Kwa Picha: Majengo marefu zaidi duniani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jumba la Jeddah Tower

Ujenzi wa jengo refu zaidi duniani huenda utakamilika hivi karibuni.

Baada ya kukamilika, jengo hili litavunja rekodi ya mijengo mingine mirefu zaidi duniani kwa tofauti kubwa.

"Jeddah Tower" lenye urefu wa ajabu wa mita elfu moja katika bandari ya Jeddah nchini Saudi Arabia ni takriban mita 200 juu kuliko majengo marefu zaidi ya kisasa duniani.

Lakini je, jengo refu zaidi duniani ambalo linashikilia rekodi ni lipi?

Burj Khalifa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Burj Khalifa, ambalo ndio jengo refu zaidi duniani likiwa na urefu wa mita 828, liko Dubai. Urefu wa jengo hili ni kama minara mitatu ya Eiffel huko Paris.

Jengo hili sio tu linashikilia rekodi ya jengo refu zaidi ulimwenguni, lakini pia linashikilia rekodi zingine, pamoja na rekodi ya lifti ndefu zaidi katika jengo na mgahawa wa juu zaidi kutoka ngazi ya chini.

Merdeka 118

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Merdeka 118 liko Kuala Lumpur, Malaysia na lina urefu wa mita 679 na kama jina lake linavyoashiria, ilna ghorofa 118. Jengo hili ni refu na ni mara saba ya sanamu ya Liberty zikisimamishwa.

Shanghai Tower

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jengo refu zaidi nchini China lina urefu wa mita 632. lilifunguliwa mwaka wa 2016 na linasemekana kuwa lenye mazingira rafiki zaidi duniani.

Mnara huu una mitambo 200 ya upepo kwenye paa lake, ambayo hutoa sehemu ya matumizi ya umeme ya jengo hilo. Urefu wa jengo hili ni zaidi ya Big Bens sita pamoja

Mecca Royal Clock Tower

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hoteli na jengo hili lenye urefu wa mita 601 lilijengwa mwaka 2012 na ndio jengo refu zaidi lenye saa duniani.

Inakadiriwa kuwa ujenzi wa jengo hili uligharimu dola bilioni 16

Ping An World Trade Center

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jengo hili lina urefu wa mita 599 na lina ghorofa 115. Jengo hili liko katika wilaya ya kati ya biashara ya Shenzhen na hutumiwa zaidi kwa ofisi za utawala

Lotte World Tower

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jengo la Lotte lina urefu wa mita 555 na Ghrofa 123 uko Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini.

Jengo hili ndio refu zaidi nchini Korea Kusini na hutumiwa kwa hafla nyingi nzuri kama vile kurusha fataki za Mwaka Mpya.

New York World Trade Tower

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jengo la World Trade Center{One} huko mjini New York lilijengwa mnamo 2014 na lina urefu wa mita 541.

Jengo hili limechukua nafasi ya majengo mawili ya World Trade center katika eneo la Manhattan huko New York.

Majengo pacha ya ya World Trade Center yalishambuliwa na al-Qaeda mnamo Septemba 11, 2001 na kuanguka.