Nchi kumi zenye nguvu zaidi kijeshi katika ulimwengu wa Kiislamu

Chanzo cha picha, AFP
'Ulimwengu wa Kiislamu' unaanzia Afrika Magharibi hadi Kusini Mashariki mwa Asia. Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ina nchi wanachama 57.
Pamoja na vita vinavyoendelea nchini Iraq, Libya, Syria na Yemen, vita vya Afghanistan, Rasi ya Sinai nchini Misri, na vurugu katika maeneo ya Palestina, vikosi vya kikanda vimelazimika kukabiliana haraka na vita vya kawaida na visivyo vya kawaida.
Nchi ambayo imetumia pesa nyingi zaidi kwa jeshi ni Saudi Arabia. Katika mwaka 2017, bajeti ya ulinzi ya Riyadh ilikuwa ya tatu kwa ukubwa duniani kulingana na Benki ya Dunia.
Hapa kuna nchi 10 zenye nguvu za kijeshi na baadhi ya zana zake za kijeshi.
10: Umoja wa Falme za Kiarabu

Chanzo cha picha, FRANK GARDNER
Idadi ya wanajeshi ni 64,000.
Bajeti ya kijeshi mwaka wa 2017: dola bilioni 14.37.
UAE inashika nafasi ya juu zaidi kati ya majirani zake katika Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC).
Baadhi ya wanajeshi wake wameshiriki katika vita nchini Afghanistan, Libya na Yemen.
Wanategemea sana wafanyikazi wahamiaji kutoka Amerika Kusini na Eritrea.
9: SYRIA

Chanzo cha picha, AFP
Idadi ya wanajeshi ni 154,000
Bajeti ya 2017: dola bilioni 1.87.
Baada ya miaka ya mapigano makali, jeshi la Syria ni kivuli cha vile ilivyokuwa zamani.
Jeshi lake linaimarishwa na wanamgambo wa Iran, vikosi vya Urusi na wanamgambo wa ndani ili kudumisha utawala wa Assad, baada ya kupata hasara kubwa, wengi wa wanajeshi wameondoka huku vita vikiendelea kupamba moto.
8: Malaysia

Idadi ya wanajeshi 110,000.
Bajeti ya 2017 ni dola bilioni 4.7.
Ingawa Malaysia haijawahi kupigana vita hapo awali, inajivunia jeshi la kisasa na safu ya kimkakati iliyosawazishwa.
Malaysia na Uchina zina mzozo juu ya Bahari ya Uchina Kusini.
Jeshi lao ni moja ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.
7: Algeria

Chanzo cha picha, AFP
Wanajeshi wake ni: 520,000
Bajeti ya 2017: dola bilioni 10.6
Algeria ndiyo nchi kubwa zaidi ya Kiarabu na imewekeza kwa kasi katika jeshi lake tangu uhuru.
Jeshi la Taifa la Algeria limehusika katika vita mbalimbali tangu kuanzishwa kwake, kwanza likishiriki katika vita vya umwagaji damu vya kupigania uhuru, vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe vilivyojulikana kwa jina la 'Black Ten', na kisha zaidi ya miongo miwili ya kupambana na ugaidi, na kulinda mipaka yao muhimu.
Pia ni nchi pekee zaidi ya Uchina kununua mfumo wa makombora wa S400 kutoka Urusi.
Algeria ina masuala magumu ya mipaka na nchi zikiwemo Libya na Mali, na inaunga mkono kikamilifu kundi la Polisario Front, ambalo linatafuta uhuru kutoka kwa Sahara Magharibi ya Morocco.
6: Saudi Arabia

Chanzo cha picha, AFP
Wanajeshi wake ni 231,000
Bajeti ya 2017: dola bilioni 69.413.
Jeshi la Saudi Arabia ndilo jeshi lenye silaha bora zaidi katika eneo hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni, wamepigana vita vya umwagaji damu nchini Yemen, wakiongozwa na muungano wa washirika wake.
5: Pakistan

Chanzo cha picha, ANATOL LIEVEN
Idadi ya wanajeshi 637,000.
Bajeti ya 2017 ni dola bilioni 7.
Jeshi la Pakistan lina nguvu na utamaduni wa kijeshi wa muda mrefu.
Katika miaka ya hivi karibuni, imefaidika kutokana na ushirikiano mkubwa na Saudi Arabia na Uchina ili kufanya vikosi vyake kuwa vya kisasa, kwa kutumia teknolojia nzito ya kijeshi na utengenezaji wa silaha.
Kiutendaji, Pakistan inajivunia mojawapo ya vikosi vikubwa zaidi vya kijeshi katika eneo hilo, ikiwa na safu dhabiti inayoungwa mkono na huduma ya kijasusi na juhudi zinazoendelea za kukuza uwezo wa tasnia ya ulinzi na kutengeneza silaha na risasi za kisasa.
Pia ni moja ya nchi katika eneo hilo ambayo ina nguvu za nyuklia.
4: Indonesia

Chanzo cha picha, EUROPEAN PHOTOPRESS AGENCY
Idadi ya wanajeshi 975,750.
Bajeti ya 2017 ni dola bilioni 6.9.
Huku Indonesia ikitarajiwa kuwa nchi ya nne kwa uchumi mkubwa duniani ifikapo 2050, jeshi lake linaendelea kukua.
Mbali na jeshi lake lenye nguvu, ni nyumbani kwa wanajeshi 281,000 zaidi.
Wana nguvu za kutosha za kijeshi, kiuchumi na kisiasa ili kuhakikisha utulivu wa ndani.
3: Iran

Chanzo cha picha, Getty Images
Idadi ya wanajeshi 534,000.
Bajeti ya 2017 ni dola bilioni 14.
Imeweza kusimamia kikamilifu wanamgambo wengi wanaopigana katika nchi tofauti.
Chini ya miaka ya vikwazo, Iran imeendeleza sekta muhimu ya ulinzi wa taifa na imepata maendeleo makubwa kuelekea kuwa nguvu ya nyuklia.
Vikosi vyake vya kijeshi pia vinazingatiwa kuwa na nguvu katika vita visivyo vya kawaida.
Iran imetoa msaada wa kiufundi na kijeshi kwa utawala wa Assad nchini Syria na Wahouthi nchini Yemen.
2: Misri

Chanzo cha picha, AFP
Idadi ya wanajeshi 438,500.
Bajeti ya 2017: ni idola bilioni 2.7.
Baada ya Rais Abdel Fatah el Sisi kuchukua mamlaka, jeshi la Misri limepewa uhuru zaidi wa kupanua na kushiriki katika karibu kila nyanja ya jamii ya Misri, ikiwa ni pamoja na bajeti ya ulinzi, mikataba ya kibinafsi ya kina, na yenye kuangazia kodi.
Jeshi la Misri limepiga hatua kubwa katika kulifanya jeshi lake kuwa la kisasa tangu Sisi aingie madarakani, hatua kwa hatua likinunua silaha mpya na za kisasa.
Pia limefanya mabadiliko hasa katika jeshi lao la majini. Misri imekuwa ikihangaika kukabiliana na waasi katika Rasi ya Sinai kwa miaka kadhaa.
1: Uturuki

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanajeshi kwa sasa: 355,800
Bajeti ya 2017: dola bilioni 10.2.
Vikosi vya kijeshi vya Uturuki vimehusika katika vita kadhaa kwa miaka.
Mbali na uwepo wake mkubwa nchini Syria, Uturuki imeendeleza sekta yake ya ulinzi, kuzalisha ndege zisizo na rubani, makombora ya hali ya juu, vifaru vya kivita vya asili, na helikopta za kivita zilizofanyiwa majaribio.
Ingawa inaorodheshwa kama jeshi la 1 lenye nguvu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na Mashariki ya Kati, pia inashikilia nafasi ya 9 ulimwenguni kulingana na Kiashiria cha Global Firepower, mbele ya Ujerumani.
Uturuki pia imeanzisha kambi zake za kijeshi huko Qatar na Somalia, na kupanua ushawishi wake wa kijiografia.