Mauaji ya 'kukufuru' nchini Nigeria
Deborah Samuel alikuwa mwanafunzi Mkristo aliyekuwa na umri wa miaka 21 katika chuo kaskazini mwa Nigeria. Kundi la wanafunzi wenzake walimpiga hadi kufa baada ya kusmhutumu kwa kukufuru kupitia ujumbe wa sauti alioutuma katika kikundi cha WhatsApp.
Mama yake na baba yake waliiambia BBC maisha yao yamebadilika haraka tangu auawe. Sheria za kukufuru hazina msingi wa dini yoyote ile, majimbo 12 katika eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi yana mahakama za Kiislamu ambazo zinaiona kufuru kama kosa linaloadhibiwa kwa kifo.Lakini hukumu za kifo kwa kukufuru hazijawahi kufanyika. Badala yake, madai ya kukufuru mara nyingi hupelekea kuuawa na kundi la watu.