kuimarisha jinsi tunavyoelewa na kusaidia matibabu mapya dhidi ya hali ya afya ya akili.

Kutokana na janga la Covid-19, ambalo limekuwa na athari mbaya kwa afya ya akili ya watu katika sehemu nyingi za ulimwengu, kubaini fumbo hili kunaweza kuwa muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Utafiti unapendekeza kwamba viumbe vyetu vinaweza kuwa vinawasiliana na akili zetu kupitia njia nyingi, kuanzia kwenye kinga hadi kemikali za kibayolojia.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti mwingi katika suala hili unafanywa kwa kuwatumia panya na wanyama wengine wadogo. Ingawa ukweli ni kuwa panya sio wanadamu, lakini wanafanana kibaiolojia kwa vitu vingi.

Kuanzisha sababu kati ya ishara za viumbe hai na mabadiliko katika mawazo na tabia ya binadamu, tafiti za wanyama zimetoa maarifa ya kuvutia kuhusu mwingiliano wa ajabu kati ya bakteria na ubongo.

Utafiti, kwa mfano, unaonyesha kuwa panya "wasio na viini" (wale wasio na vijidudu vyovyote) wana uwezekano mkubwa wa kuwa na wasiwasi, na pia hawana urafiki zaidi kuliko wale walio na vijidudu.

Panya wasio na vijidudu, na wale waliopewa dawa za kudhibiti bakteria ( antibiotiks) wamegundulika kwamba rahisi kukumbwa na tabia hatarishi na wana uwezo mdogo wa kujifunza au kukumbuka.

Kwa kuchangamana na watu wengine, kwa mfano, tunasaidia bakteria tulionao mwilini kusambaa.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Tafiti kuhusu mawasiliano kati ya utumbo, ubongo na vijidudu hivi 'microbiota' bado ni chache.

Na kuna vidokezo kwamba vijidudu hivi 'microbiota' au fangasi na bakteria na vingine vidovidogo vinavyopatikana tumboni vinaweza kuathiri ujuzi wa utambuzi kwa ukubwa zaidi, pia.

Inajulikana kuwa dawa za 'antibiotics' huharibu microbiota tumboni, lakini je, vinaathiri utambuzi wetu? Utafiti mmoja wa hivi majuzi, ambao ulifuatilia afya na ustawi wa wauguzi wa kike 14,542 kwa miaka kadhaa walipokuwa wakifanya nchini Uingereza, uligundua kwamba wale ambao walikuwa wametumia antibiotics kwa muda mrefu (zaidi ya miezi miwili) walikutwa na utambuzi wa chini katika kujifunza, kumbukumbu ndogo na umakini mdogo katika kazi kuliko wale ambao walikuwa hawajatumia dawa kama hizo.

Muhimu zaidi, utambuzi wa wanawake ambao walikuwa wametumia antibiotics ulikuwa duni kidogo walipofuatiliwa miaka saba baadaye. Ingawa huu ni uunganisho tu, watafiti wanafikiri inaweza kuwa kutokana na mabadiliko yanayotokana na antibiotics tumboni.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Bado kuna safari ndefu sana katika kuelewa suala hili vizuri. Hili ni suala linalovutia sana lakini kulitafiti zaidi kunahitaji fedha.

"Kuna vijidudu vichache tu ambavyo vimefanyiwa utafiti hadi sasa," anasema Hsiao.

"Nimefurahishwa sana na fursa ya kufichua uelewa mpya wa kiufundi wa jinsi sisi na washirika wetu 'vijidudu' tunaweza kufanya kazi pamoja kukuza afya na kuzuia magonjwa." Wakati huo huo, labda sote tunapaswa kulipa kipaumbele zaidi vijidudu hivi 'microbiota' tulivyo navyo, anasema mmoja wa watafiti.