Kuna maambukizi mapya milioni moja kila siku ya magonjwa ya zinaa, yasema WHO

Umati wa watu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu mmoja kati ya watu 25 ana ugonjwa wa zinaa,kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani

Maambukizi mapya milioni moja ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya zinaa ( STIs) hutokea kila siku , linakadiria Shirika la Afya Duniani (WHO)

Hiyo inamaanisha kuwa zaidi ya maambukizi mapya milioni 376 kutokea kila mwaka - yakiwemo magonjwa ya kisonono, kaswende chlamydia, na trichomoniasis,

WHO limesema kuwa ukosefu wa mafanikio ya kuzuwia kuenea kwa magonjwa ya zinaa ni moja ya sababu za kuenea kwa kasi na kuongeza kuwa kiwango hicho cha maambukizi kinamaanisha kuwa hatua za dharura za kukabiliana na maambukizi ".

Wataalamu zaidi wanahofu juu ya kuongezeka kwa visa magonjwa ya zinaa kuwa sugu kiasi cha kutotibiwa na dawa zilizopo kwa sasa.

Shirika la WHO mara kwa mara hutathmini athari za magonjwa manne ya zinaa ya maarufu miongoni mwa wakazi wa dunia.

Shirika hilo liliangalia utafiti uliochapishwa na kukusanya ripoti kutoka kwa wafanyakazi wake katika nchi duniani

Zikilinganishwa na tathmini ya mwaka 2012, ripoti za WHO " idadi haijapungua " katika viwango vya maambukizi mapya na yaliyopo ya magonjwa ya zinaa .

Shirika hilo la Afya Duniani linasema mtu mmoja kati ya watu 25 duniani ana walau aina moja ya maradhi ya zinaa, huku baadhi wakiwa na maambukizi ya magonjwa zaidi mmoja wa zinaa kwa wakati mmoja.

Idadi hiyo inasema kuwa mingoni mwa watu wenye umri kati ya miaka 15-49 mnamo mwaka 2016 walikuwa ni:

  • Milioni 156 walikuwa na trichomoniasis
  • Milioni 127 walikuwa na chlamydia
  • Wagonjwa milioni 87 walikuwa ni wagonjwa wapya wa Kisonono
  • na watu milioni 6.3 walikuwa ni wagonjwa wapya wa kaswende

Trichomoniasis husabishwa na maambukizi ya vimelea wakati wa ngono. Chlamydia, kaswende na kisonono ni maambukizi ya bakteria.

Man starting to take his tros off

Chanzo cha picha, iStock

Dalili za magonjwa ya zinaa

Dalili za magonjywa ya zinaa ni pamoja na kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida kwenye uke au uume ,maumivu wakati wa kwenda haja ndogo na kuvuja damu kabla ya muda wa hedhi.

Hata hivyo mara nyingi dalili huwa hazipo.

Madhara makubwa mtu anayoweza kuyapata ni pamoja na kupata maradhi ya majeraha ya kiunoni (pelvic inflammatory disease) na kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa wanawake ama kutungisha mimba na chlamydia na kisonono na kaswende huweza kusababisha maradhi ya moyo.

Kama mwanamke ataambukia ugonjwa wa zinaa iwapo ni mjamzito anaweza kujifungua mtoto mwenye ukosefu wa baadhi ya viungo vya mwili au kujifungua mtoto njiti , mwenye uzito wa chini wa mwili na huenda akawa na matatizo mengine ya kiafya kama kichomi, upofu na kuzaliwa na kasoro katika viungo vyake vya uzazi.

Daktari Peter Salama, wa shirika la Afya Duniani WHO, anasema: " Tunashuhudia ukosefu wa mafanikio ya kuzuwia usambazaji wa magonjwa ya zinaa kote duniani unaotisha.

Man blocking his genitals with his hands

Chanzo cha picha, iStock

" HiiHuu ni wito wa kufayika kwa juhudi za pamoja kuhakikisha kila mmoja, popote alipo anaweza kupata huduma anazohitaji kuzuwia na kutibu magonjwa haya ."

Kufanya ngono salama hususan kwa kutumia mipira ya kinga na upatikanaji mzuri wa vipimo vya maradhi vyote ni muhimu , limesema shirika la afya duniani WHO.

Kwa upande wa matibabu, magonjwa ya zinaa yatokanayo na na bakteria yanaweza kutibiwa kwa dawa zilizopo.

Lakini tiba ya kaswende imekuwa ni ngumu zaidi kwasababu ya ukosefu wa aina ya kipekee ya dawa ya penicillin inayohitajika na kumekuwa na ongezeko la kile kinachoitwa "kisonono sugu " ambayo ni