Afghanistan: Ndani ya fikra za Kiongozi Mkuu wa Taliban Hebatullah Akhundzada
Ali Hussaini
BBC World Service

Chanzo cha picha, bbc
Ni mwaka wa pili tangu Taliban kuchukua utawala wa taifa la Afghanistan.
Lakini miaka miwili baadaye, serikali ya Taliban imeendelea kuweka orodha ya sheria kali, zote zikizingatia tafsiri yao ngumu ya Sheria ya Kiislamu.
Nyuma ya amri kama hizo, ambazo zinasimamia maisha ya takriban watu wanaokadiriwa kuwa milioni 40 nchini, kuna mtu mmoja tu - kamanda mkuu Hebatullah Akhundzada.
Akiaminika kuwa katika miaka yake ya 70, yeye ni mtu wa siri sio tu kwa ulimwengu, bali pia kwa raia wa Afghan. Ukitafuta picha yake katika mtandao , utapata picha mbili tu. Picha maarufu zaidi ikiwa ile ya pasipoti ya miaka ya 1990.
Tangu kuondolewa kabisa kwa vikosi vya kimataifa miaka miwili iliyopita, amekuwa vigumu sana kuonekana hadharani. Hajawahi kuhojiwa na mwandishi wa habari.
Wala hajawahi kujibu maswali yaliyoulizwa kuhusu uamuzi wake wa kuwapiga marufuku wasichana shuleni na wanawake kutoka kazini na katika nyanja za umma.
Ili kumuelewa vyema kamanda huyu mkuu aliyechagua kujificha asionekane na watu, tulichambua hotuba zake zote tulizoweza kuzipata.
Amri 65, zote kutoka wakati wa alipoteuliwa kuwa kiongozi wa vuguvugu la Taliban mwaka wa 2016. Pamoja na jumbe zake zote tano za Eid tangu 2018, ambapo tatu kati yake zilikuja baada ya unyakuzi wa pili wa Taliban mwezi Agosti, 2021.
Pamoja na hotuba zake zote ambazo zimenakiliwa na kuchapishwa na serikali yake tangu achukue wadhifa wa kamanda wao mkuu.
Nakala zote zilichanganuliwa kwa kutumia zana ya Kuchakata Lugha Asilia, ambayo ilihesabu mara kwa mara jinsi ambavyo alitumia kila neno.

Uislamu wa Hebatullah
Kukiwa na idadi kubwa ya watu zaidi ya 170, neno lililotumiwa sana na kiongozi wa Taliban hadharani lilikuwa 'Uislamu'.
Likiwa ndilo kama neno kubwa zaidi kwenye kati ya maneno aliyotoa, anahubiri mara kwa mara kwamba Afghanistan inapaswa kutawaliwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu pekee.
Kwa Hebatullah Akhundzada hakuna utengano wa mungu na serikali. Uislamu wake ni Imarati ya Kiislamu inayotawaliwa na sheria za Kiislamu.
Anawaambia Waafghan kuunda maisha yao karibu na kuzingatia kanuni za kimsingi za Kiislamu.
Wakosoaji wake wanasema tafsiri hiyo kali ya Uislamu iko mbali sana na mataifa mengine 50 ya Waislamu walio wengi duniani.
Hata Umoja wa Mataifa sasa unazungumzia "ubaguzi wa kijinsia" huku serikali ya Taliban ikiendelea kukaza kamba yake juu yake juu ya uhuru wa wanawake, kuwapiga marufuku kutoka kwenye mbuga za umma, kumbi za mazoezi ya wanawake na kumbi za urembo.
Kutazama mataifa ya magharibi

Chanzo cha picha, bbc
Ni mara moja tu ambapo anatumia neno 'uchaguzi', na sio kwa njia nzuri. Wakati wa mkusanyiko mkubwa wa wasomi wa Kiislamu mjini Kabul mnamo Juni 2022, alitangaza: 'Mimi si rais, wala si mteule, wala si mwanasiasa mpotovu'. Mtazamo wa Hebatullah Akhundzada juu ya aina yoyote ya mtindo wa demokrasia ya kimagharibi unaendelea kuwa wa kudharauliwa.
Kabla ya kuanguka kwa Kabul miaka miwili iliyopita, alitumia neno 'Amerika' katika hotuba zake zaidi ya mara 55, karibu kila mara kwa sauti ya uadui
Hata hivyo, tangu kuingia madarakani, sio tu kwamba neno 'Amerika' halipatikani kwa urahisi. linapotumiwa, ni ndani ya muktadha wa azma yake ya kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Marekani, kama mtawala rasmi wa Afghanistan.
'Wanawake' - katika mtu wa tatu
Neno 'Wanawake' limerejelewa tu na kiongozi huyo mkuu mara 13 tangu aingie madarakani mwaka wa 2018.
Hasa, katika miaka miwili iliyopita, amewahi tu kurejelea 'Wanawake' katika nafsi ya tatu. Wanawake ndio mada, sio walengwa.
Licha ya maagizo yake ya kubomoa kwa utaratibu uwezo wa wanawake na wasichana kusoma na kufanya kazi, Hebatullah Akhundzada amejadili mara chache mahitaji ya wale wanaounda zaidi ya nusu ya wakazi wa Afghanistan hadharani
Vita takatifu
Kwa pamoja maneno 'Jihad' na 'Mujahedeen' yalijumlisha maneno 160.
Kwa Waislamu wengi, neno 'Jihad' linamaanisha tu kupigana dhidi ya dhambi na kuwa wema.
Lakini katika muktadha wa neno la kiongozi huyo mkuu, linatumika kurejelea mapambano dhidi ya maadui wa Uislamu na kuendeleza vita vitakatifu.
'Mujahedeen' inahusu wale walio katika safari ya Jihad.
Wito wa jihad wa kiongozi huyo unaonekana kuzua utata katikati ya kizazi cha wapiganaji wa Taliban, ambao licha ya kulelewa wakati wa vita, sasa wanajikuta wakiishi katika nchi yenye amani.
Vijana kadhaa wanajulikana hivi karibuni kuvuka kinyume cha sheria kutoka Afghanistan na kuingia Pakistan kujiunga na kundi la wanamgambo linalojulikana kama Tehrik-i-Taliban Pakistan, au TTP, linalotaka kuweka utawala mkali wa Kiislamu.
Uongozi wa Taliban umelaani hadharani kufurika kwa wapiganaji, lakini vijana wengi wanasema wamedhamiria kuendelea kupigana jihadi.