Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Newcastle yajiunga na mbio za kumsajili Delap

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle United ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 22 Liam Delap wiki hii. (Talk sport)
Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili Delap lakini kushindwa katika fainali ya Ligi ya Europa na kutoweza kumpatia soka la Ulaya msimu ujao kutaipa Chelsea faida. (ESPN)
Manchester City itamenyana na Liverpool kuwania saini ya Mchezaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 21 na beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez. (i paper- usajili unahitajika)
Brighton imekubali kumsajili beki wa Ufaransa Olivier Boscagli, 27, kwa uhamisho wa bure kutoka PSV Eindhoven. (Sky Sports)
Liverpool imepokea maombi kutoka kwa Ligi ya Sudia kumhusumshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota na winga wa Colombia Luis Diaz. (Sky )
Manchester United iko tayari kulipa ada ya kuachiliwa kwa mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha (25) kwa awamu. (Fabrizio Romano)
Manchester United pia inapania kumshawishi mshambuliaji wa klabu ya Sporting na timu ya taifa ya Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kujiunga nao msimu huu wa kiangazi. (L'Equipe - kwa kifaransa)
Aston Villa haina nia ya kumzuia kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 32, ikiwa anataka kuondoka Villa Park. (Givemesport)
Chelsea iko tayari kwa mazungumzo na klabu ya Ajax kuhusu uhamisho wa mlinzi wa Uholanzi Jorrel Hato, 19, ambaye pia ananyatiwa na Liverpool na Arsenal. (Caughtoffside)
Barcelona imefikia mkataba mpya na mshambuliaji wa Brazil Raphinha (28) ambao utamuwezesha kusalia katika klabu hiyo hadi mwezi Juni 2028. (Fabrizio Romano), external
Mkufunzi wa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo huenda akaondoka mwishoni mwa nsimu huu kufuatia mvutano wa ndani ya klabu hiyo. (Footmercato - kwa kifaransa)
Leicester City wanatarajiwa kumtimua kocha wao Ruud van Nistelrooy huku mpango wa kumsajili meneja wa zamani wa Southampton Russell Martin ukipiga hatua. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi