Mwalimu aliyepoteza kazi kwa kutuma picha zake Instagram

Baraza la chuo kikuu lilikutana naye na kumtaka ajieleze kwa baadhi ya hadithi ambazo alizichapisha miezi miwili kabla ya kuanza kazi kama profesa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baraza la chuo kikuu lilikutana naye na kumtaka ajieleze kwa baadhi ya hadithi ambazo alizichapisha miezi miwili kabla ya kuanza kazi kama profesa 

Chuo kikuu maarufu binafsi katika mji wa mashariki mwa India wa Kolkata (uliofahamika awali kama Calcutta) kimegubikwa na utata katika miezi ya hivi karibuni.   

Profesa msaidizi wa zamani katika chuo  kikuu cha  Mt Xavier aliiambia BBC kuwa alilazimika kuacha kazi yake kwa kuwa alichapisha picha zake zilizoonesha akiwa amevaa nguo ya ndani aina ya bikini kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.   

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye aliomba jina lake lisitajwe, aliwashutumu maafisa wa chuo hicho  kikuu  kwa  " kumnyanyasa kingono " na anasema "alitishwa, kudhalilishwa na kuchunguzwa maadili."

Pia aliwasilisha  malalamiko kwa polisi na kutuma taarifa ya  kisheria kwa taasisi, ambayo ilijibu kwa kumshutumu kwa kuichafulia jina na kudai ilipwe rupia milioni 990   (takriban dola milioni $2.4) kama fidia.   

   Walinipeleka katika chumba cha upelelezi

Profesa msaidizi anasema kwamba alijiunga na kitivo  tarehe 9 Agosti , 2021 kwa ajili ya kufundisha somo la Kiingereza kwa wanafunzi wanaosomea shahada.

Miezi miwili baadaye, aliitwa katika ofisi ya mkuu wa chuo kwa ajili ya mkutano.    

Aliongozwa "hadi katika chumba cha upelelezi" ambako alihojiwa na kamati inayojumuisha Makamu mkuu wa chuo  Felix Raj, katibu wa chuo Ashish Mitra na wanawake watano.

Alifahamishwa kuwa kulikuwa na malalamiko dhidi yake yaliyotolewa na baba wa mwanafunzi wa kiume anayesomea shahada. 

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walimuuliza iwapo hakuweza kufikiria hilo, kama mwanamke picha zake ziliibua maswali na kama wazazi wake walikuwa wameziona

"Mkuu wa Chuo alisema kwamba baba huyu alimpata mwanaye wa kiume akizitazama picha zangu kwenye Instagram ambapo nilikuwa nimevaa nguo ya ndani. Alisema picha zilikuwa zinaonesha utupu na akakiomba chuo kikuu kimuepushe mwanaye na uchafu wa aina hiyo."

Wajumbe wa bodi walizungusha kipande cha karatasi kilichokuwa na "picha tano- sita " na kumuomba athibitishe kwamba zilikuwa ni zake.  

"Wazazi wako wameona picha hizi");