Je, kusahau kumbukumbu za nyuma kuna faida?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
- Author, David Robson
- Nafasi, BBC
Kumbukumbu isiyo kamili na kumbukumbu za uwongo ni vipengele muhimu vya akili, mwanasayansi wa mishipa ya fahamu Charan Ranganath anabishana katika kitabu kipya cha “Why We .”
Profesa wa saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha California, Ranganath ametumia miaka 30 kusoma mfumo wa ubongo kuhusu uwezo wetu wa kukumbuka na kusahau.
Anasema uelewa wetu mwingi kuhusu kumbukumbu sio sahihi. Amezungumza na mwandishi wa habari za sayansi David Robson.
Kusahau kuna faida?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Wacha tuanze na wazo la kujifunza kupitia makosa. Kwa nini tunajifunza vizuri zaidi tunaporuhusu makosa?
Kanuni ya kujifunza kupitia makosa, unapojaribu kurejesha kumbukumbu nyuma, kukumbuka kwako daima hakutakuwa kukamilifu. Wakati ubongo unapojaribu kuvuta kumbukumbu, kumbukumbu imara huimarika zaidi na zile dhaifu huzidi kudhoofika.
Maana yake, kujipa changamoto ya kuvuta kumbukumbu ndiyo njia bora ya kujifunza zaidi, kwa sababu inafichua udhaifu, na inaupa ubongo wako nafasi ya kuboresha kumbukumbu.
Mbinu nzuri ya kujifunza - kama kuendesha gari katika eneo unalolijua badala ya kuendesha kwa kutumia ramani za Google, au kuigiza mchezo hata kama utafanya makosa ni bora zaidi kuliko kusoma skripti ya mchezo mara nyingi.
Wengi wetu huhisi kuchanganyikiwa wanaposhindwa kukumbuka, lakini unapendekeza kusahau mara nyingi kuna manufaa. Ni manufaa gani?
Mfano ninaopenda kuutoa; fikiria nilikuja nyumbani kwako, na kukuuliza; kwa nini wewe huweki kila kitu nyumbani kwako? Kwa nini usihifadhi kila kitu? Ikiwa hatuwezi kusahau, manake tungekuwa tunahifadhi kumbukumbu ya kila kitu, na hilo litakufanya ushindwe kupata unachotaka, wakati unapokitaka.
Hivi sasa ninaishi hotelini, haitakuwa na maana kwangu kukumbuka namba ya chumba hiki wiki mbili baadaye. Vivyo hivyo, fikiria watu wote unaopishana nao barabarani. Je, kweli unahitaji kukariri nyuso zao wote?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Kwanini tunakuwa wasahaulifu?
Kwa nini tunakuwa wasahaulifu zaidi kadiri umri unavyoongezeka?
Umri unavyoongezeka, si kwamba hatuwezi kuunda kumbukumbu, lakini huwa hatuzingatii taarifa ambazo tunahitaji kukumbuka.
Tunakuwa na mambo mengi, na mambo haya yote huja na gharama ya kuvuruga yale muhimu tunayojali. Na kwa hivyo, tunapojaribu kukumbuka, hatuwezi kupata kumbukumbu tunayoitafuta.
Je, ni mikakati gani tunaweza kuitumia ili kuepuka kusahau na kuboresha kumbukumbu zetu?
Kuna kanuni tatu za msingi. Kumbukumbu zetu huwa hushindana, na kwa hivyo kadri unavyoweza kukifanya kitu kionekane, ndivyo rahisi zaidi kukikumbuka.
Kumbukumbu za wazi ambazo zinahusishwa na vitu vya kipekee, kama sauti na hisia - ndizo ambazo zitadumu. Kwa hivyo shikamana na mambo yanayokupa hisia, hutusaidia kukumbuka vyema zaidi.
Mkakati wa pili ni kuweka mpangilio wa kumbukumbu zako ili ziwe na maana zaidi. Katika kitabu ninajadili njia ya "jumba la kumbukumbu," kuunganisha taarifa unayotaka kujifunza na taarifa ambayo tayari unayo.
Tatu, tunaweza kuunda viashiria. Kwa mfano, nyimbo zinaweza kuamsha kumbukumbu za wakati fulani maishani mwako.
Unatunzaje kumbukumbu?
Kando na kupoteza kumbukumbu, tunaweza kukuta kumbukumbu zetu zinajumuisha maelezo ya uwongo ambayo hayaambatani na matukio halisi. Kwa nini hili linatokea?
Kumbukumbu hubadilika kutokana na wakati. Ikiwa umemwona mtu ambaye haujaona kwa muda mrefu, na uso wake umebadilika ikilinganishwa na mara ya kwanza ulipowaona.
Unahitaji kuunda kumbukumbu sahihi zaidi kuhusu mwonekano wake. Lakini wakati mwingine kumbukumbu, zinatubakisha kwenye sura ile ile ya zamani.
Ni kwa njia gani kumbukumbu hushirikiana?
Tunapoeleza kumbukumbu zetu na watu wengine, inaweza kusababisha kumbukumbu kusahihishwa. Ninapokuelezea tukio fulani, kitendo cha kuunda hadithi hiyo ili kukusimulia kinaweza kubadilisha jinsi ninavyokumbuka.
Muitiko wako jinsi ninavyosimulia, utaunda kumbukumbu pia. Mfano, utanipa hata maelezo ya ziada - lakini yenye makosa - ambayo yanaweza kuingia kwenye kumbukumbu yangu.
Ninachanganyikiwa kati ya kile kilichotokea na kile ulichoniambia nilipokuwa nikielezea kilichotokea. Nitasema nyingi ya kumbukumbu zetu si [tu] ni zetu - ni kumbukumbu za pamoja.
Utatunzaje kumbukumbu zako mwenyewe?
Kuandika kitabu, kumenipa motisha ya kuhifadhi kumbukumbu zangu. Nafanya mazoezi, na ninazingatia sana lishe yangu, ili kuhakikisha ninadumisha afya yangu ya akili katika uzee.