Je, nguvu ya mashambulizi ya Iran inalinganishwaje na ya Israel?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, By Arif Shamim
- Nafasi, BBC News Urdu & BBC News Persian
Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limefanya mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani na roketi kaskazini mwa Israel katika kipindi cha wiki moja iliyopita, lakini linaonya kuwa hatua yake ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kamanda wa ngazi ya juu wa Israel mwezi Julai bado haijafika.
Mapema siku ya Jumanne, watu wanne waliuawa katika shambulio la nyumba moja katika mji wa Mayfadoun nchini Lebanon, karibu kilomita 30 kaskazini mwa mpaka, madaktari na chanzo cha usalama kimesema.
Mapigano hayo yanafuatia kuongezeka kwa mvutano kati ya Israel, Iran na Hezbollah, na kusababisha hofu ya kuzuka kwa mzozo mkubwa.
Kwa hivyo, pande hizi zingeegemea wapi iwapo vita vikubwa vingezuka?

Chanzo cha picha, EPA
Wiki iliyopita, Hamas ilisema kiongozi wake wa kisiasa, Ismail Haniyeh, aliuawa katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Israel haijathibitisha iwapo ilihusika na shambulio hilo.
Kumekuwa na mvutano mkubwa tangu Iran ilipoanzisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Israel tarehe 13 mwezi Aprili na ndege isiyo na rubani ya Israel ilishambulia eneo la kijeshi nchini Iran.
Ingawa hakukuwa na majeruhi wengi nchini Israel, mashambulizi ya mabomu zaidi ya 300 yalionyesha uwezo wa Iran wa kushambulia kutoka mbali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Upande gani una udhibiti?
BBC imepima swali hili kwa kutumia vyanzo vilivyoorodheshwa hapa chini, ingawa kila nchi inaweza kuwa na uwezo mkubwa ambao umefichwa.
Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati (IISS) inalinganisha nguvu ya mashambulizi ya majeshi ya mataifa yote mawili, kwa kutumia njia mbalimbali rasmi na za wazi ili kupata makadirio bora iwezekanavyo.
Mashirika mengine, kama vile Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, pia hufanya tathmini, lakini usahihi unaweza kutofautiana kwa nchi ambazo mara nyingi hazitoi takwimu.
Hata hivyo, Nicholas Marsh, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Amani Oslo (PRIO), anasema IISS inaonekana kama alama ya kutathmini nguvu za kijeshi za nchi duniani kote.

IISS inasema Israel ina matumizi ya juu zaidi katika bajeti yake ya ulinzi kuliko Iran, na kuipa nguvu kubwa katika mzozo wowote unaoweza kutokea.
IISS inasema bajeti ya ulinzi ya Iran ilikuwa karibu $7.4bn mwaka 2022 na 2023, wakati Israel ilikuwa na zaidi ya mara mbili ya bajeti hiyo, karibu $ 19bn.
Matumizi ya ulinzi wa Israel ikilinganishwa na Pato la Taifa (kipimo cha pato lake la kiuchumi) pia ni mara mbili ya Iran.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatua inayofuata
Israel na Hezbollah zimeongeza mashambulizi dhidi yao. Israel imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Hezbollah nchini Lebanon na kusema kuwa ilitekeleza mauaji ya kamanda wa ngazi ya juu Fuad Shukr tarehe 30 Julai 2024.
Hezbollah imerusha makombora kaskazini mwa Israel. Mfumo wa Israel wa Iron Dome wa kupambana na makombora ulizuia mengi kati ya mashambulio hayo.
Hata hivyo, Jeremy Binnie, mtaalamu wa Ulinzi wa Mashariki ya Kati katika jarida la uchambuzi wa ulinzi Janes anaonya, "Iron Dome ni mfumo wa ulinzi unaotetea dhidi ya makombora ya masafa mafupi na makombora yaliyorushwa kutoka Lebanon, ingawa inadhaniwa kwamba Hezbollah ina makombora mengi zaidi ya kuutatiza ulinzi wa anga wa Israel kwa muda mrefu.''
Nicholas Marsh wa Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Oslo anasema "Iran imechapisha orodha kubwa ya maeneo itakayoyashambulia. Hii inaweza kuwa ni jaribio la kusumbua. Lakini itakuwa vigumu kwa Israel kufikia malengo yote yanayowezekana."

Chanzo cha picha, WAEL HAMZEH/EPA-EFE/REX/Shutterstock
Je, kunaweza kuwa na shambulio kubwa?
Mhariri wa masuala ya ulinzi Tim Ripley ameiambia BBC kuwa wanaopanga mikakati ya kijeshi wanapaswa kufikiria "mbinu mbali mbali" kuhusu majibu ya Iran na Hezbollah.
"Lazima ujiingize katika mawazo ya Wairani, Hezbollah na Wahouthi (wanamgambo wa Kiislamu ambao wamekuwa wakishambulia meli za kimataifa katika Mashariki ya Kati). Kwa nini upoteze juhudi zako kufanya kitu kimoja tena");