Kwa nini kuna watu wengi wanaojiua nchini Korea Kusini?

Chanzo cha picha, JANG JUN-HA
"Nilipopata mwili wa mdogo wangu ukiwa baridi kama jiwe la kaburi miaka mitatu iliyopita, moyo wangu nilihisi kama moyo wangu umeganda."
Jang Joon-Ha analia, akisema ni kama roho yangu imepotea kumbuteza nduhu yake aliyekuwa na umri wa miaka 35 pekee.
Chan aliwasiliana na polisi baada ya mdogo wake kutopokea simu kwa siku kadhaa. Walipovunja mlango wa nyumba yake, Chan alikuta mwili wa kaka yake ukiwa umelala kitandani.
"Nilikuwa naenda kuchukua kozi katika kituo cha kuzuia kujiua na kuwa mwalimu."
"Nimekuwa nikienda shuleni na kuwaambiawatu kuhusu dalili za watu wanaofikiria kujiua ni zipi na jinsi ya kuwasaidia. Nimesaidia watu wengine kutoka kwenye tisho la kifo cha kujiua , lakini sikuwahi kufikiria kama hii ingeweza kutokea kwangu na kifo cha aina hii kumfika kaka yangu."
Kwa Chan mwenye umri wa miaka 45, si rahisi kuzungumzia kifo cha marehemu wa familia yake katika utamaduni wa Korea, kwani ni suala nyeti sana katika jamii ya Korea Kusini. Hata hivyo, anasaidia kuinua kiwango cha habari kuhusu tatizo hili katika jamii kwa kuzungumza kwa uwazi kuhusu yale aliyoyaona na kujifunza.
Kiwango cha juu cha vifo vya kujiua
Korea Kusini ni maarufu duniani kwa K-Pop na makampuni ya kimataifa kama Samsung. Lakini nyuma ya ustawi huo wa kiteknolojia, watu 36 hufa kila siku. Nchi hii inaongoza duniani kwa viwango vya juu vya visa vya vifo vya kujiua.

Shirika la takwimu la Korea Kusini linaripoti kuwa watu 13,352 walijiua mnamo 2021.
Kujiua ni sababu kuu ya vifo kati ya Wakorea wenye umri wa miaka 10 hadi 39. Kiashiria hiki ni cha juu sana kati ya vijana (43.7%), na wenye umri wa miaka ishirini (56.8%).
Seoul ina vifo 23.6 kwa kila watu 100,000, idadi ambayo ni ya juu kuliko wastani wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (11.1).
Hivi karibuni serikali ilitangaza mpango wa miaka mitano wa kuzuia tatizo hilo. Lengo ni kupunguza viashiria vya matatizo yanayopelekea kujiua kwa watu kwa asilimia 30.
Jamii ya shinikizo la juu
Kiwango cha juu cha visa vya kujiua nchini Korea Kusini hutokana na sababu mchanganyiko za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.
Nchi hii ilikuwa na uchumi mkubwa duniani baada ya kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953. Hata hivyo, maendeleo ya haraka ya kiuchumi hayajasababisha kupanuka kwa huduma za umma, na badala yake umeongezeka ukosefu wa usawa.

Chanzo cha picha, NEWS1
Mbali na kiwango kikubwa cha watu wanaojiua nchini Korea Kusini, pia kuna tatizo la mfumo duni wa ustawi wa jamii," anasema Sung-nan Jang, mkuu wa Chuo Kikuu cha Chung-Ang.
"Vifungo vya jadi kati ya wanafamilia na majirani vinavunjika polepole, na kila mtu anaachwa peke yake anapokabiliwa na matatizo katika maisha haya."
"Tuongee"
Utamaduni wa jamii unabadilika polepole, lakini juhudi zaidi zinapaswa kufanyika.
"Wakorea Kusini wamezoea kuishi kwa ushindani katika jamii hii yenye ushindani mkubwa, lakini Korea sio nchi ambayo watu wanaweza kukaa na kuzungumza waziwazi juu ya shida zao," Yeon Soo Kim, mkurugenzi wa LifeLine Seoseoul, shirika la hisani linalowahimiza kuacha kujiua.

Chanzo cha picha, ANG JUN-HA
Chan sasa anafanya kazi kama mwanasaikolojia katika kituo cha afya ya akili mjini Seoul, ambapo yeye huzisaidia familia ambazo zina watu waliojiua au zinazokabiliana na hisia za kujiua.
Pia anaongoza kikundi cha usaidizi kwa familia zilizofiwa na wapendwa wao waliojiua. "Hii ni kazi ngumu. Mara nyingi jamaa huwa wa kwanza kupata mtu aliyejiua. Inakua alama isiyofutika katika nyoyo zao, na watakumbuka na kusimulia hadithi kwa undani."
Chan anaelewa jinsi ilivyo vigumu kwao kuzungumza kuhusu mada kama hizo.
"Lakini kazi hii ni muhimu, itakuwa rahisi baada ya kusema, kuzungumzia kifo cha wapendwa wao waliojiua," anasema.
Kabla ya kujitoa uhai, mdogo wa Chan aliandika barua akiwaomba msamaha wazazi wake kwa kumtelekeza.
Alipozuru kaburi lake mwaka jana, Chan alimwambia kaka yake kwamba "kila kitu kiko sawa". “Usijali. Kila kitu kiko sawa kwetu, tunatunzana,” alisema Chan. (KS)