Sare za 9 za kuvutia zitakazovaliwa na wachezaji katika Olimpiki 2024

Chanzo cha picha, Left on Friday
Kuanzia mavazi ya kuvutia ya voliboli hadi mavazi maridadi ya kuteleza, hafla ya mwaka huu - katika mji mkuu maarufu wa Ufaransa - imeitwa "Olimpiki ya mtindo". Haya ni baadhi ya mavazi yanayothibitisha hilo.
Paris, jiji linalosifika kwa mitindo, Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 na Michezo ya Walemavu. Lakini yote hayaishi hapo - kabla ya Michezo, kuna maonyesho katika mji mkuu wa Ufaransa yanayoadhimisha uhusiano kati ya mitindo na michezo. Kando, Vogue imejitolea ukurasa wa mbele kwa hafla hiyo, na jarida hilo lilifanya sherehe ya Ulimwengu wa Vogue katika jiji hilo. Huku lebo zilizo nyuma ya sare zikiinua mchezo wao kwa mtaji wa mitindo, tumekusanya baadhi ya mavazi maarufu ya timu.

Chanzo cha picha, Lulumelon
1. Timu ya Canada ikiwa na lululemon
Mwaka huu, Timu ya Canada itavaa moja ya chapa maarufu nchini, lululemon, kwa sherehe ya ufunguzi na nyakati wakiwa uwanjani. Ukiangalia kifurushi hicho kwa mbali, mandhari bora ni vivuli vya rangi nyekundu, lakini vuta karibu kidogo na utaanza kuona maelezo ya uchapishaji tata. Kuna mimea na wanyama katika chapisho ili kuonyesha mandhari kubwa na tofauti ya nchi. Kwa mchambuzi wa mitindo na muundo Elizabeth Segran, ni "sanduku kamili".
Anaiambia BBC, "Idadi ya watu wa Canada imezidi kuwa tofauti, na kwa kweli nadhani lululemon ilizingatiwa ili kuwasaidia wanariadha kujihisi kuwa karibu na wanariadha wenzao".
Segran anavutiwa sana na mavazi yatakayovaliwa wakati wa sherehe ya kufunga mashindano hayo. "Hiyo iliundwa na msanii wa Asili [Mason Mashon, kutoka Saddle Creek Cree Nation], na inaonyesha aurora borealis kwa njia hii nzuri sana, ya mbele ya mitindo na yenye maana".
2. Timu ya Canada (sehemu ya 2)
Timu ya Canada inapata majina mawili ya heshima hapa, kama mojawapo ya nchi zinazochagua chapa ya kuanzia ili kubuni baadhi ya sare zao zinazoshindana. Ikiwa huna habari Left On Friday ni Chapa bora ya mavazi ya kuogelea itakayovaliwa na timu ya voliboli ya Canada.
Shannon Savage alibuni mavazi hayo akiwa na Laura Low Ah Kee na anaambia BBC kwamba anafurahia sana kuhusishwa na chapa yao, kile anachoita, "Olimpiki ya mtindo zaidi".
"Kuwa sehemu ya mashindano haya ya kimataifa ya Paris ambapo kila mmoja anaangazia kile walichovalia wanariadha, sio tu jinsi wanavyocheza, ni fursa kwetu kama chapa ndogo ambayo inavutia."
Kuhusiana na jinsi walivyovutia Canada, Low Ah Kee anasema lengo lilikuwa kusherehekea rangi nyekundu na vionjo vyake tofauti.

Chanzo cha picha, Getty Images
3. Timu ya Ufaransa ikiwa na Stephane Ashpool
Hatuwezi kuzungumzia 'mavazi ya Olimpiki ya Paris bila kujumuisha taifa mwenyeji. Katika michezo yote, wanariadha wa Ufaransa watashiriki wakiwa wamevalia mavazi ya mwanamitindo Stéphane Ashpool, inayojulikana zaidi kama Pigalle. Sare hiyo ina msukumo wa miaka ya 90 na inaangazia rangi za bendera ya Ufaransa.
Kwa mtindo wa kawaida wa wakazi wa Paris, inaonekana ilizinduliwa katika Wiki ya Mitindo ya Paris, ambapo Ashpool alielezea mbinu yake: "Wanariadha waliniambia wanataka kuwa na muonekano wa msichana mrembo, kifahari na wenye mvuto. Matokeo yake ni rangi hizi zilizochanganywa."
Seti hizo zimesifiwa sana kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok na katika tasnia ya mitindo pia. Lou Lewer ni mbunifu ambaye alifanyia kazi sare za London 2012 kwa Timu ya Great Britain, na anaiambia BBC kuwa amefurahishwa sana na mitindo ya kuvutia ya Ashpool.
"Inashangaza jinsi alivyoshona suruali nyeupe kwa kutumia mkanda wa ngozi. Anachanganya mavazi ya michezo na ushonaji nguo kwa namna ambayo sijawahi kuona uwanjani."

Chanzo cha picha, Team GB/ Adidas
4. Timu ya Uingereza na Adidas
Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 40 ya Adidas kuwa mshirika rasmi wa mavazi ya michezo wa Timu ya Uingereza, kwa hivyo wanariadha wa Uingereza watavaa tena chapa ya Ujerumani msimu huu wa joto. Akiwa amewahi kufanya kazi na Adidas kwenye vifaa vya London 2012, anajua kwanza vipaumbele vya wanariadha wa Timu ya Ungereza ni Lewer .
Anaiambia BBC: "Ni muhimu sana wanariadha kuhisi kuunganishwa na timu yao. Hiki ndicho kilele cha kile ambacho wamekuwa wakifanyia mazoezi kwa miaka mingi, na wanataka sana kuwakilisha nchi yao, na ionekane. "
Mwaka huu, Lewer anabainisha kuwa Adidas wamehifadhi utamaduni, kwa kutumia rangi za Union Jack na kuangazia bendera kwa uwazi kwenye miundo yote. Huenda pengine unajiuliza uamuzi wa kuwa makini unahusishwa na utata wa mwaka jana kuhusu jezi za soka za Uingereza zilizobuniwa na Nike, ambazo ziliangazia St George's Cross kwa kutumia rangi ya zambarau na bluu.
"Watu wanaweza kuwa na ulinzi mkubwa dhidi ya bendera, ndiyo maana wakati mwingine inafanya kazi vyema zaidi kuzichanganya na muonekano wa kitamaduni."

Chanzo cha picha, Ralph Lauren
5. Timu ya Marekani na Ralph Lauren
Tangu 2008, mwanamitindo mkubwa wa Marekani Ralph Lauren ameunda mavazi ya sherehe kwa Timu ya Marekani, na mwaka huu sio tofauti. Taarifa iliyotolewa na chapa hiyo inasema mwonekano "unakumbatia uzalendo uliyoakisiwa katika saini ya rangi nyekundu, nyeupe na bluu".
Watengezaji wa sare hizo wameamua kutumia mitindo tofauti kabisa kwenye sare za sherehe za ufunguzi na kufunga. Sherehe ya ufunguzi ni rasmi, na inaangazia mshono wa kawaida wa Ralph Lauren, na wanariadha wamevaa jaketi zilizofungwa, tai zilizounganishwa, mashati ya mistari na suruale ndefu ya jeans.
Sio kila mtu aliyevutiwa, baadhi ya wachambuzi wanasema timu inaonekana kama imevalia sare ya shule ya kibinafsi. Mavazi ya sherehe ya kufunga ni ya kawaida zaidi, yanajumuisha jaketi za mtindo wa gari zenye viraka na jeans nyeupe.

Chanzo cha picha, Puma
6. Timu ya Jamaica na Puma
Sawa na Uingereza, timu ya Olimpiki na Paralimpiki ya Jamaica wanatunza utamaduni wao kwa kuvaa rangi za bendera ya nchi; michirizi ya rangi nyeusi, manjano angavu na kijani kibichi. Kwa mara nyingine tena, mavazi yao yameundwa na Puma.
Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Arne Freundt alisema kuwa muundo wa mwaka huu unaambatana na "kasi na mtindo", na umeundwa ili kuonekana mzuri wakati unapotembea: "Mistari iliyopunguzwa imewekwa kimkakati ili kusisitiza umbo la wanariadha huku ikitoa picha ya kuvutia. Hii inasisitiza uzuri wa mwanariadha katika mwendo."
Puma imefadhili wanariadha wa Jamaica tangu 2001. Kwa kawaida wakati wa kufanya kazi na timu inayoenda kasi kama hii, kila kipengele cha kitambaa kinahitaji kuzingatiwa, kama Freundt anavyoelezea.
"[Tulitumia] kitambaa cha jacquard kilichobuniwa kwa ajili ya kupunguza joto na uwezo wa kupumua, kwa teknolojia ya thermoadapt kudhibiti halijoto ya mwili ili kuwezesha utendakazi bora."
7. Timu ya Ureno na Cariuma
Wakati baadhi ya nchi zinachagua kasi, zingine zinatetea uendelevu. Chapa endelevu ya Skate ya Brazil Cariuma iko nyuma ya mavazi ya timu za skate za Ureno, Slovakia na Uholanzi.
Kuvutia timu ya taifa ni changamoto zaidi wakati si nchi yako lakini mbunifu mkuu Pedro Andrade anaambia BBC kwamba hakuna kitu ambacho hakiwezi kutatuliwa kupitia utafiti. Ilipofika Ureno, Andrade anasema alitiwa moyo na utamaduni wao wa soka. "Imejaa msisimko na ina shauku, kwa hivyo nilienda na kitu ambacho kinalingana na ubora huo." Matokeo yake ni jezi nyekundu yenye vitalu vya teal na buluu iliyokolea.
Kila kitu cha Cariuma huundwa kwa kuzingatia uendelevu, na vifaa vya michezo sio ubaguzi. Jezi za skate zinafanywa na chupa za plastiki zilizosindikwa, ambazo kwa bahati nzuri kwa wanariadha, hufanya kukausha haraka na kitambaa cha ultra-breathable. Muhimu, kwani joto kali linaweza kuwa la kawaida nchini Ufaransa wakati wa kiangazi.

Chanzo cha picha, Asics
8. Timu ya Japani na Asics
Kwa mara nyingine tena, Timu ya Japani itavalishwa na Asics kwenye Michezo ya mwaka huu. Kama Cariuma, chapa hiyo pia inaweka uendelevu mbele.
Kwa kujumuisha matumizi ya nyenzo zilizorejeshwa na nishati mbadala, kampuni inadai kuwa imepunguza utoaji wa gesi wa jaketi za jukwaa na suruali kwa takriban 34% ikilinganishwa na Michezo ya awali.
Muundo ni rahisi na unazingatia vivuli viwili vya rangi nyekundu, "Japan nyekundu" na "jua jekundu", mwisho ulisema kuelezea joto la anga ya asubuhi ya Paris.
9. Timu ya Uholanzi na The New Originals
Jinsi orodha ya michezo inavyotofautiana katika kila Michezo, ndivyo wabunifu walio nyuma ya vifaa hivyo. Mwaka huu, breakdancing itafanya kwanza. Kinachovutia timu ya densi ya Uholanzi ni chapa ya Amsterdam The New Originals. Ilianzishwa mwaka wa 2015, inatengeneza mavazi ya utendaji kwa wabunifu.
Kwenye Instagram, kampuni hiyo inasema "imeshirikiana kwa karibu na wacheza densi kuunda sare zinazofaa kila moja ya mitindo yao tofauti". Matokeo yake ni tracksuit ya mtindo wa miaka ya 80, inayocheza kwa rangi za bendera ya Uholanzi na rangi ya chungwa ya timu ya taifa ya kandanda.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Seif Abdalla