Tazama: Waandamanaji wa Bangladesh wavamia makazi rasmi ya Waziri Mkuu

Maelezo ya video, Tazama: Waandamanaji wa Bangladesh wavamia ikulu ya waziri mkuu
Tazama: Waandamanaji wa Bangladesh wavamia makazi rasmi ya Waziri Mkuu

Waandamanaji nchini Bangladesh wamevamia makazi rasmi ya waziri mkuu, huku wimbi la maandamano dhidi ya serikali likiendelea. Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amejiuzulu na kukimbia nchi, BBC inafahamu.

Kujiuzulu huko kumekuja wakati maelfu ya waandamanaji wameingia barabarani katika mji mkuu Dhaka, siku moja baada ya makabiliano kati ya polisi na waandamanaji na kusababisha vifo vya takriban watu 90.

Shirika la habari la Reuters lilishiriki video hiyo iliyokuwa ikionyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Bangladeshi-Bengali Channel 24.