Lifahamu Jiji la Afrika, linalotaka kufutwa na Ulaya

Great Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Mji wa kale wa Great Zimbabwe ulikuwa wa ajabu kiuhandisi. Lakini wanaakiolojia na kila mtu aliusifu, kuanzia Wababeli, Waarabu - isipokuwa Waafrika ambao ndio waliojenga.

Hata hivyo, kwa karibu karne moja, wakoloni wa Ulaya wa mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 walihusisha ujenzi huo na watu wa mataifa ya nje na wavumbuzi wa nje, badala ya Waafrika wenyewe.

Wageni wanaokuja Great Zimbabwe leo bado wanaweza kutembelea sehemu tatu: Magofu ya Milima (ya kale zaidi, yenye jumba kubwa linaloaminika kuwa la kifalme); Uzio uliozungukwa na ukuta mkubwa, mrefu na una mnara wenye urefu wa mita 11); na Magofu ya Bonde (mkusanyiko wa nyumba za matofali ya udongo ambapo watu wengi wa kale waliishi).

Cynthia Marangwanda, mwandishi anayeandika kuhusu utambulisho wa taifa la Zimbabwe, alieleza kuwa "baadhi ya watu wanataka kuiita 'magofu ya Great Zimbabwe', lakini sikubaliani na hilo."

Katika lugha ya Kishona, Great Zimbabwe hutafsiriwa kama "nyumba ya mawe", kwa sababu ya ukubwa wake. Zaidi ya hayo, haikuwa Great "Zimbabwe" pekee kama hiyo: kuna mabaki ya takriban makazi 200 madogo au vituo vya biashara vilivyoenea katika eneo lote, kutoka Jangwa la Kalahari nchini Namibia hadi Msumbiji.

Great Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuta zake zimefungwa kwa usahihi na hazitumii chokaa ama saruji kuzijenga. Zimetumia madini ya granite, inayopatikana katika mazingira ya karibu. Umaarufu wa mji huu wa kale wa Great Zimbabwe ulianza kupungua katikati ya Karne ya 15 wakati Ufalme wa Zimbabwe ukidhoofika, lakini mabaki ya jiji hilo hayajatelekezwa.

Unaetembelewa mara kwa mara na vikundi mbalimbali vya Washona kwa sababu za kiroho mpaka wakati wa ukoloni wa Waingereza mwishoni mwa Karne ya 19.

Munyaradzi Manyanga, profesa wa mambo ya kale na urithi wa kitamaduni wa Chuo Kikuu cha Great Zimbabwe, anasema,"Ubaguzi wa rangi wa wakati huo haukuweza kufikiria kuwa Great Zimbabwe unaweza kuhusishwa na wakazi wa Afrika, ambao wakati huo walikuwa wakiishi maisha ya vijijini sana katika vibanda vidogo vidogo vya vilimani".

Great Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanaakiolojia wa Uingereza James Theodore Bent, baada ya kuongoza kuchimba waka 1891, aliandika kitabu akitangaza kwamba Waafrika hawakuwa na uwezo wa kujenga kile alichokiona.

Hata hivyo, kumekuwa na taarifa za kihistoria zinazolionyesha eneo hilo kama kazi za wageni na sio waafrika. Ni kama kusambaratisha historia yake.

"Serikali ya wakati huo ya kikoloni ilikandamiza maoni kwamba ni kazi ya wazawa, na simulizi rasmi katika vyombo vya habari vya umma na majumba ya makumbusho ni kwamba Great Zimbabwe ilikuwa na asili ya kigeni," alisema Manyanga.

Great Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Eneo hili la historia lilidumishwa hadi miaka ya 1960 na 1970 na serikali ya wazungu wachache ya koloni.

Ni mwaka 1980 , Baada ya Zimbabwe kupata uhuru, ndipo viongozi wapya walipoweza kuthibitisha kwamba eneo hilo lilijengwa na mababu zao wenyewe. Wakati wa miaka ya 1960, wazalendo weusi walikuwa wameishi Zimbabwe kama jina la nchi waliyotarajia kuongoza kwa uhuru, wakirejea Zimbabwe Kuu.

Tangu 1980, utafiti wa kiakiolojia wa ndani umekuwa umekua ukisuasua kuendelea na zaidi umejikita kwa kiasi kikubwa kwenye matengenezo na ukarabati.

Leo, jiji kuu la kale bado ni muhimu kwa Wazimbabwe. Vijiji vya Washona viko karibu, na wakazi wengi wanafanya kazi ili kulitunza eneo hilo. Kituo cha kidini kiko karibu pia, na eneo hilo bado linawavutia wanaoabudu na wanaofuata imani za kitamaduni za Kishona.

"Waafrika ndio walitengeneza hili," mwandishi Cynthia Marangwanda alisema. "Na zaidi ya milenia moja baadaye bado lipo imara. Ni ushuhuda wa sisi ni watu wa aina gani."