Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Cunha tayari kujiunga na Man Utd

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha anatarajiwa kujiunga na Manchester United baada ya msimu kukamilika wikendi hii huku klabu hiyo ya soka ya England iitarajiwa kuanzisha kipengele cha kutolewa kwa mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kwa pauni milioni 62.5. (Sky Sports)
Manchester United pia imefanya mazungumzo ya ana kwa ana na mshambuliaji wa Ipswich Town na England Liam Delap, 22. (The Athletic)
Beki wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 24, amekamilisha vipimo vyake vya afya katika klabu ya Liverpool siku ya Jumatatu. Tetesi zinasema mchezaji huyo wa Uholanzi alisafiri Uingereza siku ya Jumapili kufanikisha mchakato huo. (Sky Sports)
Aston Villa ina nia ya kumsajili mlinda lango wa Liverpool na Ireland Caoimhin Kelleher, 26, huku MArgentina Emiliano Martinez, 32, akitarajiwa kuondoka Villa msimu wa kiangazi. (Sun)
Manchester United, Barcelona na Saudi Pro League ni miongoni mwa klabu zinazofuatilia hali ya Martinez. (Sun)