Tufahamishe iwapo unakubali kupokea cookies
Tunatumia kuki kukufanya ufurahie mtandao. Tafadhali tufahamishe iwapo unakubali kupokea cookies au vidakuzi vyote hivi
Kutana na wanasoka bibi vikongwe wanavyotishia soka la Afrika
Kutana na wanasoka bibi vikongwe wanavyotishia soka la Afrika
Huenda wasiwe na ujuzi wa Lionel Messi au Cristiano Ronaldo, lakini hilo haliwazuii bibi vikongwe hawa ama maajuza wa Kiafrika kufanya mazoezi ya kufunga bao na kukaba kwa ustadi.
Rebecca Ntsanwisi mwenye umri wa miaka 57 kutoka Afrika Kusini ameanzisha timu za Soka kwa ajili ya bibi wazee ama Maajuza (Football Grannies) katika bara zima la Afrika katika jitihada za kuboresha afya ya akili na kimwili za wanawake wazee.
Timu tano kutoka Afrika kwa sasa zinashiriki katika mashindano ya Kombe la Dunia la Football Grannies huko Limpopo, zambia ambapo mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi ana zaidi ya miaka 80.