Zuio la kuvua dagaa Ziwa Victoria linavyowaathiri wafanyabiashara Tanzania

Maelezo ya video, Zuio la kuvua dagaa Ziwa Victoria Tanzania
Zuio la kuvua dagaa Ziwa Victoria linavyowaathiri wafanyabiashara Tanzania

Zuio la kuvua dagaa kwa siku nane kila baada ya wiki tatu katika Ziwa Victoria Nchini Tanzania limesababisha uhaba mkubwa wa dagaa katika maeneo mbalimbali.

Zoezi hili hufanyika na mamlaka ya ziwa hilo, ili kuruhusu dagaa kuzaliana kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uvuvi haramu.

Lakini baadhi wanahoji kwanini zoezi hilo linahusisha dagaa peke yake na kuacha aina nyingine ya Samaki ziwani humo?

Mwandishi wa BBC David Nkya ametembelea Ziwa Victoria Mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na kuandaa taarifa ifuatayo.