Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Sesko au Gyokeres kutua Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanasaka mshambuliaji na wameelekeza macho yao kwa Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Slovenia mwenye umri wa miaka 21, au Viktor Gyokeres wa Sporting na Sweden mwenye umri wa miaka 26. (Independent)
Newcastle wanamfuatilia winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 20, Jamie Gittens, na pia wanaweza kumsajili kipa mwenzake wa Uswisi, Gregor Kobel mwenye umri wa miaka 27. (Mail)
Liverpool wanaamini Florian Wirtz atasalia Bayer Leverkusen au kujiunga na Bayern Munich, lakini watajaribu kumsajili iwapo kiungo huyo mshambuliaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 ataamua kuondoka Bundesliga. (Times)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji mkongwe wa England Jamie Vardy ataondoka Leicester City msimu huu wa joto lakini hana mpango wa kustaafu na anaamini bado anaweza kucheza Ligi Kuu. (Sky Sports)
Mazungumzo mapya kati ya Bayern Munich na beki wa Ufaransa Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 26, yameanza kuhusu mkataba mpya hadi 2030. (Sky )
Lazio itailipa Arsenal ada ya euro milioni 9 (£7.57m) kumsaini beki wa kushoto wa Ureno, Nuno Tavares mwenye umri wa miaka 25. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester United na Denmark, Rasmus Hojlund, mwenye umri wa miaka 22, anakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wake Old Trafford, kwani kocha Ruben Amorim atalazimika kuuza baadhi ya wachezaji kabla ya kufanya usajili mpya majira ya joto. (Telegraph)
Bournemouth wameweka bei ya pauni milioni 45 kwa beki wao wa kushoto kutoka Hungary, Milos Kerkez mwenye umri wa miaka 21, ambaye anawaniwa na Liverpool. (iSport)
Kiungo wa kati wa Fulham, Tom Cairney, mwenye umri wa miaka 34, anawindwa na Wrexham walioelekea Championship, na huenda akapewa mkataba wa pauni 50,000 kwa wiki baada ya kuondoka Fulham kwa uhamisho wa bure. (Talksport)