Fahamu kiini cha msako mpya dhidi ya 'polisi wauaji' wa Kenya na kutafuta haki

Na Ambia Hirsi

Wanaharakati wa Kenya wamekuwa wakiandamana kupinga mauaji ya kiholela yanayofanywa na polisi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanaharakati wa Kenya wamekuwa wakiandamana kupinga mauaji ya kiholela yanayofanywa na polisi

Kukamatwa kwa maafisa wanne wa polisi wa Kenya wanaodaiwa kuhusika na msururu wa mauaji, utekaji nyara na mateso nchini Keya kumezua gumzo kuhusu utenda kazi wa polisi.

Maafisa hao waliofikishwa mahakamani mjini Nairobi Jumanne Oktoba 24 walikuwa sehemu ya kikosi maalum ambacho kilivunjwa na Rais William Ruto kwa madai ya kutekeleza mauaji ya kiholela na kutoweka kwa washukiwa kwa miaka kadhaa.

Miongoni mwa wanaodaiwa kuwa wahasiriwa wa hivi punde ni raia wawili wa India waliotoweka mwezi Julai na ambao mabaki yao yaligunduliwa wiki iliyopita katika msitu mmoja katikati mwa Kenya.

Wanachama wa Kitengo cha Huduma Maalum kilichovunjwa sasa wanakabiliwa na mashtaka mengi yakiwemo mauaji, matumizi mabaya ya ofisi na kula njama ya kutenda uhalifu.

Kitengo hicho kilivunjwa baada ya rais kupokea ripoti ya polisi kuhusu kutoweka kwa raia hao wawili wa India.

Zulfiqar Ahmad Khan na Mohamed Zaid Sami Kidwai walikuwa nchini Kenya kusaidia kampeni za uchaguzi za Bw Ruto, lakini walitoweka pamoja na dereva wao wa eneo hilo Nicodemus Mwania mara baada ya kuchukuliwa na polisi jijini Nairobi.

Polisi Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema uchunguzi wao huru umehusisha kikosi hicho na vitengo vingine vya polisi na vifo vya zaidi ya watu 600 katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Baadhi ya miili hiyo ilipatikana baadaye katika mito magharibi na kaskazini mwa Kenya.

Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na ya ndani sasa unaitaka serikali kuwafungulia mashitaka maafisa hao, na kuwalipa fidia waathiriwa wa unyanyasaji wa polisi.

Historia ya mauaji ya kiholela

Vitengo hivi maalum hubuniwa kukabiliana na uhalifu lakini maswali yameibuka kuhusu ni wakati gani maafisa wanakiuka maadili ya kazi na wao wenyewe wakageuka kutekeleza uhalifu wanaopambana kukabiliana nao.

Mchambuzi wa masuala ya usalama Georgre Musamali anasema: Tatizo ni moja Ufisadi- Hili linakuja pale maafisa wa kitengo hicho maalum wanapoingiwa na amaa ya kijitajirisha wao wenyewe ndipo wanachana na majukumu walilopewa na kuingilia masuala mengine ambayo hayaambatani na kazi yao.

''Kitengo kinaanza vizuri hapo katikati mambo yanabadilika wanaanza kuwa wahalifu ...kikivunjiliwa mbali tunaleta kigine hali ninakuja inakuwa ni hiyo hiyo tu'' alisema akiongeza kuwa maafisa wanaishia kutumiwa vibaya kwa maslahi ya watu binafsi badala ya kazi waliyopewa kufanya.

Pia naongeza kuwa historia ya mauaji ya kiholela imekuwepo tangu miaka ya sabini. Lakini ilipofika miaka ya tisini anasema kulianzishwa kitengo cha kukabiliana na uhalifu cha Flying Squad.

''Kitengo hicho kilibuniwa na Kamishena wa polisi wakati huo Phillip Kilonzo ili kukabiliana na wizi wa mabavu, na uhalifu mwingine sugu kwa sababu serikali wakati huo ilionelea haja ya kutumia nguvu kiasi kuvunja mtandao wa uhalifu,'' anasema Bw. Musamali.

Kwa miaka kadhaa vikosi hivi maalum vimetumiwa kukabiliana na uhalifu kwa kiwango kikubwa. kwa wale wanaoathiriwa moja kwa moja na wahalifu hao wamepata ahueni.

Kesi za mauaji amabazo hazijatatuliwa

Miongoni mwa mauaji na kupotea kwa watu mashuhuri ambayo bado hayajatatuliwa ni mauaji ya mfanyabiashara Jacob Juma, meneja wa ICT wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Chris Musando, shahidi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Meshack Yebei, afisa wa usalama wa Rais Ruto Kipyegon Kenei, mwanaharakati Oscar King' ara, Mbunge wa Kabete George Muchai, Sheikh Abubakar Shariff almaarufu Makaburi na Sheikh Aboud Rogo.

Wanaharakati wa haki pia wameitaka tume ya uchunguzi kuchunguza mauaji ambayo hayajasuluhishwa na kutekelezwa kwa watu kutoweka.

Hilo likitokea, linaweza kitafichua shughuli za siri za baadhi ya vipengele katika jimbo na kuwavuta waendeshaji wa ngazi za juu katika mfumo wa usalama wanasema wanaharakati hao.

M

Kitengo cha SSU kilibuniwa vipi?

Kitengo Maalum cha Kuzuia Uhalifu (SU) kilibadilishwa na kuitwa Kitengo Maalum cha Huduma (SSU).

Kulingana na muundo wa utenda kazi wa Idara ya polisi nchini Kenya, Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI ina mamlaka ya kubuni kitengo maalum cha polisi ili kusaidia kukabiliana na uhalifu sugu.

Ni kwa msinguo ndiposa Mkuu wa zamani wa DCI George Kinoti alibuni kitengo hicho chini ya Idrara ya Upelelezi mwaka 2019.

Kwa muda mrefu Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ya Kitengo Maalum cha Huduma (SSU) iliyovunjwa ilitegemewa kutatua uhalifu tata. Kitengo hicho pia kilitegemewa kujibu tukio lolote la mauaji lililohusisha wahalifu wa kikatili kwa kukimbia au masuala ambayo hayajatatuliwa na hata ugaidi.

Baadhi ya maafisa waliohudumu katika kitengo kilichovunjwa cha SSU walikuwa waliwahi kuhudumu katika kitengo cha SU na Kikosi cha Flying Squard kilichovunjiliwa mbali miaka kadhaa iliyopita.

Vitengo vingine maalumu chini ya Idara ya Upelelezi wa Jinai ni Pamoja na kile kinachohusiana na uhalifu wa mtandaoni, Sting Squad Headquarters (SSH), Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi (CRIB) ambayo ni ya shughuli zinazoendeshwa na kijasusi, Silaha, Eneo la Uhalifu, Msajili Mkuu wa Uhalifu, Kitengo cha Ujasusi wa Uhalifu na Vitengo vya Maabara ya DNA, Sumu, Kemia na Biolojia ya Mauaji.

Maafisa wa polisi wanaohusishwa na vitengo hivi maalum ni tofauti na wenzao wanaofanya kazi za kawaida. Kwa mfano, wao huvaa nguo za kawaida na kupanda magari yasiyo na alama, ambayo nyakati zingine zinatumia nambari za usajili za kigeni.

Na ingawa maafisa wa polisi wanaofanya kazi za kawaida wanatakiwakunyoa nywele na kudumisha unadhifu wa hali ya juu, wale walio katika vitengo hivi mara nyingi huvaa suruali zisizo na mvuto, fulana za mtindo, nywele zilizosokotwa na ndevu ndefu endapo tu watalazimika kuficha muonekano wao.

Ni nadra sana maafisa wa kitengo hiki kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi kw asababu oparesheni zao hufanywa kwa usiri mkubwa.

Pia hawapelekwi kukamata watu kwa sababu oparesheni yao inahusisha kufyatulianaji wa risasi na mara nyingi huishia katika vifo vya washukiwa.

Kwanini kilivunjiliwa mbali?

Kumekuwa na tuhuma kwamba polisi wamekuwa wakihusika na vifo na kupotea kiholela kwa Wakenya ambapo wanaharakati wa haki za binadamu wametaka uchunguzi ufanyike.Mnamo Aprili na Mei 2019, Shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ilihoji watu 35 wakiwemo mashahidi, wanafamilia wa waathiriwa, madaktari na wafanyakazi wa kijamii, wanaharakati, na wafanyakazi wa polisi akiwemo msemaji wa polisi jijini Nairobi.

Shirika hilo katika ripoti yake linasema lilifanya kazi kwa karibu na mashirika washirika huko Dandora na Mathare jijini Nairobi katika kutambua waathiriwa na familia.

Mfanyabiashara ambaye pia ni mtoaji habari wa polisi aliiambia Shirika hilo kwamba polisi wana orodha ya watu wanaopanga kuwaua, wakiwemo wezi mbali na wanaume na wanawake ambao wametofautiana na maafisa hao.

Human Rights Watch pia imeandika mauaji ya kiholela katika muktadha wa ghasia za uchaguzi na oparesheni za kukabiliana na ugaidi huko Nairobi na eneo la kaskazini mashariki, na pwani katika operesheni za kukabiliana na ugaidi.

Imedaiwa kwamba  baadhi ya wanachama wa kitengo hicho pia walihusika katika uhalifu wa kutumia silaha katika eneo la matuu ambapo walivamia kampuni moja ya kusambaza gesi na kuiba zaidi ya  ksh.370,000  miongoni mwa visa vingine chungu nzima. Â