Mambo 5 rahisi unayoweza kufanya na kufurahia wakati wa msimu wa sikukuu

Kupiga violin

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipindi cha sikukuu, hasa cha mwisho wa mwaka, watu wengi ni wakati wao wa kupumzika na familia zao.

Ni kipindi cha likizo hivyo walio wengi hawapo kazini, huwa mapumzikoni kujiweka mbali kidogo na shughuli za kila siku kama ilivyo ada.

lakini wakati huu ni vitu gani hasa unaweza kuvifanya wakati huu wa mapumziko ya sikukuu na ukavifurahia?

Unaweza kusoma

Kuendesha baiskeli

Mama akiendesha baiskeli

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwakuwa ni kipindi cha mapumziko tulio wengi hujipweteka wakati huu, maana yake kutoushughulisha mwili wala akili, isipokuwa ni kula, kunywa na kulala.

Kuepuka hali hii tunaweza kuanzisha tabia ya kuushughulisha mwili kwa namna ya kufurahisha kama kuendesha baiskeli.

Ingawa ni zoezi la kushughlisha mwili lakini linatujenga kiafya pia.

Utafiti umeonesha manufaa yanayotokana na kuendesha baiskeli au kutembea

Hupunguza hatari ya mtu kuugua kisukari, maradhi ya moyo na aina kadha za saratani.

Uchambuzi katika Jarida la Uingereza la Sports uliangalia utafiti uliochapishwa kuhusu faida za mazoezi katika karibu tafiti 100 kubwa na karibu nakala 200 zilizopitiwa ili kupata muhtasari wa ushahidi.

Waligundua kwamba ikiwa kila mtu atatenga angalau dakika 150 za mazoezi kwa wiki, basi karibu kifo kimoja kati ya sita vya mapema huzuiwa.

Watafiti wanasema kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ndio jambo linalohitajika.

Mapishi

Chakula

Wakati huu ambapo jamii na familia zetu zinakutana pamoja, kuna shughuli ambazo zinaweza kufanywa kwa pamoja na kufurahia, ikiwemo mapishi, hii ni tabia ambayo inaweza kujengwa katika kipindi hiki kifupi wakati wa sikukuu.

Kupika kama familia moja ni jambo linalofurahisha sana kwasababu linawaleta wana jamii pamoja na kuwa na mahusiano yenye nguvu kupitia chakula.

Mapishi huwezesha kuibua hisia na kumbukumbu kupitia hisia za kuonja na kunusa. Kama vile ilivyo kwa msanii anayetumia rangi, umbile, na umbo kuunda mchoro,

Mapishi ya kutumia viambato, vionjo, ni ubunifu wa kufurahisha sana kwani hufanya familia, jumuia kuyafurahia mapishi wakati huu wa mapumziko.

Hata kama hujawahi kupika hapo awali, ni sawa kwa sababu unaweza kuanza na mapishi rahisi na kuandaa yale yaliyo magumu zaidi kadiri unapopata uzoefu.

Kumbuka kujipa nafasi ya kufanya makosa na kujifunza kutoka kwayo, ili uweze kufurahia mchakato wa kupika na milo ya ladha inayokuja nayo.

Kupika ni muhimu kwa sababu ya mchakato wa kupika chakula tangu mwanzo. Ni aina ya sanaa inayoleta furaha na kuridhika.

Kujitolea

Kijana akijitolea kufanya usafi

Chanzo cha picha, Supplied

Ingawa msimu wa likizo ni wakati wa mambo ya kujifurahisha na ya kujistarehesha, pia ni fursa ya kujiburudisha na kuleta matokeo chanya.

Kujitolea ni njia ya kuridhisha na yenye maana ya kutumia muda wako wakati wa likizo, na inaweza kuleta furaha na utoshelevu mkubwa.

Fikiria kujitolea katika makazi ya karibu au kwenye ghala ya chakula, ambapo unaweza kusaidia kutoa chakula kwa wale wanaohitaji.

Shiriki katika michezo au matukio ya kufunga zawadi ya likizo ambayo huleta furaha kwa watoto wasiojiweza.

Iwapo una ujuzi au utaalamu mahususi, kama vile kufundisha, huduma za afya, au ufundi, zingatia kutoa huduma zako kwa mashirika au watu binafsi ambao wanaweza kufaidika kutokana na ujuzi wako.

Kujifunza kupiga Ala

Ala za muziki

Chanzo cha picha, Getty Images

Muziki una nafasi ya pekee katika msimu wa likizo, na kujifunza kupiga ala kunaweza kuwa jambo la kuridhisha na la kufurahisha.

Ni kitu chenye nguvu ya kuwaleta watu pamoja bila kujali lugha. Unaweza kujifunza wimbo kutoka nchi nyingine lakini pia kujifunza jinsi ya kupiga ala ya kitamaduni.

Iwe ni kinanda, gitaa, violin, mrimba au ala nyingine yoyote, muziki hukuruhusu kutengeneza nyimbo zako za sherehe.

Kuna mafunzo na programu nyingi zinazofaa kwa wanaoanza kujifunza zinazopatikana ili kukusaidia kuanza kujifunzia.

Unapoendelea, unaweza hata kuwashangaza wapendwa wako kwa maonesho ya muziki wa likizo ambayo huongeza ladha maalum kwa sherehe za mwisho wa mwaka.

Kutunza bustani

Bustani ya mboga za majani

Chanzo cha picha, Getty Images

Kupanda bustani ni mchakato wa kukuza mimea kwa ajili ya mboga, matunda, maua, mimea, na kuonekana ndani ya eneomaalum.

Bustani hutimiza madhumuni mbalimbali, hasa uzalishaji wa maeneo yanayopendeza, dawa, vipodozi, rangi, vyakula, sumu, makazi ya wanyamapori na bidhaa zinazoweza kuuzwa.

Kulima bustani katika kipindi hiki kunafanya uwe na mahusiano mazuri na mazingira ambayo huyapa muonekano mzuri mazingira ya nyumba, pia unapata lishe kutokana na mazao.

Utunzaji wa bustani ni burudani ya kupumzika na yenye faida ambayo inaweza kupunguza mafadhaiko na wasiwasi. Inaweza pia kukupa hisia ya kufanikiwa wakati mimea inakua.

Katika kipindi hiki ambacho muda mwingi watu wangependa kutumia kwenye skrini, bustani ni njia nzuri kwa kizazi cha kidijitali kuunganishwa na mazingira ya asili. Kupanda matunda na mbogamboga.

Msimu wa likizo hutoa fursa ya kipekee ya kuchunguza mambo mapya ya kufurahisha na shughuli za kina na starehe katika maisha yako.

Iwe utachagua kufurahisha hisia zako kwa kuoka, kukumbatia ubunifu wako kwa kutengeneza, au kulisha akili yako kwa mafumbo, kuna jambo la kufurahisha kwa kila mtu kufurahia wakati huu wa sherehe za mwaka.

Kwa kufuatia mambo haya ya kufurahisha, unaweza kuweka kumbukumbu za kudumu, uhusiano na wapendwa wako, na kutumia vyema msimu wa likizo huku ukifurahia mambo unayopenda na yanayokuvutia.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga