Afcon 2023: Jinsi ‘wanyonge’ walivyokaidi makali ya vigogo huko Ivory Coast

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Emmanuel Akindubuwa na Isaiah Akinremi
- Nafasi, BBC Sport Africa, Lagos
Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, inayofanyika nchini Ivory Coast, imeibuka na matokeo yasiyotarajiwa na kushtukiza, na kurekebisha historia ya michuano hiyo.
Vigogo wa soka barani kote wamejikuta wakipata kushindwa kwa kushtukiza, huku wapinzani wasiotarajiwa wakichukua nafasi hiyo katika tamasha kubwa sana.
Mojawapo ya matukio ya kustaajabisha sana ilitokea wakati wenyeji, mbele ya mshambuliaji mashuhuri wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, walipopata kichapo cha 4-0 kutoka kwa Equatorial Guinea katika mchezo mzuri kwenye Uwanja wa Stade Olympique Alassane Ouatara mjini Abidjan.
Visa kama hivyo vya matokeo yasiyotarajiwa vilijitokeza kwa nguli mwingine wa soka barani Afrika, Samuel Eto'o , ambaye timu yake ya Cameroon ilikabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa mabingwa watetezi, Senegal, kabla ya kushindwa kwa mabao 3-1. Mfungaji wa bao la rekodi ya Afcon, ambaye ni Rais wa shirikisho la Soka la Cameroon, FECAFOOT, alitazama timu yake ikipambana na nguvu ya kikosi cha Senegal katika onyesho kuu kwa mabingwa hao.
Vinara wa kitamaduni wa soka kama vile Misri, wanaojivunia kuwa na rekodi ya kutwaa mataji saba ya Afcon, Ghana, Tunisia na Algeria tayari wamekumbwa na misukosuko kwenye michuano hii huku wanyonge wakionyesha umahiri wao na kuvuruga timu zenye nguvu katika soka la Afrika.
Kutotabirika kwa mechi hizo kunaweza kuonekana huku timu kama Equatorial Guinea, Cape Verde na Angola zikiibuka kileleni mwa makundi yao bila kutarajiwa, na kukaidi matokeo na kuwaacha mashabiki na wadadisi wakishangaa.
Hatua ya makundi ya Afcon 2023, iliyo na mshangao na misukosuko, imeweka mazingira mazuri ya awamu ya muondoano ya kusisimua, ambayo inaahidi nyakati zisizotabirika na vita vikali katika kutafuta bingwa wa bara hilo.
Kombe la Mataifa ya Afrika 2023
- P - Imecheza
- W - Imeshinda
- L - Imeshindwa
- D - Imetoka Sare
- GD - Tofauti ya bao
- Pts - Alama
-
-
Kundi A
Nchi P W L D GD Pts Equatorial Guinea 3 2 0 1 6 7 Nigeria 3 2 0 1 2 7 Ivory Coast 3 1 2 0 -3 3 Guinea Bissau 3 0 3 0 -5 0 -
13/01/2024, 20:00Ivory Coast 2-0 Guinea Bissau-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
14/01/2024, 14:00Nigeria 1-1 Equatorial Guinea-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
18/01/2024, 14:00Equatorial Guinea 4-2 Guinea Bissau-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
18/01/2024, 17:00Ivory Coast 0-1 Nigeria-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
22/01/2024, 17:00Equatorial Guinea 4-0 Ivory Coast-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
22/01/2024, 17:00Guinea Bissau 0-1 Nigeria-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
-
Kundi B
Nchi P W L D GD Pts Cape Verde 3 2 0 1 4 7 Misri 3 0 0 3 0 3 Ghana 3 0 1 2 -1 2 Msumbiji 3 0 1 2 -3 2 -
14/01/2024, 17:00Misri 2-2 Msumbiji-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
14/01/2024, 20:00Ghana 1-2 Cape Verde-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
18/01/2024, 20:00Misri 2-2 Ghana-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
19/01/2024, 14:00Cape Verde 3-0 Msumbiji-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
22/01/2024, 20:00Cape Verde 2-2 Misri-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
22/01/2024, 20:00Msumbiji 2-2 Ghana-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
-
-
-
Kundi C
Nchi P W L D GD Pts Senegal 3 3 0 0 7 9 Cameroon 3 1 1 1 -1 4 Guinea 3 1 1 1 -1 4 Gambia 3 0 3 0 -5 0 -
15/01/2024, 14:00Senegal 3-0 Gambia-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
15/01/2024, 17:00Cameroon 1-1 Guinea-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
19/01/2024, 17:00Senegal 3-1 Cameroon-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
19/01/2024, 20:00Guinea 1-0 Gambia-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
23/01/2024, 17:00Gambia 2-3 Cameroon-(Uwanja wa Bouaké)
-
23/01/2024, 17:00Guinea 0-2 Senegal-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
-
Kundi D
Nchi P W L D GD Pts Angola 3 2 0 1 3 7 Burkina Faso 3 1 1 1 -1 4 Mauritania 3 1 2 0 -1 3 Algeria 3 0 1 2 -1 2 -
15/01/2024, 20:00Algeria 1-1 Angola-(Uwanja wa Bouaké)
-
16/01/2024, 14:00Burkina Faso 1-0 Mauritania-(Uwanja wa Bouaké)
-
20/01/2024, 14:00Algeria 2-2 Burkina Faso-(Uwanja wa Bouaké)
-
20/01/2024, 17:00Mauritania 2-3 Angola-(Uwanja wa Bouaké)
-
23/01/2024, 20:00Angola 2-0 Burkina Faso-(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
23/01/2024, 20:00Mauritania 1-0 Algeria-(Uwanja wa Bouaké)
-
-
-
-
Kundi E
Nchi P W L D GD Pts Mali 3 1 0 2 2 5 Afrika Kusini 3 1 1 1 2 4 Namibia 3 1 1 1 -3 4 Tunisia 3 0 1 2 -1 2 -
16/01/2024, 17:00Tunisia 0-1 Namibia-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
16/01/2024, 20:00Mali 2-0 Afrika Kusini-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
20/01/2024, 20:00Tunisia 1-1 Mali-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
21/01/2024, 20:00Afrika Kusini 4-0 Namibia-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
24/01/2024, 17:00Namibia 0-0 Mali-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
24/01/2024, 17:00Afrika Kusini 0-0 Tunisia-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
-
Kundi F
Nchi P W L D GD Pts Morocco 3 2 0 1 4 7 DR Congo 3 0 0 3 0 3 Zambia 3 0 1 2 -1 2 Tanzania 3 0 1 2 -3 2 -
17/01/2024, 17:00Morocco 3-0 Tanzania-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
17/01/2024, 20:00DR Congo 1-1 Zambia-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
21/01/2024, 14:00Morocco 1-1 DR Congo-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
21/01/2024, 17:00Zambia 1-1 Tanzania-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
24/01/2024, 20:00Tanzania 0-0 DR Congo-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
24/01/2024, 20:00Zambia 0-1 Morocco-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
-
-
Hatua ya 16 Bora
-
27/01/2024, 17:00Angola 3-0 Namibia-(Uwanja wa Bouaké)
-
27/01/2024, 20:00Nigeria 2-0 Cameroon-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
28/01/2024, 17:00Equatorial Guinea 0-1 Guinea-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
28/01/2024, 20:00Misri 1-1 DR Congo7-8(Penati)(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
29/01/2024, 17:00Cape Verde 1-0 Mauritania-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
29/01/2024, 20:00Senegal 1-1 Ivory Coast4-5(Penati)(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
30/01/2024, 17:00Mali 2-1 Burkina Faso-(Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
-
30/01/2024, 20:00Morocco 0-2 Afrika Kusini-(Uwanja wa Laurent Pokou)
-
-
Robo- Fainali
-
02/02/2024, 17:00Nigeria 1-0 Angola-(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
02/02/2024, 20:00DR Congo 3-1 Guinea-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
03/02/2024, 17:00Mali 1-2 Ivory Coast-(Uwanja wa Bouaké)
-
03/02/2024, 20:00Cape Verde 0-0 Afrika Kusini1-2(Penati)(Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
-
-
Nusu- Fainali
-
07/02/2024, 17:00Nigeria 1-1 Afrika Kusini4-2(Penati)(Uwanja wa Bouaké)
-
07/02/2024, 20:00Ivory Coast 1-0 DR Congo-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
-
Nafasi ya 3 na ya 4
-
10/02/2024, 20:00Afrika Kusini 0-0 DR Congo6-5(Penati)(Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
-
-
Fainali
-
11/02/2024, 20:00Nigeria 1-2 Ivory Coast-(Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
-
Ni nani nyota wanaovutia macho huko Ivory Coast

Chanzo cha picha, Getty Images
Emilio Nsue Lopez (Guinea ya Ikweta)
Nahodha wa National Thunders ya Equatorial Guinea, ameibuka kinara katika hatua ya makundi, akifunga mabao matano katika mechi tatu tayari. Licha ya kuwa mlinzi wa klabu yake, mchezaji huyo wa zamani wa Middlesbrough na Birmingham City anaongoza safu ya ushambuliaji katika timu yake ya taifa. Akiwa na mabao matatu ya ajabu dhidi ya Guinea Bissau na mabao mawili dhidi ya wenyeji Ivory Coast, Nsue ni mshindani mkubwa wa tuzo ya Golden Boot
Georges-Kevin N'koudou (Cameroon)
Akiwa na msaada wa kufunga mabao mara tatu kwenye michuano hiyo, winga wa Cameroon, Nkoudou ni mmoja wa waliobadilisha mchezo kwenye Afcon 2023. Huenda Indomitable Lions walitatizika kupita hatua ya makundi, lakini kiungo huyo anayeishi Saudia hajashindwa kufanya vizuri wakati muhimu zaidi. Misaada yake mara mbili katika mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Gambia, uliokoa ushindi wa mabao 3-2 kwa Simba, ambao sasa wanatarajiwa kumenyana na wapinzani wanaowafahamu, Nigeria katika hatua ya 16 bora.
Sadio Mane (Senegal)
Wengi walidhani kwamba uhamisho wa pesa nyingi wa Sadio Mane kwenda klabu ya Saudia, Al-Nassr ungeweza kuashiria mdororo wa mchezo kwa winga huyo wa Senegal, lakini mwanasoka huyo bora wa mwaka wa Afrika mara mbili anadhihirisha wenye shaka kuwa sio sahihi nchini Ivory Coast. Akija kwenye dimba hilo, siku chache baada ya harusi yake, Mane amekuwa na ushawishi mkubwa katika utendaji bora wa mabingwa hao watetezi kwenye hatua ya makundi, akiwa na bao moja na asisti mbili.
Achraf Hakimi (Morocco)
Hakimi has been at the heart of the Atlas Lion's campaign at the Afcon so far. With one goal and an assist to his name, Hakimi has been involved in most of the goals scored by the pre-tournament favourites, creating attacking threats from the flanks and stepping up to set piece duties.
Gelson Dala (Angola)
Gelson Dala alifunga mabao mawili wakati Angola ilipoilaza Mauritania 3-2 katika moja ya mchezo wa kuburudisha sana Afcon 2023. Mchezaji huyo wa Angola amekuwa mzuri kwa kuiongoza nchi yake katika michuano hiyo kwa kasi yake ya kulipuka na ustadi wa kucheza chenga na kusababisha matatizo kwa wapinzani. Mshambulizi huyo wa Qatar anatarajiwa kuimarika katika kiwango chake kizuri kwa Palancas Negras katika hatua za mwisho za shindano hilo.
Stanley Nwabali (Nigeria)
Kuingia kwa Afcon mwaka huu, wasiwasi mkubwa wa Nigeria ulikuwa kuhusiana na nafasi ya golikipa huku mashabiki wakihoji uwezo wa makipa, Francis Uzoho na Maduka Okoye. Mchezaji wa Chippa United Stanley Nwabali aliingia pichani kwa ajili ya Nigeria usiku wa kuamkia mchuano huo na alicheza mechi yake ya kwanza tu katika kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa awali dhidi ya Guinea. Onyesho lake la hadi sasa kwenye dimba, hata hivyo imekuwa msaada mkubwa kwa safu ya ulinzi ya Super Eagles, kwa kutofungwa mara mbili katika mechi tatu.
Uchaguzi wa kikosi cha AFCON 2023 na ushirikishe
Kwa kutumia mtandao wetu, chagua timu yako unayoipenda ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutoka kwenye orodha yetu na uishirikishe marafiki zako.
Chagua mbinu
Chagua Mlinzi
Michuano hiyo itajumuisha makundi sita ya timu nne (A-F) huku timu mbili za juu zikifuzu moja kwa moja hatua ya 16 ya mwondoano.
Timu hizo 12 zitaunganishwa na timu nne zilizoshika nafasi ya tatu bora kutoka makundi sita, zikiwa na vigezo vinavyozingatia matokeo sambamba baina ya timu na pili tofauti ya mabao.
Utafiti na Damilola Ojetunde, uliyofanyiwa kazi na Olaniyi Adebimpe na Umeandaliwa na Boaz Ochieng
Wachezaji sita ambao vilabu vya Ulaya huenda vinawaangalia katika mashindano ya Afcon 2023

Chanzo cha picha, Getty Images
Lamine Camara (Senegal) | 20 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa – Metz ()
Mwanasoka huyo bora chipukizi wa Afrika amejitangaza kwenye onyesho kubwa zaidi la soka barani Afrika kwa kufunga mabao mawili na kufanya vyema kwa mabingwa hao watetezi katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Gambia. Baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (Chan), Camara anaweza kuwakito cha thamani kwa dimba hilo huku vilabu vya juu vya Ligi ya Premia vikimtaka kinda huyo mwenye umri wa miaka 20.
Jesus Owono (Equatorial Guinea) | 22 | Mlinda lango | Klabu ya sasa– Alaves (Spain)
Golikipa huyo wa Equatorial Guinea amekuwa kipa bora zaidi kwenye michuano hiyo akiwa amecheza vyema dhidi ya Nigeria na Ivory Coast, jambo ambalo lilimwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Akiwa na umri wa miaka 22, anaweza kuwa kipa bora zaidi barani Afrika, akifuata njia ya magwiji kama Carlos Kameni, Vincent Enyeama na Thomas Nkomo, kama wafungaji bora kutoka bara.
Mohammed Kudus (Ghana) | 23 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa – West Ham
Huenda ikawa kampeni ya kutamausha kwa Black Stars ya Ghana kwenye Afcon 2023 lakini Mohammed Kudus wa West Ham, aliridhisha matarajio ya wengi licha ya kusumbuliwa na majeraha. Alikosa ushindi wa 1-2 dhidi ya Cape Verde katika mechi ya kwanza ya kundi la Ghana lakini akarejea kwa kufunga bao moja katika mchezo bora dhidi ya timu ya Mo Salah ya Misri. Alipata tena tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika sare ya 2-2 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wao wa mwisho wa kundi, ambao ulihitimisha matumaini ya Ghana kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Emam Ashour (Egypt) | 25 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa - Al Ahly (Egypt)
Kiungo wa Al Ahly, Emam Ashour amekuwa bora mpaka sasa -Misri, licha ya Farao kutinga hatua ya 16 bora Afcon 2023. Washindi hao ambao walimpoteza nahodha Mohammed Salah kutokana na majeraha katika mchezo wao wa pili wa kundi, wamefanikiwa kutinga hatua hiyo ya mtoano, baada ya Msumbiji kuharibu nafasi za Ghana. Ashour, ambaye anafananishwa na wengi na mchezaji wa zamani wa Misri, Ahmed Hassan, amekuwa mtu mzuri wa kati kwa Mafarao, akitoa msaada wa ulinzi na kulipuka kwa nguvu kwenye mashambulizi ya timu hiyo. Anahusishwa na uhamisho wa kwenda Uhispania, Barcelona msimu ujao wa joto
Aboubakary Koita (Mauritania) | 25 | Mshambuliaji | Klabu ya sasa - Sint Truidense (Belgium)
Bila shaka Mauritania ni moja ya timu za kushtukiza kwenye Afcon 2023 na mtu mmoja, anayeendesha ndoto ya timu kwenye mashindano hayo ni Aboubakary Koita. Miondoko yake ya kasi, uchezaji wa winga na jicho la kulenga lango kumeisaidia Al-Murabitun kutinga hatua ya 16 bora, waliyoipata kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa Afcon 2019, Algeria. Bila shaka Koita ndiye wa kuangaliwa katika hatua inayofuata ya shindano hilo.
Aguibou Camara (Guinea) | 22 | Mshambuliaji wa pembeni |Klabu ya sasa - Atromitos (Greece)
Camara alivutia wengi kwenye michuano ya Afcon inayoendelea baada ya kuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Gambia. Bao lake la dakika ya 69 lilitosha kuwapatia Waafrika Magharibi ushindi wa kwanza kwenye dimba hilo na Camara anaweza kuweka historia zaidi huku Syli Nationale wakijikatia tiketi ya kutinga hatua ya mtoano kama moja ya timu zilizo nafasi ya tatu bora.
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah