Ni kwanini Ubelgiji ilitunza jino la dhahamu la shujaa wa Afrika?

Chanzo cha picha, Getty Images
Jino lililovikwa taji la dhahabu ndio masalia pekee ya shujaa wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba.
Alipigwa risasi na kikosi cha kufyatua risasi mwaka 1961 kikiungwa mkono kimya kimya na utawala wa ukoloni wa Kibelgiji, mwili wake ulizikwa katika kaburi fupi, lilichimbwa na kusafirishwa kilomita 200 (maili 125 ), akazikwa tena, akafufuliwa na halafu akakatwa vipande vipande na hatimaye kuyeyushwa kwa asidi.
Kamishna wa polisi wa Ubelgiji, Gerard Soete, ambaye alisimamia na kushiriki katika kuangamiza mabaki alichukua jino, alikiri baadaye.
Pia alizungumzia kuhusu jino la pili na vidole viwili vya maiti, lakini hivi havikupatiana.
Imepangwa sasa kwamba jino lake litarejeshwa kwa familia yake katika sherehe itakayofanyika katika mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.
Soete ambaye alitunza vipande vya mwili ilielezea pia kuhusu tabia ya maafisa wa kikoloni wa Ulaya ya kurejesha masalia ya mwili nyumbani baada ya miongono kama kipindi cha kukumbuka kuwa kila mtu lazima atakufa.
Lakini pia hatua hiyo ni udhalilishaji wa mwisho wa mwanaume ambaye Ubelgiji ulimchukuliwa kama adui.
Soete, ambaye alionekana katika makala mwaka 1999, alilielezea jino na vidole alivyovichukua kama "aina ya nyara ya uwindaji". Lugha inayoonyesha kwamba kwa polisi huyo Mbelgiji, Lumumba- ambaye alikuwa anaheshimiwa kote barani Afrika kama sauti inayoongoza ya ukombozi wa Waafrika – alikuwa binadamu wa kudharauliwa.
Kwa binti yake Lumumba, Juliana, swali analojiuliza ni iwapo waliomuua walikuwa binamu au la. "Unahitaji kiwango gani cha chuki kufanya unyama kiasi hicho");