Picha mpya zinazoonyesha jinsi Meli ya Titanic inavyooza chini ya bahari

v

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc

Maelezo ya picha, kwa sasa meli ya Titanic imepoteza sehemu yake kubwa

Ilikuwa ni picha iliyofanya kifusi cha meli ya Titanic iliyopata ajali kutambulika mara moja kikionekana kwenye eneo la giza la kina cha bahari ya Atlantiki.

Lakini uvumbuzi huu mpya umefichua athari za kuoza taratibu kwa sehemu kubwa ya mabaki ya meli hiyo iko kwenye sakafu ya bahari.

Mabaki ya meli hiyo yaligunduliwa wakati wa msururu wa upigaji wa roboti za chini ya maji katika msimu huu wa kiangazi.

Picha zilizochukuliwa na roboti hizo zinaonyesha jinsi kifusi hicho cha Titanic kilivyobadilika baada ya zaidi ya miaka 100 chini ya mawimbi ya bahari.

Meli hiyo ilizama Aprili 1912 baada ya kugonga jiwe la barafu, na kusababisha vifo vya watu 1,500.

Unaweza pia kusoma:
g

Chanzo cha picha, RMS Titanic Inc

"Muundo wa upinde wa Titanic ni wa kipekee – na ni wa nyakati zote - na ndivyo unavyofikiria unapofikiria ajali ya meli. Lakini sasa hauonekani hivyo tena,” alisema Tomasina Ray, mkurugenzi wa ukusanyaji wa vifusi katika taasisi ya RMS Titanic Inc, kampuni iliyofanya ugunduzi huo.

"Ni ukumbusho mwingine tu wa kuoza kwa meli unaotokea kila siku. Watu huuliza kila mara: 'Titanic itakuwa huko kwa muda gani");