Bi. Zarka amekuwa akipigwa na mumewe kwa muda mrefu

Maelezo ya video, Bi. Zarka amekuwa akipigwa na mumewe kwa muda mrefu

Unyanyasaji kwa wanawake ni jambo la kawaida nchini Afghanistan. Utafiti nchini humo ulionukuliwa na Umoja wa Mataifa unasema kuwa asilimia 87 ya wanawake nchini humo hunyanyaswa kisaikolojia, kingono na kimwili.

Katika matukio mabaya zaidi , waume huwashambulia wake zao kwa tindi kali au visu.

Zarka ameolewa kwa miaka 10 na yeye na mumewe wana mtoto wa kiume wa miaka sita.

Mke huyu,28 alikuwa amezoea kupigwa na mumewe lakini hakutegemea kama atadhuru kiasi hicho.

Zarka anatoka katika familia masikini kusini mwa mji wa Kabul karibu na mpaka wa nchi yake na Pakistan.

Zarka hajui kusoma wala kuandika.