Faida za kuota jua kwa moyo, hali na mfumo wa kinga (na ni kwa muda gani inashauriwa kufanya hivyo)

Mujer caminando bajo el sol

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kila mtu anafahamu uhimu wa kujikinga na jua. Lakini ukweli ni kwamba miili yetu inahitaji jua

Mwangaza wa jua unaweza kuboresha hali zetu, kupunguza kiwango cha chini cha msukumo wa damu, kuimarisha mifupa yetu, misuli, na hata mfumo wetu wa kinga ya mwili.

Na kukaa kwenye jua kwa muda mfupi kunaweza kutosha kuvuna faida zote hizi.

Nguvu ya jua

Kimsingi, bila mwangaza wa jua wa moja kwa moja, miili yetu haiwezi kutengeneza vitamini D, kirutubisho ambacho hufanya mambo kadhaa katika miili yetu.

Wakati mwangaza wa jua unapopiga kwenye Ngozi yetu, mwili huufyonza na kuutengeneza kuwa nguvu hii ya virutubisho.

Wakati jua linapochomoza kwenye Ngozi yetu, mionzi yake hutengeneza vitamini D.

Baada yah apo, huchukua dakika kadhaa kwa kipindi cha kabla ya kutengenezwa kwa vitamini D hadi kutengenezwa kwa vitamini D. Ni joto la mwili ambalo hufanya mabadiliko haya," anaeleza Ann Webb, profesa wa mionzi ya jua katika Chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.

Tunahitaji vitamini D, kwa mfano, kwa ajili ya miili yetu kufyonza madini ya calcium na fosphati kutoka kwenye chakula; madini yote hay ani muhimu kwa afya ya mifupa, meno, na misuli. Na haijalishi una umri gani.

Utafiti wa hivi karibuni hata umeonyesha kuwa kupata vitamini D huimarisha misuli miongoni mwa wanariadha, na uwezekano wa kuwa kichocheo cha ukuaji wa seli za misuli.

Lakini faida za vitamini D ni zaidi ya kuimarisha mifupa yetu na misuli.

"Inaonekana kuna Ushahidi kwamba inachangia katika mfumo wa kinga mwili, Pamoja na kusaidia kulinda mwili dhidi ya aina za saratani na magonjwa ya mfumo wa kinga ," aliongeza profesa Webb.

Utafiti huo ulionyesha kuwa watu wenye viwango vya chini sana vya Vitamini D wana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari, na magonjwa ya ubongo kama vile dementia. Vitamin D ni muhimu muonekano wa ngozi yetu.

Plato de salmón

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya vyakula kama vile samaki mwekundu- salmon, ni vyanzo vya vitamini D, lakini ni vigumu kupata vitamini hii ya kutosha kwa njia mlo pekee.

Ni ukweli kwamba unaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula vya aina fulani, kama vile mayai, maziwa na mafuta ya samaki . Lakini ni vigumu sana kupata kiasi sahihi kwa njia chakula pekee.

Kwa bahati nzuri, tunaweza kupata dozi ya kila siku kwa kuota jua (na bila garama yoyote)

Ni zaidi ya vitamini D

Lakini vitamini D sio faida pekee tunayoipata kutokana na jua.

Tunafahamu jinsi mwanagaza wa jua unavyokuwa mzuri ; Hiyo ni kwasababu kuota jua huboresha hali zetu na kuongeza uwezo wa ubongo wa kutoa homoni zinazoitwa serotonin , ambazo husaidia mtu kujihisi mtulivu na kuwa makini.

Vitamina D

Chanzo cha picha, Getty Images

Si ajabu kwamba wakati wa msimu wa majira baridi katika ncha ya dunia , ambako kuna mwangaza mdogo wa jua, watu hupata ukosefu wa kumakinika wa kipindi (SAD), aina fulani ya msongo wa mawazo unaotokana kuwa na viwango vya chini vya homoni za serotonin.

Tafiti zimeonyesha kuwa tuna viwango vya juu zaidi vya serotonin katika damu yetu katika siku zenye jua la kutosha ikilinganishwa na siku zenye wingu jeusi.

Zaidi ya hayo, tafiti zimeonyesha kuwa mwangaza wa jua wa moja kwa moja husababisha utengenezwaji wa seli za ngozi.

Muda wa kuota jua

Lakini kuota jua kunapaswa kuwa kwa uangalifu ili kuepuka kuungu, saratani ya ngozi na kuzeeka mapema.

Kiasi cha jua kinachohitajika kutengeneza kiwango kinachofaa cha vitamini D kinategemea kwa kila mtu; Inategemea aina yako ya ngozi, kule unakoishi na uwezo wa mwili wako wa kupokea jua. Kitu cha muhimu zaidi ni kutojichoma.

Ngozi nyeusi zaidi, kwa mfano ina kiwango cha juu cha rangi ya melanin , kiungo kinachofanya kazi kama kinga ya kuungua kwa mwili, kwa kufyonza mionzi na kuilinda ngozi dhidi ya kuharibika.

Na hii husaidia kuzuwia kutengenezwa kwa Vitamini D kwa urahisi, hivyo unahitajika kukaa kuota jua kwa muda mrefu zaidi.

Mujeress tomando el sol

Chanzo cha picha, Getty Images

Kidogo na mara kwa mara

Unaweza kutamani kuota jua mara kwa mara, lakini vitamini D huzalishwa mara unapotoka nje ya nyumba yako. Na pia kupunguza ukaaji wa muda mrefu zaidi pia ni njia bora aidi ya kuepuka madhara ya kuungua kutokana na jua.

"Vitamini D hupatikana mara tu unapoota jua kwa mara ya kwanza, kwahiyo pata jua ," anasema Webb.

Kama unakwenda kuota jua kwa muda mrefu na unakabiliwa na uwezekano wa kuungua kwa jua, ni muhimu kulinda ngozi yako.

" Ujumbe muhimu ni usiwahi kujiunguza kwa jua, hilo ni muhimu sana," aliongeza.

Ni muhimu kukumbuka kwamba baadhi ya vipodozi vya mwili, na hata dawa, zinaweza kuathiri uwezo wa mwili wako wa kuhimili mionzi ya jua.

Aplicación de protector solar

Chanzo cha picha, Getty Images

"Iwapo una ngozi isiyoweza kuhimili jua, unapaswa kuwa mwangalifu. Ni muhimu kujua ngozi yako mwenyewe. Unapaswa kuwa mwangalifu iwapo unakunywa dawa ambayo inaweza kusababisha ngozi yako kushindwa kuvumilia mionzi ya jua.

Iwapo unatumia baadhi ya kidhaa za vipodozi kama vile losheni, ambazo zinaweza kusababisha ngozi yako kushindwa kuhimili jua, uwe mwangalifu na usome maelezo yote kuihusu vipodozi ," anaonya Webb.

Kugeuka

Unaweza kufikiria kwamba jua linalokupiga kwenye uso wako linatosha, lakini kupata jua la kutosha kutokana na mionzi ya jua, unapaswa pia kuhakikisha jua linapiga kwenye miguu na mikono yako.

"Kila kipande cha sehemu ya mwili ambayo haijakingwa na jua kitatengeneza vitamini D.Kwahiyo kadri unavyoanika ngozi yako zaidi juani, ndivyo vitamini D inavyoendela kuzunguka ndani ya mwili wako ," anafafanua Webb.

Na ni muhimu kwenda nje kuongeza vitamini D hata katika siku yenye wingu?

"(Mawingu ) hupunguza mwangaza wa jua, kwahiyo hutengenezi kiwango kikubwa cha vitamini D katika muda saw ana siku ya jua, lakini bado tunaweza kupata kiwango kidogo cha vitamini D. Iwapo mvua inanyesha, kuna uwezekano mkubwa wa kupata mwangaza kidogo wa jua. Lakini kama kuna mawingu, unaweza kwenda nje kuota jua."