Wasichana wadogo mjini Nairobi wanavyokabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Maelezo ya video, Wasichana wadogo mjini Nairobi wanavyokabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Zubeida Yusuf mwenye umri wa miaka 22 ameishi katika kitongoji cha Kibera viungani mwa mji mkuu kwa miaka mingi. Anasema unyanyasaji wa kijinsia umekuwa sehemu ya maisha yake tangu alipokuwa msichana mdogo.

Wanaume wanakuambia maneno ya kudhalilisha kama vile ‘umenona sana...kwani mama yako anafanya kazi katika duka la kuuza nyama? ameiambia BBC kuwa wasichana wanahitaji ujasiri wa hali ya juu kutembea katika mtaa wa Kibera.