Kaka wa nyota maarufu Nicki Minaj afungwa miaka 25 jela
Kaka wa nyota maarufu Nicki Minaj, Jelani Maraj amepewa kifungo cha miaka 25 hadi maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji. Muathiriwa wa Maraj alisema alibakwa mara kwa mara na Maraj wakati mama yake alipokuwa kazini. Msichana huyo alisema kuwa jambo hilo lilitokea hadi mara nne kwa wiki na wakati mwingine mara mbili kwa siku .