Fahamu teknolojia mpya ya tiba ya usahaulifu kwa kupandikiza kifaa cha kielektroniki kwenye ubongo

Ubongo

Chanzo cha picha, Getty Images

Kutoka kwenye kifaa cha kupandikiza kwenye moyo kudhibiti matatizo ya moyo hadi kifaa cha cochlear ili kuboresha uwezo wa kusikia, maisha ya mamilioni ya watu tayari yamebadilishwa kwa kupandikizwa kwa vifaa vidogo vya kielektroniki.

Sasa, timu ya Cambridge kutoka sekta ya afya, sayansi na biashara imepewa ufadhili wa mamilioni ya dola kugundua kwa haraka teknolojia mpya zinazolenga kuboresha afya ya ubongo.

Watafiti kote Uingereza watapewa fursa za kufanya majaribio. Itatumia matokeo ya kutibu watu wanaougua shida ya akili, unyogovu na maumivu sugu.

Profesa George Mellieras, mmoja wa wanasayansi wakuu kwenye timu ya Cambridge, anatumai tangazo hilo litasaidia mradi wake mpya.

Unaweza kusoma

Teknolojia ya kusaidia kutibu matatizo ya afya ya akili

Chuo Kikuu cha Cambridge kinakadiria kuwa baadhi ya matatizo ya neva na kiakili huathiri watu wanne kati ya watano. Timu ya Profesa George Melliaras inatafiti vifaa vidogo ambavyo vinaweza kuwasaidia kutoa matibabu.

“Vipandikizi vya Ubongo vinaweza kutoa tiba mpya ya magonjwa ambayo hayawezi kutibiwa kwa dawa,” anaeleza Profesa Melliaras.

"Orodha ya magonjwa ya aina hiyo inaendelea na kuendelea. Lakini tunachozungumzia hapa ni majeraha ya ubongo na uti wa mgongo, Parkinson's, amnesia, depression, obsessive-compulsive disorder. Na ni Rheumatoid Arthritis, type Inatarajiwa kusaidia kutibu Aina. 1 kisukari," alisema.

Pia alisema kwamba ulikuwa utafiti unaofaa na wa kutia moyo sana.

Mabadiliko katika namna neva zinavyofanya kazi

Prof George

Chanzo cha picha, Martin Giles/BBC

Vifaa hivi vilivyopandikizwa mwilini hutuma mawimbi madogo madogo ya umeme ili kubadilisha jinsi niuroni katika miili yetu inavyofanya kazi. Seli za neva zinazoitwa niuroni husambaza ujumbe kati ya mwili wetu na ubongo kupitia msukumo wa umeme.

Wanadhibiti mwelekeo wetu wa kutembea, kuzungumza, kula na kupumua. Watafiti wanaamini kwamba kwa kubadilisha jinsi niuroni hizi zinavyofanya kazi, zinaweza kupunguza maumivu au kuchochea tena maeneo yaliyoathirika ya ubongo.

"Tayari tunajua kuwa kutumia kichocheo cha umeme kunaweza kupunguza kutetemeka kwa baadhi ya watu wenye kifafa," anasema Profesa Melliaras, "lakini ili kuendeleza aina hii ya teknolojia tunahitaji kuleta pamoja timu ya wahandisi, madaktari na viwanda kote Uingereza."

Changamoto ni nini?

Choukun Tong, daktari anayefanya utafiti katika Chuo Kikuu cha Cambridge

Chanzo cha picha, Martin Giles/BBC

Ukubwa wa chombo hiki ni changamoto kwa watafiti.

"Elektrodi zinazotoka kwenye kifaa hiki hazipaswi kuwa kubwa kuliko neuroni moja. Ukubwa huu ni mdogo mara tano kuliko kipenyo cha nywele za binadamu, "anataja Profesa Melliaras.

"Lakini kifaa kikiwa kidogo sana, kitakuwa na matatizo katika kuwasiliana na mwili. Madaktari wanaweza kupata ugumu wa kukipandikiza kwenye mwili wa mgonjwa. Kinapaswa kuwa suluhisho la matatizo yote mawili kwa usawa," aliongeza.

Pia, lazima wahakikishe kuwa kifaa cha kuingiza sauti kimezalishwa kwa wingi, kwa gharama nafuu, na hakina madhara kwa wagonjwa.

Vipandikizi vya matibabu si vipya kwa wahandisi hawa. Dk. Chaukun Tong anatengeneza kifaa ambacho hufunika mishipa dhaifu bila kuiharibu.

Dong anatafiti nyenzo ambayo inaonekana kama utepe mdogo kwenye kiputo cha kioo. Imetengenezwa kwa polima iliyowekwa dhahabu.

Wakati umeme unatumika, hujikunja kwa hiari. Vifaa hivi husaidia kufuatilia ishara za msukumo kutoka kwa neva na kuzichochea wakati wa upasuaji tata.

Umeme umetumika kwa muda mrefu kutibu magonjwa mengi

Chanzo cha picha, Martin Giles/BBC

Umeme umetumika kwa muda mrefu kutibu magonjwa mengi. Tiba ya Electroconvulsive (ECT) kama matibabu ya msongo mkubwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo ilianza miaka mingi iliyopita.

Lakini Melliaras anaamini kwamba, ingawa utaratibu wa upasuaji utafuatwa ili kutoshea vifaa vya kupandikiza, itakuwa na manufaa kama matibabu ya mara moja kwa magonjwa hayo.

Vifaa vinavyoweza kupandikizwa vinaweza kugundua shughuli isiyo ya kawaida kwa kufuatilia ubongo kila mara na kurekebisha kwa upole inapohitajika, anasema.

Matokeo ya utafiti uliochapishwa na wanasayansi wa Marekani mwaka 2021 yalikuwa na matumaini kwamba suluhu inaweza kupatikana kwa kupandikiza vifaa vya kuingiza kwenye ubongo ili kutibu uchovu mkubwa wa kiakili.

ARIA, wakala unaoungwa mkono na serikali, utafadhili Mkataba wa Cambridge kwa miaka mitatu.

Profesa Melliaras ana uhakika kwamba ndani ya kipindi hiki, wataweza kufika mbali katika kutafiti tiba mpya.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga