'Ikiwa unakula hapa, ujue unakula na panya'

Ongeza tauni ya panya ni miongoni mwa changamoto zingine zinazokumba Jiji la New York

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ongeza tauni ya panya ni miongoni mwa changamoto zingine zinazokumba Jiji la New York

Diem Boyd alikuwa ameketi nje ya mgahawa mmoja katika mji wa Greenwich village huko New York mnamo Septemba, wakati familia ya panya ilipombusu miguu yake.

"Ndani ya sekunde chache kila mtu aliruka juu," anasema."Tulipoteza hamu yetu ya kula."

Kila mtu huko New York ana hadithi kama hiyo ya kusimulia, anaelezea.

"Tuna mlipuko wa panya." "Unawaona unapotoka usiku," anakiri Deborah Gonzalez, ambaye, kama Diem, anaishi Upande wa Chini Mashariki mwa Manhattan.

"Unapotembea kwenye jengo hili unaona wanakimbia huku na kule." Ni vigumu kupima idadi sahihi, lakini simu ya dharura ya malalamiko ya New York City imezidiwa na malalamiko kuhusu panya mwaka huu kwa 15% kabla ya janga hilo.

"Ni wazi kwamba New York daima imekuwa na panya," anasema Marcell Rocha, ambaye pia anaishi jirani, lakini sasa "wao ni wakubwa zaidi na wenye ujasiri, wanaruka mithili ya wanamichezo wa sarakasi.''

Diem Marcell na Deborah
Maelezo ya picha, Diem, Marcell na Deborah wanapinga madai kwamba mikahawa hiyo imechukuwa nafasi katika barabraza mitaa yao

Hivyo, nini kilichobadilika?

Diem, Deborah na Marcell walilalamikia wimbi hili jipya la corona, na kuhimiza watu wengi zaidi kula kwenye meza za nje.

Mamia ya barabara za New York sasa zimepangwa - mara nyingi pande zote mbili - na makazi ya dharura, na kubadilisha kabisa mandhari ya mijini.

Kuna maeneo mapya zaidi ya 11,000 ya nje ya kula. Baadhi ya kumbi hizi mpya ni kidogo zaidi ya fremu na viti vilivyotawanyika, vingine ni miundo thabiti yenye sakafu, taa, mitungi ya maua na vifaa vya umeme vya kupasha moto.

Mamia ya mitaa ya New York sasa imejaa malazi ya dharura
Maelezo ya picha, Mamia ya mitaa ya New York sasa imejaa malazi ya dharura

Diem, Deborah na Marcell wanasema katika makazi hayo marundo ya ya mifuko ya takataka ya plastiki kando ya barabara, na kufanya kuwa maficho mazuri ya panya chini ya ubao wa sakafu.

Hatahivyo, kumbi hizi zimeonekana kupendwa sana na wateja katika mwaka mmoja na nusu uliopita.

Inajulikana sana kwa kweli, kwa wakazi wa eneo hilo. "Hii ni kuzimu ya duniani kwa sababu ya umati na kelele," anasema Marcell.

Upande wa Mashariki ya Chini daima kumekuwa makazi ya kupendeza, lakini majira ya joto yaliyopita ilikuwa kama "kuishi kwenye tamasha" anaelezea.

Mwanzoni mwa janga hilo, meya wa New York Bill de Blasio alizindua mpango wa "migahawa ya wazi". Ilikuwa ni sehemu ya maono mapana ya jiji ambalo halijatawaliwa sana na msongamano na lililolenga zaidi wakaazi na wageni wake

Njia zilizosongamana
Maelezo ya picha, Wakazi wana wasiwasi kuwa hamu ya kula nje inachangia kuongezeka kwa uchafu

Anasema panya, umati wa watu, matapishi na uchafu, vinakasirisha, lakini pia ana wasiwasi kwa wakazi wazee wanaojaribu kuvuka barabara zenye shughuli nyingi.

Vyombo vya moto vinapaswa kupunguza kasi ya ili kupita mitaa yenye maduka ya migahawa, anasema.

Wengine wameibua wasiwasi kama huo,na mnamo Mei Idara ya Zimamoto ya Jiji la New York ilituma barua pepe kwamba vibanda viliwachelewesha kufika kwenye eneo la moto kwenye mgahawa wa Wachina katikati mwa Manhattan.

Wakazi kutoka Chinatown hadi Queens, Brooklyn hadi Greenwich Village, sasa wanataka kukaguliwa kwa athari za milo ya nje.

Wengine wanasema kimsingi inabadilisha tabia ya vitongoji ambavyo havikuwa vimetawaliwa na maisha ya usiku yenye kelele,katika maeneo mengine inazidisha matatizo yaliyopo.

Kadiri hali ya hewa inavyozidi kuwa baridi, vihenge vimefungwa kwa karatasi za plastiki, hivyo basi kushindwa lengo la awali la kiafya na usalama la kutoa nafasi ya kula chakula kwenye mazingira ya hewa ya kutosha.

Baadhi ya wakazi wanatoa wito wa kukaguliwa kwa athari za milo ya nje

Chanzo cha picha, Lief Arntzen

Maelezo ya picha, Baadhi ya wakazi wanatoa wito wa kukaguliwa kwa athari za milo ya nje

"Ni kama mji duni," anasema Diem. Lakini si kila mtu anaiona hivyo.

Andrew Rigie, mkurugenzi mtendaji wa Muungano wa Ukarimu wa Jiji la New York anasema mpango wa chakula cha nje kuwa wa kudumu kunaweza kuthibitisha kichocheo ambacho jiji linahitaji kushughulikia shida yake ya muda mrefu ya taka.

Takataka za New York mara nyingi huachwa kando ya barabara kwenye mifuko ya rangi nyeusi ya plastiki ili kukusanywa na wahudumu wa umma au wa binafsi.

Bw Rigie anakubali mfumo huo unahitaji kuboreshwa, lakini anasema hilo halipaswi kuzuia mlo wa nje. "Ukweli sasa ni kwamba umma sasa umepata ladha ya migahawa ya nje na wanaipenda.

Kuna mahitaji ya kuifanya iwe ya kudumu." Lakini mpango wa sasa wa muda - ulioanzishwa haufanywi kuwa wa kudumu.

Badala yake, kanuni zinaboreshwa ili kushughulikia masuala mengi ya wakazi, pamoja na mazoea ya usafi wa mazingira; kelele usiku; na ni shughuli gani zinaruhusiwa, anasema.

"Je, watu watakuwa na maoni tofauti kama wanataka aina tofauti za shughuli mitaani au la? Bila shaka.

Jiji la New York ni eneo kubwa tata lenye matumizi mengi yanayoshindana kwenye maeneo ya umma," anasema.

Jiji linasema kanuni kuu za mpango huo mpya zitakuwa ufikiwaji, muonekano - ikiwa ni pamoja na usafi, usawa - kuruhusu vitongoji vyote kushiriki, kuhakikisha migahawa kufanya kazi katika mazingira ya ujirani na usalama, ikijumuisha ufikiaji wa magari ya dharura.

Jacob Siwak owner of Forsythia restaurant
Maelezo ya picha, Jacob, head chef and owner of Forsythia, says the scheme offers huge advantages

Idara ya Uchukuzi, ambayo itasimamia mpango huo wa kudumu, na Idara ya Mipango zilizindua mashauriano ya kuwauliza wakazi wa New York jinsi wanavyofikiri malengo hayo yanaweza kufikiwa vyema zaidi.

"Mafanikio ya ajabu ya milo ya nje yanaonyesha jinsi tunaweza kufikiria upya mazingira yetu ya mtaani ili kuhudumia vitongoji vyetu vyema," anasema kamishna wa idara ya uchukuzi, Hank Gutman.

Bw Gutman anasema atashauriana na umma "kutayarisha miongozo" ambayo itaongeza ufikiwaji, usalama na kushughulikia masuala kama vile kelele, saa za kazi na usafi wa mazingira.

Lakini wakazi wengi wanasalia na mashaka makubwa. Wanasema mashauriano hayatafikia sehemu nyingi za jamii, haswa wale ambao hawatumii mitandao.

Hata kama masharti magumu yatakubaliwa na kutekelezwa wanashuku nguvu zinazohusika kwenye mpango huo.

Wamiliki wa mikahawa na baa wanasema vibanda vimewaruhusu kuwapa ajira watu wengi wakati wa janga hilo
Maelezo ya picha, Wamiliki wa mikahawa na baa wanasema vibanda vimewaruhusu kuwapa ajira watu wengi wakati wa janga hilo