Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Bruno Fernandez na Alejandro Gernacho katika hatari ya kuuzwa Man United

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Alejandro Gernancho na Bruno Fernandes

Mkufunzi wa United Ruben Amorim anasema ni wachezaji tisa katika kikosi chake ambao "hawawezi kuuzwa", huku kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 30, na winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, wakiwa miongoni mwa majina yaliyo katika hatari ya kuuzwa. (Mail)

Klabu kadhaa kubwa za Ulaya zimeonyesha nia ya kumnunua beki wa pembeni wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 24 Alphonso Davies, ikiwemo Liverpool, Real Madrid na Barcelona. (Athletic - Subscription Required),

Manchester City wamekubali kuwa wanahitaji kununua wachezaji katika dirisha la usajili la Januari kufuatia mwenendo wao mbaya, huku kukiwa na uwezekano wa kusajili kati ya wanne hadi sita katika madirisha mawili yajayo. (Telegraph - Subscription Required),

City wanamtaka kiungo wa kati wa Valencia Muhispania Pepelu, 26, kutoa ulinzi kwa Rodri aliyejeruhiwa. (Estadio Deportivo),

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Thomas Partey

Arsenal wako hatarini kumpoteza kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 31, bila malipo msimu wa joto. {Mirror),

Mshambulizi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 21 raia wa Uingereza Carney Chukwuemeka anavutia vilabu vya Ligi ya Premia. (Football Insider),

Mshambulizi wa Brazil Richarlison, 27, atakataa kutumwa kwa klabu ya zamani ya Fluminense anapojaribu kujithibitisha Tottenham. (TNT Sports Brazil - In Portuguese), nje

Manchester United wanamtaka mlinzi wa Girona Muhispania Miguel Gutierrez, 23, mwezi Januari huku wakionekana kuimarisha chaguo lao la beki wa kushoto. (TeamTalk).

Newcastle wanamfuatilia winga wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Maghnes Akliouche.

Tottenham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ufaransa Andy Diouf, 21, baada ya kumtazama akiwa Lens. (GiveMeSport).

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ashley Phillips

Spurs wanafikiria kumwita mlinzi wa Uingereza Ashley Phillips, 19, kutoka kwa mkataba wake wa mkopo huko Stoke mwezi Januari ili kusaidia kupunguza tatizo lao la majeraha. (Standard)

Wolves watalazimika kumuuza mmoja wa wachezaji wao nyota mwezi Januari ili kuepuka kuvunja sheria za Fifa (Football Insider)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Manchester United Dan Ashworth anaweza kuchukua nafasi ya Edu katika klabu ya Arsenal, hata hivyo Roberto Olabe wa Real Sociedad pia anazingatiwa. (Mail- Subscription Required)

Crystal Palace wanataka wachezaji watatu kutoka Lyon, huku winga wa Ghana Ernest Nuamah, 21, winga wa Ufaransa Rayan Cherki, 21, na mlinzi wa Ufaransa Sael Kumbedi, 19, wakiangaziwa. (TBR Football),

Mlinzi wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 30, anavutia vilabu kadhaa vya Serie A, ikiwemo AC Milan. (TeamTalk)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla