Mji wa Colombia uliosifika kwa kuwa kitovu cha 'utalii wa ngono'

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Jose Carlos Cueto
Mwandishi wa BBC Mundo,Colombia
Ninachokuambia kilitokea kabla ya janga, kabla ya utalii wa ngono kukua sana huko Medellín.
Rafiki yangu aliniwezesha kuwasiliana na baadhi ya Wamarekani. Mmoja wao, 'Herbie', alikuwa na umri wa miaka 39. Mwingine, ni Víctor, aliyekuwa na zaidi ya 40. Nilikuwa na umri wa miaka 15.
"Rafiki", yangu ambaye anayeunganisha watu wanaofanya biashara ya ngono na wateja , alikuwa mjinga kama mimi. Alikutana na mtu ambaye sio Mlatino kwenye sherehe ambapo walimuuliza wasichana, waliwasiliana na alipokea pesa kwa kila mmoja.
Walichukua asilimia moja kutoka kwa mmoja wao kwa kuwa nao kila wakati kimwili.
Mkutano wa kwanza na 'Herbie' ulifanyika huko El Poblado, katika jumba la zamani la kukodisha lililobadilishwa kuwa vyumba vya kifahari. Kulikuwa na hata dimbwi la ndani la kuogelea (jacuzzi).
Nilikuwa na wanaume wengine na tayari nilikuwa na moyo wa jiwe. Kuanzia wakati huo nilikuwa na 'Herbie' tu. Alikuwa mwema.
Victor alinitendea vibaya sana. Sijawahi kuwa pamoja naye. Alirekodi tu video ambayo sikujua mpaka nilipoitwa na polisi kutoa ushahidi.
Walifanikiwa kuifuta kwa wakati, lakini unajua mtandao ni nini: nakala na nakala ziliuzwa kwenye WhatsApp nchini Marekani.
Wakati 'Herbie' alipowekwa gerezani nilipokea vitisho na wakili wake alinipa pesa za kumsaidia kutoka, lakini nilibadilisha nambari yangu, nikafuta Facebook . Sasa nina binti, mpenzi thabiti na biashara yangu mwenyewe.
Sasa unyanyasaji wa kijinsia ni dhahiri sana. Kabla usingeona wasichana wengi katika bustani ya Lleras Park.
The Lleras

Chanzo cha picha, OSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Ushuhuda unaotolewa ni wa María Saavedra *, lakini unaweza kufananishwa na ule wa waathirika wengi, watoto wengi, ambao wananyanyaswa kingono na kibiashara kila mwaka huko Medellín.
Makazi anayoyazungumzia , El Lleras, yamezungukwa na vilabu vya usiku, migahawa na hoteli. Ni eneo maarufu la mkutano katika sekta ya kipekee ya El Poblado, ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa kitovu cha utalii wa ngono ambao hufurika jiji kutafuta ngono.
Mita chache kutoka hapa, ishara inatangaza kufungwa kwa hoteli ya Gotham, ambapo mwishoni mwa Machi polisi waligundua mtalii wa Marekani Timothy Alan Livingston alikuwa akifanya ngono na wasichana wawili wa umri wa miaka 12 na 13.

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Kesi hiyo ilisababisha kashfa iliyosababisha meya wa jiji hilo, Federico Gutiérrez, kuanzisha kampeni "dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na kibiashara, hasa kwa wasichana, wavulana na vijana katika Lleras Park" na "maeneo mengine yaliyoathiriwa" ya El Poblado.
"Hakuna mtu anayeweza kuja mjini kwa madhumuni ya unyonyaji wa watoto," alisema Gutiérrez, ambaye aliamuru marufuku ya miezi sita ya usambazaji na mahitaji ya huduma za ngono na kuweka masaa ya kufungwa kwa vilabu katika eneo hili.
Siku chache baada ya amri hiyo nilitembelea Lleras na mazingira yake kwa usiku kadhaa. Niliona, kuwa licha ya marufuku ya meya, kulikuwa bado kuna watalii wengi wa kigeni wakiongozana na wanawake wa ndani.
"Ni mara ya pili tumekuja na hii bado ni sawa: biashara hii bado nzuri na ya bei rahisi," Wamarekani wawili kutoka Chicago wananiambia.
Kuna uzio wa polisi kwenye milango ya kuingilia kwenye bustani. Mawakala wa kutafuta, kuuliza kwa ajili ya utambulisho. Ni vigumu kuthibitisha ni nani anayedai au kutoa ngono.
"Ukiangalia kwa karibu, wale wazuri wanaingia, wale waliovaa vizuri, wale ambao wanaonekana kama makahaba," mhudumu katika moja ya baa katika bustani ananielezea."Katika mazingira ya karibu utaona wahamiaji, wasio na furaha, watoto."

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Hifadhi haikuwa hivyo kila wakati. Jazmín Santa, mtafiti katika Universidad Pontificia Bolivariana, anakumbuka mabadiliko katika muongo uliopita.
"Watu walikuwa wakitoka hapa, ilikuwa ni sehemu tulivu, na ghafla tuliona wageni zaidi na zaidi wakiwasili na wanawake vijana wa eneo hilo.
Janga la covid lilipokuja kulikuwa na ongezeko la watalii, na mahitaji ya makahaba yakaongezeka. Wanawake katika ukahaba waliona uwezekano katika sekta hiyo."
"Nenda El Poblado kwa sababu wanalipa zaidi," walipendekeza kwa Valery Parra Ramírez, mfanyakazi wa ngono ambaye anasema kwamba watalii wanaotembelea eneo hilo wanaweza kushtakiwa kwa mamlaka hapa

Chanzo cha picha, Getty Images
57% ya wageni milioni 1.2 kati ya 2022 na 2023 walikuwa wanaume wenye umri wa wastani wa miaka 37.7, kulingana na Mfumo wa Upelelezi wa Utalii. Karibu nusu ya watu hao walitoka Marekani, karibu 503,000, ikifuatiwa na Wapanama (167,000) na Wamexico walikuwa (159,000).88.29% waliwasili kutafuta burudani.
Watafiti na wafanyakazi wa ngono waliohojiwa na BBC Mundo wanaunganisha ukuaji huu na umaarufu wa utalii wa maeneo ya biashara ya ngono nchini humo.
Katherine Jaramillo Díaz, mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Valientes, anasema kuwa Medellín imekuwa ikikua kutokana na ngono kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini ukuaji huo uliharakisha zaidi karibu na mwaka 2019.
"Chuo kikuu cha kwanza cha mifano ya kamera za wavuti kilifunguliwa huko Medellín, kwa ajili ya kuzungumza juu ya mji huo kama mji mkuu wa ngono ambapo wanawake walifundishwa kutoa huduma za ngono kwenye wavuti," anaelezea BBC Mundo.

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Nchini Colombia, ukahaba ni halali kwa hiari na unaruhusiwa kwa mtu mwenye umri wa miaka 18, lakini uhusiano wowote w kingono na mtoto- mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 inachukuliwa kuwa unyonyaji.Ubakaji pia ni uhalifu.
Pamoja na hayo, kesi za unyanyasaji wa kijinsia zinaendelea.
Siku ya Ijumaa, Aprili 19, Mmarekani mmoja alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Miami kabla ya kupanda ndege kwenda Medellín kwa madai ya kuwanyanyasa watoto, kwa mujibu wa mazungumzo ambayo polisi waliingilia kati na mtu anayedaiwa kuwa mlanguzi wa binadamu katika mji huo.
Kati ya 2010 na 2022, zaidi ya waathirika 3,000 wa unyonyaji, unyanyasaji na uhalifu mwingine wa kijinsia dhidi ya watoto na vijana walihesabiwa huko Medellín, kulingana na takwimu rasmi kutoka ofisi ya meya, polisi, ofisi ya mwendesha mashtaka na Taasisi ya Ustawi wa Familia ya Colombia.
Mwaka 2023, kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Valientes, waathirika wengine 329 waliripotiwa kwa uhalifu unaohusishwa na unyanyasaji wa kingono wa watoto.

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Kwa mujibu wa ofisi ya meya, El Poblado kulikuwa na ongezeko la uhalifu unaohusishwa na kukuza vitendo vya uhalifu kama vile bidhaa za utalii, "na ongezeko la 200% katika simu zinazoripoti uhalifu wa kijinsia."
Meya Gutiérrez anasema kwamba katika eneo hili ambalo "limekuwa ardhi ya mtu" kuna mtandao wa biashara ya binadamu na miundo ya uhalifu ambayo hutumia fursa ya sekta ya ngono na utalii kuwanyonya watu na kuuza dawa za kulevya.
Watafiti, wafanyabiashara, mashirika yasiyo ya kiserikali na wafanyakazi wa ngono waliohojiwa na BBC Mundo wanaamini kwamba hatua za meya katika eneo hili linalotembelewa zaidi na watalii vitabadilisha matatizo kwa jamii zingine zilizo katika mazingira magumu.
Wanaamini kuwa hatua hizi hupunguza umakini katika masuala ya msingi kama vile ukosefu wa usawa na zitasaidia kupunguza mazingira hatari ya kazi ya ngono.
Zaidi ya hayo, wanaona kwamba makatazo hayo yanainyanyapaa El Poblado na kuwanyima haki watu wanaofanya ukahaba kwa faida yao wenyewe.
Katika taarifa iliyosambazwa na BBC Mundo, katibu wa usalama wa meya Manuel Villa Mejía, alikiri "kwamba hatua hizi sio suluhisho," lakini anaamini kwamba zitawakilisha "hatua ya kugeuka katika ujenzi wa sura ya Parque Lleras."
Eneo lililobadilishwa kwa utalii

Chanzo cha picha, OSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Nyumba kadhaa kando ya hapa kuna majengo mengi ya juu ya ghorofa 6 na usalama wa kibinafsi, mabwawa ya kuogelea, mazoezi na kuna maeno makubwa ya kuegesha magari ya hali ya juu. Katika mali nyingi hizi kuna zaidi ya vyumba 5,000 vya Airbnb( nyumba za kukaa kwa muda), likiwa ni eneo kubwa zaidi katika jiji lote.
Tunapoenda katika moja ya barabara kuu, dereva wa teksi anakumbuka zamani ya kile kilichooonekana pori ambacho leo na kitovu cha utalii.
"Hakuna mtu aliyeishi katika sehemu hii kwa miaka kumi. Kila kitu kimebadilishwa kuwa sherehe, baa na hoteli. Haiwezekani kuishi kwa sababu ya kelele."
Kwenye njia hiyo hiyo, kuna duka la usambazaji wa bidhaa za sherehe ya siku ya kuzaliwa, biashara safi ya jiran.
‘’ Mtaa huu huo ambapo kuna biashara chache za jadi hujazwa na watoto usiku ," anasema karani wa duka, ambaye anapendelea kutofichua jina lake kwa hofu ya kufukuzwa kazi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nilizungumza na wafanyabiashara kadhaa karibu na Lleras. Wanalaani uhalifu, wizi, mauaji, unyanyasaji wa kijinsia wa watoto ambao katika miezi ya hivi karibuni umefikia vyombo vya habari duniani kote.
Wanavumilia ukahaba wa kisheria. Ni wa faida, wanasema.
"Tunapata pesa nyingi kutoka kwa watalii wanaokuja huku," wanaafiki wafanyabiashara kadhaa katika eneo hilo.

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Kuongezeka kwa ufuatiliaji wa polisi huko El Poblado, kama ilivyotarajiwa na wataalam, inaonekana imetokana na kwamba sehemu ya watoto hao walihamishwa kwenda sehemu nyingine za jiji.
"Tuliwaona tu kadhaa kwenye kona hapa chini, lakini sio jukumu letu kuwauliza iwapo wana kitambulisho. Hiyo ni kazi ya mawakala walioidhinishwa, lakini hakuna rasilimali za kutosha," kinalalamika chanzo kutoka Ofisi ya Ombudsman.
Nilitembelea maeneo mengine ya ukahaba ambayo siyataji, kufuatia mapendekezo ya watafiti, ili kuzuia kile kinachotokea katika El Poblado na mazingira yake kuendelea kuenea.
"Katika El Poblado ni mahali ambapo ni dhahiri zaidi, lakini kati ya wenyeji pia kuna wateja wa unyonyaji. Inatokea katika sehemu nyingi za jiji," anasema Santa, mtafiti katika Universidad Pontificia Bolivariana.

Chanzo cha picha, OSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Mjadala juu ya mtindo wa utalii
Mapema mwaka huu, Marekani ilitoa onyo kwa raia wake baada ya watalii kadhaa kupatikana wamekufa katika mji wa Medellin katika hali ya mashaka inayohusisha matumizi ya programu za kuchumbiana.
Uhalifu ambao mamlaka zinaunganisha na utalii wa ngono sio tatizo la kipekee huko Medellín. Pia hutokea katika Cartagena, Bogotá na karibu idara zote za nchi, kulingana na Jaramillo.
Lakini hapa na katika El Poblado wanaruhusu vyombo vya habari kufanya kazi kutokana na mapambano ya wazi yaliyoamriwa na ofisi ya meya na umaarufu wa kimataifa wa Medellín.
Kashfa za hivi karibuni zilichochea mjadala kuhusu utalii katika mji huo, mara nyingi huhusiana na biashara ya ngono na madawa ya kulevya "kwa bei ya chini," anasema Jaramillo.
Carlos Calle, kiongozi wa Shirika la Utalii la Wilaya ya Medellín, mabaye anasema kuwa hivi karibuni aliliambia shirika la EFE kwamba "kuna sifa mbaya kwa watalii ambao huja kwa sababu wanapata katika Medellín ni mahali pa kufanya kile ambacho hawawezi kukifanya katika nchi yao . "
Na ofisi ya meya inataja uhalifu na kesi za unyanyasaji wa kijinsia kwa "kuionyesha Medellín kama kituo cha utalii kinachohusishwa na vitendo vya uhalifu."
Licha ya uhalali wao, ukahaba na utalii wa ngono ni suala la linaloibua mgawanyiko wa maoni nchini Colombia, nchi ya jadi ya kihafidhina.
Katika Medellín niliwahoji wanawake wawili wenye uzoefu katika kazi ya ngono na maono tofauti sana.

Chanzo cha picha, Kwa hisani
Valery Parra Ramírez, ambaye pia ni rais wa chama cha wafanyakazi wa ngono wa Antioquia, anakosoa "maadili ya mara mbili ya Medellín" na anaongeza kuwa "ingawa unasumbua, ukahaba unakuza uchumi nchini Colombia."
"Kuwanyanyasa wageni au sisi sio suluhisho la kutokomeza unyonyaji wa watoto, ambao tunalaani kama uhalifu mwingine. Kama watafunga Lleras, mtalii huyo huyo anatafuta mvulana au msichana karibu na mji na kuwapeleka kwa teksi nyumbani kwao."…Au Nyumba za makazi ya muda (Airbnb), ambapo ni vigumu zaidi kudhibiti nani anakuja na kwenda," anasema
Ndiyo maana anawaomba wale wanaofanya kazi kwa hiari na kwa manufaa yao wenyewe walindwe, kwamba shughuli zao zisichanganywe na uhalifu na kwamba udhibiti uongezwe kwenye makazi ambayo "yanaruhusiwa" na unyonyaji wa watoto.

Chanzo cha picha, OSÉ CARLOS CUETO / BBC NEWS WORLD
Mary Luz López Henao, mwandishi, mfanyakazi wa zamani wa ngono na mwathirika wa unyonyaji na usafirishaji, ananipa mtazamo mwingine.
"Katika nchi maskini, yenye ubaguzi wa rangi, katika vita na nchi isiyo na usawa kama Colombia, hakuna fursa za kutosha za kuchagua kwa uhuru."
Kwa sababu ya matatizo haya, López Henao anaelezea jinsi ilivyo vigumu kutoka kwa ukahaba na kuzuia wasichana, wavulana na vijana kuangukia katika hali za unyonyaji au mitandao.
"Leo mabinti na wajukuu wa wenzangu ambao walifanya kazi nami ni makahaba."
López Henao anajuta "picha" ambayo Medellín anatoa na hii, na kuwafanya wageni wengi kufikiri kwamba "hapa sisi ni coke tu au makahaba."
"Ni jambo la kudhalilisha kwamba wanawake wenye shida zaidi wanakanyaga tu El Poblado ili kufanya ukahaba au kusafisha nyumba za matajiri."
Nikirudi Lleras, naweza kuwaona wafanyabiashara husafisha kwa nyumba zao muda mfupi baada ya mchana.
Kuna masaa machache tu yaliyobaki kabla ya kitongoji hicho tena kufurika watalii wa kigeni, wakivutiwa na mji ambao unapambana na upande wa giza wa utalii wa ngono.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi