'Bibi wa Taifa wa Burundi' anavyowasaidia waathirika wa mauaji ya kikabila
Baadhi humuita Bibi wa Taifa na wengine Mama wa Taifa: Haya ni majina aliyopewa Marguerite Barankitse, mwanaharakati na mwanzilishi wa kituo cha Maison Shalom nchini Burundi.
Amejitolea kusaidia wanyonge, hasa wale ambao walikuwa hatarini baada ya mauaji ya kikabila yaliyotokea kwa nyakati tofauti nchini Burundi.
Marguerite Barankitse [Maggy] alikimbilia Rwanda mwaka 2015 akishutumiwa na serikali ya Burundi kuungana na wale waliotaka kupindua serikali madai anayokanusha.
Huku kituo chake cha Maison Shalom kikiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, Barankitse anasema ingawa aliacha shughuli zake nyingi Burundi, hana hamu ya kurejea nchini humo hadi usalama utakaporejea.
Serikali ya Burundi inasema hali ni salama na kuwataka wakimbizi wote kurejea makwao.
Marguerite Barankitse amezungumza na Mwandishi wa BBC Yves Bucyana mjini Kigali.